CHAMBUA AMPA NENO AJIB

>>Akiri akilifanyia kazi, nyota huyo atapendwa kuliko mchezaji yeyote Yanga

NA ADAM MOHAMMED (DSJ)

MCHEZAJI wa zamani wa Yanga, Sekilojo Chambua, amemtaka staa wa timu hiyo, Ibrahim Ajib, kubadilika ili kuwa na madhara zaidi kwa timu pinzani hali inayoweza kumfanya kuwa ‘Mfalme wa Jangwani’.

Akizungumza na BINGWA Dar es Salaam jana, Chambua alisema katika mchezo uliopita wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Welayta Dicha ya Ethiopia kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Ajib hakuwatendea haki Wanayanga.

Katika mchezo huo wa kwanza wa hatua ya mtoano kuwania kutinga makundi, Yanga ilishinda mabao 2-0 wafungaji wakiwa ni Raphael Daudi na Emmanuel Martin.

Chambua alisema katika mchezo huo wa Jumamosi iliyopita, Ajib alikuwa akicheza na majukwaa, hivyo kupoozesha mashambulizi.

Chambua alisema, Ajib ni mchezaji anayetegemewa hivi sasa katika kikosi cha Yanga, lakini kutokana na uwezo alioonesha siku hiyo anatakiwa kubadilika na kuanza kucheza kitimu ili kuipatia matokeo mazuri timu yake.

“Ajib anatakiwa aache kucheza mpira wa majukwaa na kucheza kitimu. Ukweli ni kuwa Ajib anatakiwa abadilike na aongeze bidii ili aweze kuipatia mafanikio timu yake na iweze kusonga mbele katika mechi za kimataifa na Ligi Kuu Bara,” alisema.

Mkongwe huyo aliongeza kuwa mchezo wa marudiano utakaochezwa Ethiopia wiki ijayo, hautakuwa mwepesi kwa Yanga hivyo mchezaji kama Ajib, atalazimika kuonesha kiwango cha hali ya juu ili kuiwezesha timu yake kusonga hatua inayofuata. Inaendelea………….. Jipatie nakala ya Gazeti la #BINGWA

 

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*