CHALZ BABA AREJEA RASMI TWANGA PEPETA

NA MWANDISHI WETU


MWIMBAJI mahiri wa muziki wa dansi, Charles Gabriel ‘Chalz Baba’, amerejea rasmi kwenye bendi yake ya zamani ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’.

Chalz aliondoka Twanga mwaka 2012 na kujiunga na Mashujaa Musica, lakini miaka ya hivi karibu nyota huyo hakuwa na bendi yoyote.

Mmoja wa kiongozi wa Twanga Pepeta aliliambia BINGWA hivi karibuni kuwa, mwimbaji huyo aliyetamba amerejea rasmi kwenye bendi yao.

“Chalz Baba amesharejea Twanga Pepeta ila bado hatujaamua kutangaza ndio maana umemwona kwenye bendi na amevaa sare kama waimbaji wengine,” alisema kiongozi huyo.

Chalz Baba alipokuwa Twanga Pepeta alitunga nyimbo kadhaa zilizofanya vizuri kama Mwana Dar es Salaam na Dunia Daraja.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*