googleAds

Cisse awahofia Tanzania, Kenya

NA MWANDISHI WETU 

KAMA ulidhani Taifa Stars ya Tanzania na Harambee Stars ya Kenya ndiyo timu dhaifu katika Kundi C michuano ya Kombe la Afrika, basi sikiza hiki alichosema kocha mkuu wa Senegal, Aliou Cisse. 

Kocha huyo mzawa ambaye aliichezea Senegal kwa mafanikio, amekiri kwamba Algeria na Simba wa Teranga ndiyo wanaopewa nafasi kufuzu moja kwa moja kutoka Kundi C lakini akatahadharisha kutowapuuza wawakilishi wa Afrika Mashariki; Harambee Stars na Taifa Stars. 

Nahodha huyo wa zamani wa Senegal ambaye pia alisema timu yake haina hofu na watakaowakabili, atakuwa anakutana na Algeria kwa mara ya tatu mfululizo kwenye michuano ya AFCON.

“Hii ni mara ya tatu mfululizo tunacheza na Algeria katika hatua ya makundi,” Cisse aliliambia mtandano wa Cafonline akidhibitisha kocha wa Algeria, Djamel Belmadi ni rafiki yake wa muda mrefu. “Tulikutana 2015 (Equatorial Guinea), 2017 (Gabon) na sasa Misri. Ni historia ndefu kati ya timu hizi mbili.” 

Senegal hawajawahi kushinda taji la Kombe la Afrika licha ya kuwa na wachezaji wenye vipaji lakini wanaamini kufanya vizuri na kukata kiu yao hiyo wakiwa na Sadio Mane, Kalidou Coulibaly na Keita Balde.  


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*