googleAds

Chuji azivutia kasi Simba, Yanga

NA ZAINAB IDDY

KIUNGO wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Athuman Iddi ‘Chuji’, amezipa Simba na Yanga mechi nne tu kujua nani yupo bora zaidi ya mwingine.

Chuji ambaye mbali na kucheza Stars, amezitumikia timu zote hizo kwa nyakati tofauti na kwamba msimu huu ameamua kukaa nje ya soka ili kufanya mambo mengine.

Akizungumza na BINGWA jana, Chuji alisema kwa sasa mashabiki wa timu hizo kila mmoja anaona kikosi chake ni bora zaidi ya kingine jambo ambalo si kweli.

“Haiwezekani timu zote mbili kuwa na ubora sawa, binafsi natoa mechi nne tu za Ligi Kuu kwa kila mmoja baada ya hapo itajulikana nani zaidi.

“Mpira unamambo mengi sana, unaweza kuona Simba bora zaidi Yanga au Yanga bora zaidi ya Simba lakini mwisho yule aliye dhaifu ndio akaja kuwa bingwa mwisho wa msimu,” alisema.

Chuji aliongeza: “Kutokana na mpira kuwa matokeo ya ajabu ndani ya dakika 90, mechi nne anazotoa zitakuja kujieleza Simba na Yanga ipi ni bora zaidi ya mwingine.”


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*