Category: Uncategorized

Mgunda ataka usajili ‘bab kubwa’

ZAINAB IDDY KOCHA wa timu ya Coastal Union ya jijini Tanga, Juma Mgunda, amesema kuwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara anahitaji kuwa na kikosi kipana na cha ushindani ili kuepukana na changamoto alizokutana nazo 2018/19. Katika msimu huu uliofika tamati wiki hii, Coastal Union imemaliza ikiwa katika nafasi ya nane, ikiwa na alama 48 ilizozipata ndani ya mechi […]

Kocha KMC apania kuitafuna Mbao FC

NA GLORY MLAY KOCHA wa KMC, Etienne Ndayiragije, amesema wamejipanga kuitafuna Mbao FC ili kupata ushindi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza. Akizungumza na BINGWA jana, Ndayiragije, alisema anafahamu ugumu wa Uwanja wa CCM Kirumba, lakini ameandaa jeshi lake kukabiliana na hali yoyote. Alisema kuelekea mchezo huo, wamefanya maandalizi ya […]

Pogba, Sanchez wachafua hali ya hewa Man Utd

LONDON, England MASTAA Paul Pogba na Alexis Sanchez, wanadaiwa kuwa chanzo cha kuzuka mgawanyiko kwenye vyumba vya kubadilishia jezi vya Manchester United, kutokana na kiasi kikubwa cha fedha ambacho wanalipwa wanapofunga bao na kutoa ‘asisiti’. Wawili hao wanadaiwa kuwa na mikataba minono katika klabu hiyo ya  Manchester United na ni miongoni mwa wachezaji wanaolipwa fedha nyingi. Kwa mujibu wa gazeti […]

Aussems ataka pointi 15 tu mechi tano Dar

MAREGES NYAMAKA NA GLORY MLAY KOCHA wa Simba, Patrick Aussems, ameshaanza kupigia hesabu ubingwa wa Ligi Kuu Bara huku akihitaji ushindi katika mechi tano kati ya nane walizobakisha. Mbeligiji huo juzi alikiongoza kikosi chake hicho kuibuka na ushindi muhimu wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Bao pekee […]

Makocha wa Liverpool washusha neema Bongo

Elizabeth Joachim,Dar es Salaam Makocha wawili, Anthony Godfrey na Dave Rogers, waliowahi kufundisha timu za vijana wametua kwa ajili ya mafunzo ya soka kwa vijana wadogo nchini. Makocha hao wameletwa na kituo cha 7 Elite Academy kutoka Marekani, chini ya raisi wake Reggie Wilson, ambapo wanashirikiana na watanzania wengine, akiwemo mchezaji wa zamani wa Simba na Yanga, Amri Kiemba. Akieleza […]

CHEKIBUDI Mkongwe wa filamu aliyekaa benchi kusubiri soko lisimame YUKO WAPI

NA JEREMIA ERNEST UIGIZAJI ni sehemu tu ya kipengele katika sanaa ambacho kimeibua mastaa kibao waliojizolea umaarufu kutokana umahiri wao wa kuigiza kulingana na kazi wanazofanya. Wasanii wengi wenye majina makubwa hapa nchini wameibukia kwenye tasnia hiyo na miongoni mwao ni Mohamed Nurdin ‘Chekibudi’ ambaye pia alikuwa mchezaji wa mpira wa miguu. Msanii huyu alipata umaarufu zaidi mwaka 1999 wakati […]

Kenny Guitar Mkali wa gitaa aliyeupaisha wimbo ‘You Are The Best’ wa Ommy Dimpoz

NA CHRISTOPHER MSEKENA MIONGONI mwa wimbo unaokonga mioyo ya watu kwa sasa hapa Bongo ni You Are The Best wa mwimbaji, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, iliyonogeshwa kwa gitaa asili ya Hispania na kufanya wimbo huo uwe burudani kwa yeyote anayesikiliza. BINGWA lilikutana na mpiga gitaa la solo, Kennedy Masanja ‘Kenny Guitar’, ambaye ndiye alipiga chombo hicho kwenye wimbo huo ambao […]

Dereva aieleza mahakama alivyokuwa akichukua fedha kwa mhasibu kumpelekea Malinzi

Kulwa Mzee, Dar es Salaam Aliyekuwa dereva wa Rais wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi, Steven John, ameileza mahakama alikuwa anachukua fedha kutoka kwa aliyekuwa mhasibu wa shirikisho hilo, Hellen Ndaro na kumpelekea Malinzi. Aidha, dereva huyo ambaye ni shahidi katika kesi hiyo ya utakatishaji fedha inayomkabili Malinzi na wenzake, baada ya kujitambulisha alishindwa […]