Category: Sport Extra

Griezmann amchefua bosi Atletico

MADRID, Hispania RAIS wa Atletico Madrid, Enrique Cerezo, ameeleza kusikitishwa kwake na uamuzi wa Antoine Griezmann, kusema ataondoka klabuni hapo. Griezmann aliitangaza hatua yake hiyo, akisema huu utakuwa msimu wake wa mwisho akiwa na Atletico aliyojiunga nayo mwaka 2014 akitokea Real Sociedad. “Ni zaidi ya hasira, nimesikitishwa. Nilifikiri Antoine angekuwa na muda mrefu Atletico,” alisema bosi huyo.

Ugonjwa wa tumbo wamkosesha Sarri safari ya Marekani

LONDON, England KOCHA Maurizio Sarri amelazimika kuikosa safari ya Chelsea kwenda kutembelea jumba la makumbusho la Holocaust Memorial lililopo nchini Marekani, baada ya kukumbwa na ugonjwa wa tumbo. Sarri alikutana na hali hiyo wakati timu yake hiyo ya Chelsea ikianza ziara ya kujiandaa na msimu ujao, ambapo mapema wiki hii walikipiga na New England Revolution katika mchezo wa krafiki. Hata […]

De Jong aagwa kifalme Ajax

AMSTERDAM, Uholanzi KIUNGO wa Ajax, Frenkie de Jong, ameagwa kifalme na mashabiki wa timu hiyo wakati akijiandaa kwenda kujiunga na klabu yake mpya ya Barcelona. Kiungo huyo Mholanzi alikuwa na mchango mkubwa hadi Ajax ilipofanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya nchi hiyo, Eredivisie, na aliiwezesha kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Ulaya. Wakati ada yake ya usajili ya pauni […]

Vidal anasa kwa kimwana mtunisha misuli

MADRID, Hispania NYOTA wa Barcelona, Arturo Vidal, amenasa kwa kimwana mtunisha misuli raia wa  Colombia, Sonia Isaza, wakionekana kuponda raha katika fukwe za kifahari nchini Marekani. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, kimwana huyo alitupia picha juzi kwenye mtandao wake wa kijamii wa Istagram akiwa na nyota huyo wakiwa wanaota jua katika ufukwe mmoja uliopo California. Vidal alishawahi kutangaza kutengana […]

Pogba, Lukaku, Sanchez wapigwa ‘kibuti’ Man Utd

LONDON, England MASHABIKI wa Manchester United wamepiga kura kuhusu uwepo wa mastaa wao, Paul Pogba na Romelu Lukaku ndani ya klabu hiyo na wengi wao wamewapiga kibuti, wakisema kuwa ni bora waondoke zao. Kura hizo zilizoendeshwa na gazeti la  The Sun, zimekuja wakati kocha wao, Ole Gunnar Solskjaer, akiwa tayari ameshawapa taarifa za kupitishwa panga kubwa kwa baadhi ya nyota […]

MTACHAKAA

NA MAREGES NYAMAKA, MWANZA MABINGWA watetezi Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba,  jana wameendeleza ubabe baada ya kuichapa KMC mabao 2-1 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza. Simba walipata bao la kwanza dakika ya 22, kupitia Emmanuel Okwi, aliyeunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Chama baada ya John Bocco kufanyiwa madhambi na beki wa KMC Yusuf Ndikumana. Simba imeibukana ushindi […]

Makambo aiponza Yanga Iringa

KOCHA Mkuu wa Lipuli FC, Samwel Moja, amefichua siri ya kilichoimaliza Yanga kuwa ni kuzoea mfumo wa kumtegemea zaidi Heritier Makambo, kufunga mabao. Lipuli juzi iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Samora, Iringa.  Akizungumza na BINGWA jana, kocha huyo alisema alikuwa akiifuatilia Yanga kwa muda mrefu […]