COMING SOON Braza K

Filamu hii inatarajiwa kutoka wiki ijayo katika mfumo wa DVD. Story yake inamhusu Braza K, ambaye anaingiwa na dudu la ajabu ambalo linamtumia kuua watu bila yeye kujua, hata kama akiwa amelala lile dudu linamuingia na kumnyanyua na kufanya uhalifu, watu wanaumiza kichwa kutaka kujua ni nani anayefanya uhalifu huo.

Mwanadada Johari anafanikiwa kumuona Braza K, anamfuatilia, ndipo anapogundua kuwa si yeye halisi anayefanya hivyo.

Imechezwa na Johari Chagula, Braza K na wengine wengi.

ENZI HIZO

BAD BOYS – 1995

Ni filamu ya vichekesho ya Kimarekani iliyoanza kuonekana mwaka 1995. Iliigizwa na wapelelezi, Marcus Burnett (Martin Lawrence) na Mike Lowrey (Will Smith), ambao walipewa jukumu la kufanya uchunguzi wa tukio la wizi wa dawa za kulevya aina ya Heroin, zenye thamani ya dola milioni 100, zilizokamatwa kutoka kundi la mafia na kufichwa katika kituo cha polisi cha Miami.

Hata hivyo, Wizara ya Mambo ya Ndani iliingiwa na shaka kwamba huenda mpango huo ulitelekezwa ndani ya Kitengo hicho cha Ssalama na kuwapiga mkwara kama wakishindwa kurudisha mzigo huo wa dawa za kulevya, kitengo chote kitaondolewa.

Imeongozwa na Michael Bay, imeandaliwa na Jerry Bruckheimer na Don Simpon, imesambazwa rasmi  Aprili 7, 1995.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*