Conte aishangaa kikosi chake

TURIN, Italia 

KOCHA wa Inter Milan, Antonio Conte, amesema kikosi hicho kina wachezaje wenye uwezo wa kawaida ambao hawakidhi mahitaji ya klabu hiyo msimu huu.

Conte alisisitiza wachezaji waliopo kikosini hawana uzoefu na hategemei endapo watafanya makubwa asilimia 100.

“Wachezaji hawajabeba taji lolote hadi sasa, utaona hata uzoefu hawana, kikosi cha kawaida mno, kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya na Serie A kinatakiwa kikosi kipana,” alisema kocha huyo wa zamani wa Chelsea.

Miongoni mwa wachezaji wapya Inter Milan ni Romelu Lukaku ambaye hadi sasa amefikisha mabao 14 katika mashindano yote na Alexis Sanchez. 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*