CLEVELAND HOI KWA WARRIORS, LEBRON BADO TISHIO

LOS ANGELES, Marekani


 

MCHEZO wa kwanza wa fainali ya Ligi Kuu ya Kikapu ya Marekani (NBA), ilichezwa jana ikiwakutanisha wababe Cleveland Cavaliers na Golden State Warriors.

Warriors ambao ni mabingwa watetezi waliianza vizuri safari yao ya kuutetea ubingwa wa msimu uliopita kwa kuwachapa wenzao hao kwa pointi 124-114, lakini hawakuweza kumzuia LeBron James kung’ara.

Licha ya timu yake kupoteza matokeo, Lebron aliye katika kiwango cha juu msimu huu, aliweza kutupia pointi 51 peke yake.

Stephen curry, mshindi mara mbili wa tuzo ya MVP (Mchezaji Bora wa Msimu), alikuwa mwiba mchungu kwa Cavaliers, akiumaliza mchezo akiwa na pointi 29, ukiacha ‘asisti’ zake tisa.

Staa mwingine wa Warriors aliyekuwa moto ni Kevin Durant ambaye aliwatungua Cavaliers pointi 26, akicheza mipira iliyorudi ‘rebound’ mara tisa na kutoa asisti sita.

Mchezo wa pili utachezwa Jumatatu ya keshokutwa, kabla ya mwingine kufuata siku tatu baadaye, yaani Alhamisi.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*