Category: Sport Extra

Klopp: Mkizidi kunifurahisha nitawakumbatia mpaka basi

MERSEYSIDE, Liverpool KOCHA wa timu ya Liverpool, Jurgen Klopp, amewapasha wachezaji wake kwa kuwaambia kwamba kama wanataka kuuona upendo wake kwao, basi hawana budi kupambana uwanjani na kumpa raha. Bosi huyo wa majogoo hao wa jiji alionekana ni mwenye Furaha, huku akiwakumbatia wachezaji wake mara baada ya kumaliza mchezo wao wa ligi dhidi ya Chelsea kwa ushindi wa mabao 2-1. […]

Conte amtaja mchawi wake Chelsea

LONDON, England KOCHA mkuu wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte, amefunguka na kusema kwamba kiungo wake, Cesc Fabregas, ndiye anayempa tabu ndani ya kikosi hicho hadi sasa. Conte hakumpanga Mhispania huyo kwenye kikosi cha kwanza kilichocheza mtanange wa ufunguzi wa Ligi Kuu England, na amekiri kuwa alipata wakati mgumu wa kumpanga kwenye kikosi cha kwanza kilichofungwa mabao 2-1 na Liverpool […]

Torres: Huu ni wakati mzuri wa kupambana na Barcelona

MADRID, Hispania MSHAMBULIAJI mkongwe wa klabu ya Atletico Madrid, Fernando Torres, ameweka wazi morali ya hali ya juu aliyonayo kwa kusema kuwa, wakati huu ndio mzuri kupambana na Barcelona kwenye mtanange wao wa La Liga wiki hii. Torres aliiongoza Madrid kuinyuka klabu ya Sporting Gijon mabao 5-0, huku wapinzani wao watakaokutana nao mapema wiki hii, Barca wakiitandika Leganes mabao 5-1 […]

Man United wachapwa mechi ya tatu mfululizo

LONDON, England Manchester United wamepoteza mechi yao ya tatu mfululizo, baada ya kuchapwa mabao 3-1 dhidi ya Watford kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa jana. Etienne Capoue alifunga bao lake la nne msimu huu katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Vicarage Road, kabla ya Marcus Rashford kusawazisha baada ya mapumziko. Mabadiliko yaliyofanywa na kocha Walter Mazzarri ya kumwingiza Juan […]

Shearer aivulia kofia Arsenal

LONDON, England ALAN Shearer ameisifia Arsenal baada ya kuichapa Hull City kwenye mchezo wa Jumamosi ya wiki iliyopita. Gunners walishinda mabao 4-1 kwenye Uwanja wa KC dhidi ya kikosi ambacho mchezaji wao, Jake Livermore alitolewa kwa kadi nyekundu. Lakini Shearer alisema kadi nyekundu imeleta mabadiliko madogo kwenye matokeo. Akiwa kama mchambuzi wa mechi hiyo kwenye moja ya vituo vya televisheni […]

BEST FRIENDS Mastaa hawa ni maswahiba kinoma

LONDON, England URAFIKI ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Kwa upande mwingine, wapo wanaoamini kuwa rafiki ni zaidi ya ndugu wa damu. Hivi ni kweli? Sina hakika juu ya hilo, ila naamini kuwa kuna baadhi ya mambo huwezi kuyaweka wazi kwa kaka, dada, mjomba, ila utakuwa huru zaidi kumwambia rafiki yako wa karibu. Kutokana na hilo, ni ngumu […]

Hawa wataula kufungiwa Real Madrid kusajili

MADRID, Hispania  TIMU za Real na Atletico Madrid  wiki iliyopita zilianza rasmi kutumikia adhabu yake ya kufungiwa kwa muda wa miaka miwili kutofanya usajili iliyopewa na Shirikisho la Soka Ulaya, UEFA. Vigogo hao wa soka Hispania wanatumikia adhabu hiyo baada ya UEFA kuvitia hatiani  kwa kukiuka kanuni za usajili za kimataifa kwa kusajili  wachezaji wenye umri mdogo. Adhabu hiyo inaonekana […]

Waliong’ara na waliochemka Ligi ya Mabingwa Ulaya

LONDON, England MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya kwanza ilihitimishwa juzi ambapo ilishuhudia miamba mbalimbali ikichuana kutafuta ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa taji hilo kubwa barani humo. Katika mitanange hiyo ambayo ilipigwa mwanzoni na katika mwa wiki hii ipo miamba ambayo  ilifanya vizuri na huku mingine ikijikuta ikiangukia pua. Hata hivyo, pamoja na miamba mingine  […]

Ushauri wa Scholes kwa Paul Pogba

MANCHESTER, England PAUL Scholes amefunguka kuwa mchezaji ghali wa Manchester United, Paul Pogba, hachezi sawa na mtu mwenye thamani ya pauni mil 86. Haya yamekuja baada ya Pogba, aliyeanza vyema michezo ya Premier League kuchemka katika mechi mbili za hivi karibuni, ikiwemo ya Uropa, United waliyochezea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Feyenoord. Licha ya nyota kadhaa wa United kucheza […]