Category: Sport Extra

Angalau Taifa Stars imetuondolea ‘gundu’

NA ZAINAB IDDY KUMEKUWA na maneno mengi yanayozungumzwa juu ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, inayoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon2019) nchini Misri. Maneno hayo yamekuja kutokana na matokeo yasiyoridhisha wanayoyapata Stars tangu kuanza kwa michuano hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita. Ikiwa Kundi C, Stars imecheza mechi mbili na kupoteza zote, hivyo kushika mkia, ikiwa […]

TUTOKE AFCON, TUFIKIRIE CHAN

NA MWANDISHI WETU MICHUANO ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon 2019), inaendelea, Cairo nchini Misri huku timu ya Tanzania, Taifa Stars, ikipoteza mwelekeo wa kutinga 16 bora. Kitendo cha kupoteza michezo miwili ya Kundi C, tunaifanya Taifa Stars kuaga michuano hiyo, licha ya kusalia na mchezo mmoja dhidi ya Algeria utakaochezwa Jumatatu ijayo  kwenye Uwanja wa 30 June nchini humo. […]

KELVIN YONDANI; Beki Yanga aliyetamani kuwa mfanyabiashara

NA GLORY MLAY KILA mtu katika maisha, anajaribu kufanya shughuli mbalimbali ili aweze kufikia ndoto na malengo yake aliyojiwekea. Lakini wengi wao wameshindwa kufikia malengo yao kutokana na changamoto wanazokumbana nazo, hivyo kuamua kufanya shughuli nyingine. Kelvin Yondani, ni beki wa Yanga na Taifa Stars, ambaye alikuwa na ndoto ya kufanya biashara, lakini hakuweza kufikia malengo yake, baada ya kunogewa […]

Zahera yupo sahihi kwa Kamusoko

NA ZAINAB IDDY HIVI sasa ndani ya klabu ya Yanga, kumekuwa na makundi mawili yenye mtazamo tofauti juu ya kurejeshwa au kutorejeshwa kikosi kwa kiungo, Thabani Kamusoko. Mgawanyiko huo umekuja baada ya ripoti ya kocha Mwinyi Zahera, kuonyesha haimuhitaji kwa kile kilichodaiwa ameshuka kiwango, umri mkubwa pamoja na majeraha ya mara kwa mara aliyonayo. Wakati ripoti ya Zahera ikionyesha kutomuhitaji, […]

KMKM walivyopania kukinukisha Ligi ya Mabingwa Afrika

NA IBRAHIM MAKAME, ZANZIBAR KLABU ya KMKM iko katika harakati ya kuiboresha timu yao ili iweze kufanya vyema msimu ujao wa Ligi Kuu Zanzibar na Ligi ya Mabingwa Afrika baadaye mwaka huu.   Katika kuhakikisha hilo linatimia, kocha wa KMKM, Ame Msimu Khamis, amesema amepanga mkakati mzuri utakaowezesha timu hiyo kuwa tishio msimu mpya unaokuja. Usajili mpya 2019/2020 Khamis anasema […]

Samatta: Misri imetuonyesha njia yakutokea makundi

NA WINFRIDA MTOI NAHODHA wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, amesema mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Misri umewazindua kufahamu ugumu watakaokutana nao katika mechi za hatua ya makundi ya AFCON. Taifa Stars juzi ilicheza na Misri ambao ni wenyeji wa michuano ya AFCON mwaka huu katika Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandraia na kufungwa bao 1-0. Akizungumza baada […]

Matawi Azam roho kwatu kumnasa Ndayiragije

NA WINFRIDA MTOI KOCHA mpya wa Azam, Etienne Ndayiragije, amesaini mkataba wa miaka miwili kwa ajili kuifundisha timu hiyo. Ndayiragije amesaini mkataba wiki hii, baada ya kuwasili  nchini, akitokea kwao Burundi na kupokewa kwa shangwe na matawi ya klabu ya Azam. Kocha huyo, amechukua nafasi ya Hans van de Pluijm, aliyetimuliwa na uongozi wa Azam kutokana matokeo mabaya ya timu […]

KELVIN JOHN ; Kinda Serengeti Boys aliyetamani kuwa tabibu wa akina mama

NA GROLY MLAY LICHA ya timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, ‘Serengeti Boys’ kufanya vibaya katika michuano ya Kombe la Vijana Afrika (U-17 Afcon), mshambuliaji wa kikosi hicho, Kelvin John, ndiye aliyeonekana kivutio kutokana na uwezo wake wa kusakata kabumbu. Kutokana na kiwango alichoonyesha katika michuano hiyo, kilimfanya Kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike, kumwiita […]

Aliyetemwa Harambee Stars atoa neno

PARIS, Ufaransa LICHA ya kutemwa katika kikosi cha Harambee Stars ya Kenya, Christopher Mbamba, anamatumaini timu hiyo itafika mbali katika michuano ya Kombe la Afrika. Mbamba anayekipiga na timu ya IK Oddevold inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Sweden, ni miongoni mwa wachezaji nne waliotemwa na kocha mkuu, Sebastien Migne, katika kikosi cha wachezaji 23 kabla ya kuanza michuano hiyo […]

Burundi yawakamata wabaya wa Taifa Stars

DOHA, Qatar ALGERIA ambao wapo kundi moja na Taifa Stars katika michuano ya AFCON, walilazimishwa sare ya bao 1-1 na Burundi maarufu Intamba Mu Rugamba katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Al Sadd nchini Qatar. Baghdad Bounedjah aliipatia bao la kwanza Algeria inayofahamikia kama Mbweha wa Jangwani dakika ya 68 baada ya timu zote kumaliza kipindi cha […]