Category: Sport Extra

Rashford ampa somo Ibrahimovic

LONDON, England KINDA wa Manchester United, Marcus Rashford, ni kama kampa somo staa mwenzake Zlatan Ibrahimovic akisema kuwa anatakiwa kuwa na ndoto za ubingwa kutokana na kuwa anataka kujifunza mengi kutoka kwa straika huyo. Ibrahimovic alijiunga na Man United akitokea katika timu ya Paris Saint-Germain kabla ya msimu huu kuanza na kwa sasa Rashford anajivunia kupata nafasi ya kujifunza kutoka […]

Messi huenda akaitema Barcelona

BARCELONA, Hispania STRAIKA Lionel Messi ni dhahiri hafikirii kustaafia soka Barcelona licha ya kuwa mhimili wa klabu hiyo ya Hispania na inasemekana angependa kurejea kwa Argentina muda ukifika. Hatua hiyo inaelezwa ni baada ya Messi kutaka kipengele cha kumruhusu kuihama Barcelona kwenye mkataba wake mpya. Hata hivyo, mshindi huyo mara tano wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia, Ballon d’Or, […]

Moses ajisababishia matatizo Nigeria

LAGOS, Nigeria RIPOTI zimeibuka juu ya staa wa klabu ya Chelsea, Victor Moses, kuwa yupo kwenye hatari ya kufungiwa kucheza mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Leicester City, baada ya kugomea wito wa kuitumikia timu ya taifa ya Nigeria. Kwa mujibu wa mtandao wa soka wa Nigeria, Complete Sports Nigeria, shirikisho la soka la nchi hiyo haliamini kama winga […]

England yatamba chini ya kocha mpya

LONDON, England KOCHA wa muda wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate, ameanza vizuri kibarua chake hicho kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Malta, kwenye mchezo wa kufuzu kucheza michuano ya Kombe la Dunia 2018, uliopigwa usiku wa kuamkia jana kwenye dimba la Wembley. Southgate alikabidhiwa timu hiyo mara baada ya Sam Alardyce kubwaga manyanga hivi karibuni, ambapo […]

Nani atapotea ndani ya kizazi hiki cha dhahabu?

LONDON, England JARIDA maarufu la soka na lenye heshima duniani la World Soccer liliwahi kuwaorodhesha wachezaji makinda wenye kiwango cha hali ya juu mwaka 2007, ambapo baadhi ya waliokuwepo walikuwa Juan Mata, Mesut Ozil, Karim Benzema, Ivan Rakitic, Sergio Aguero na Gareth Bale, ambao walifanikiwa kunyakua mamilioni, kushinda tuzo kubwa michezoni pamoja na kujizolea umaarufu duniani kote. Makinda wengine wa […]

Woods athibitisha kurejea mzigoni

California, Marekani NYOTA wa gofu, Tiger Woods, amethibitisha kurejea uwanjani kwenye michuano ya Safeway Open, itakayofanyika mjini California, Marekani, kuanzia wiki ijayo. Tiger, mwenye umri wa miaka 40, alikusudia kushiriki kwenye michuano ya Silverado mjini Napa, baada ya kukaa nje tangu Agosti, mwaka jana. Woods amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mgongo kwa miaka kadhaa, hivyo amefanyiwa upasuaji mara tatu katika […]

Hamilton adai kuna hujuma

Kuala Lumpur, Malaysia Lewis Hamilton ametema cheche baada ya injini ya gari lake kuwaka moto kwenye mashindano ya Malaysia Grand Prix. Dereva huyo wa England, Hamilton, ambaye amenyakua ubingwa wa dunia mara tatu, ameilaumu timu yake ya Mercedes, baada ya injini hiyo kulipuka akiwa amebakiza kona 15 kumaliza mashindano hayo. Badala yake, madereva wa Red Bull, Daniel Ricciardo na chipukizi […]

Miezi 12 ya Klopp Liverpool Ana tofauti na Rodgers?

MERSEYSIDE, England MWISHONI mwa wiki iliyopita, Kocha Jurgen Klopp amesherehekea kutimiza mwaka mmoja tangu apewe kibarua cha kuinoa Liverpool, lakini Klopp amefanya kitu gani cha tofauti na kocha aliyemrithi kwenye nafasi hiyo, Brendan Rodgers? Klopp alirithi mikoba ya Rodgers, Oktoba 8 mwaka 2015, Reds ikiwa nafasi ya 10 baada ya kushinda mechi tatu za Ligi Kuu England kati ya nane. […]