BUFFON: HUYU RONALDO KAMA PELE TU

TURIN, Italia

KIPA mkongwe wa Juventus, Gianluigi Buffon, amemfananisha staa Cristiano Ronaldo na Pele.

Kauli ya mlinda mlango huyo imekuja baada ya Ronaldo kufungwa mara mbili katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Juve katika mchezo wa juzi wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Katika hali ya kushangaza, uzalendo uliwashinda mashabiki wa Juve na kujikuta wakishangilia bao la pili la nahodha huyo wa tiomu ya Taifa ya Ureno.

“Tumemuona Ronaldo kama ambavyo amekuwa siku zote. Mchezaji wa kiwango cha kipekee, ambaye anafanikiwa katika mambo makubwa, sambamba na Lionel Messi,” alisema Buffon.

Matokeo hayo yanawaweka Juve katika hatari ya kung’olewa Ligi ya Mabingwa msimu huu kwani Aprili 11 watakuwa jijini Madrid kucheza mchezo wa marudiano.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*