COLEEN ROONEY AWAAGA MARAFIKI ZAKE LONDON

LONDON, England


 

MKE wa straika Wayne Rooney, Coleen Rooney, amenaswa akila bata katika klabu moja ya usiku jijini London ikiwa ni sehemu ya kujiweka sawa kwenda kuungana na mumewe nchini Marekani.

Mwanamama huyo mwenye umri wa miaka 32 na watoto wanne, alinaswa juzi usiku akijiachia na marafiki zake ikiwa ni baada ya mwezi uliopita kuthibitisha safari hiyo ya Marekani, baada ya mumewe kusaini mkataba wa kulipwa  pauni 300,000 na timu ya DC United  yenye makao yake makuu katika jiji hilo kuu la Marekani.

Katika tukio hilo, staa huyo alionekana akifurahia maisha na baadhi ya marafiki zake kabla ya kuwapa mkono wa kwa heri tayari kwenda kuanza maisha mapya nchini Marekani.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*