Category: michezo kimataifa

LIGI YA MABINGWA AFRIKA WANAUME 15 WALIVYOTINGA RAUNDI YA KWANZA

CAIRO, Misri KIVUMBI cha Ligi ya Mabingwa Afrika kilianza Februari 10 na kinatarajiwa kumalizika Novemba 5, mwaka huu. Tayari jumla ya michezo 15 imeshachezwa tangu kuanza kwa mashindano hayo makubwa barani Afrika kwa ngazi ya klabu. Kwa mujibu wa ratiba, wababe hao watapepetana katika mechi za raundi ya kwanza zitakazoanza kuchezwa Machi 10-12 na 17-19. Miongoni mwa mechi kali zilizovuta […]

DAKIKA 7 ZILIVYOWANYIMA TP MAZEMBE MIL 200 ZA SUPER CUP

PRETORIA, Afrika Kusini MWISHONI mwa wiki iliyopita, mashabiki wa soka walipata burudani ya kutosha kwa kushuhudia mchezo mkali wa michuano ya Super Cup kati ya Mamelodi Sundowns na TP Mazembe. Mazembe waliingia kwenye mchezo huo wakiwa mabingwa watetezi, kwani ndio waliochukua taji hilo mwaka jana. Lakini, hawakuwa na kibarua chepesi kulitetea taji lao hilo, kwani walikuwa wakivaana na mabingwa watetezi […]

SUAREZ- BARCA IMETOLEWA? TULIENI VITA BADO MBICHI

CATALONIA, Hispania STRAIKA wa klabu ya Barcelona, Luis Suarez, amesema bado wana matumaini ya kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, licha ya kichapo cha mbwa mwizi walichokipata kutoka kwa PSG wiki iliyopita. Mabingwa hao watetezi wa La Liga walinyukwa mabao 4-0 na PSG kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora uliopigwa nchini Ufaransa. Kutokana na kichapo […]

KOMBE LA DUNIA 2018 ‘WAHUNI’ URUSI WALIVYOJIPANGA KUTISHIA USALAMA

MOSCOW, Urusi KIKUNDI cha wahalifu nchini Urusi kimedai  ‘kitazingua’ wakati wa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2018 zitakazofanyika katika ardhi hiyo. Hilo limeibua shaka kubwa hasa kwa Shirikisho la Soka Ulimwenguni (Fifa) ambalo limekua likisisitiza hali ya usalama katika michuano yake hiyo. “Kwa wengine itakuwa ni sherehe ya soka lakini wengine wataiona ni sherehe ya vurugu,” alisema mtu […]

NASHANGAZWA KUONA WIJNALDUM ANAJARIBIWA LIVERPOOL

Na Kelvin Lyamuya USIKU wa Jumamosi kuamkia jana Jumapili kulikuwa na sherehe za mashabiki wa Liverpool, ni kama ulikuwa mchezo wa mwisho wa ligi na ubingwa ulitua Anfield. Hatari. Kelele hazikuwa kwa sababu ya ubingwa, lakini ile ilikuwa ni furaha ya kuwa juu ya mahasimu wao wakubwa, Manchester United. Ni kama mashabiki wa Spurs wanavyoshangilia kila mwisho wa msimu wanapomaliza […]

PETER LIM; BILIONEA WA SINGAPORE ANAYEIMALIZA VALENCIA

MADRID, Hispania BILIONEA Peter Lim ametumia fedha nyingi kujaribu kurejesha makali ya Valencia ambayo yameonekana kupotea katika miaka ya hivi karibuni. Hata hivyo, bado ndoto ya mmiliki huyo wa Valencia mwenye utajiri unaotajwa kufikia Dola za Marekani bilioni 2.3, imeshindwa kutimia. Alitumia kitita cha euro milioni 200 kuinunua klabu hiyo pamoja na kuifanyia marekebisho kadhaa. Bilionea huyo hajaonekana uwanjani kuitazama […]

SIRI YA KIPAJI CHA KANTE YAGUNDULIKA

LONDON, England MKURUGENZI wa soka wa klabu ya Everton, Steve Walsh ambaye alimwibua kiungo mkabaji wa Chelsea, N’Golo Kante, amefafanua hatua alizozitumia kuibua vipaji na kujizolea umaarufu alipokuwa kwenye klabu ya Leicester City misimu kadhaa iliyopita hadi timu hiyo iliponyakua ubingwa wa Ligi Kuu England. Walsh alinyakuliwa na Everton majira yaliyopita ya kiangazi, baada ya mabosi wa klabu hiyo kuridhishwa […]

GUARDIOLA AKIJICHANGANYA TU KUMWACHA AGUERO, AMEUMIA

MANCHESTER, England NI wazi maisha ya straika Sergio Aguero ndani ya klabu ya Manchester City yameanza kuingiwa na shaka baada ya ujio wa straika wa Kibrazil, Gabriel Jesus. Aguero alijikuta akipigwa benchi akiwa shahidi wa kiwango cha hali ya juu alichokionesha kinda huyo ndani ya mechi mbili za mwisho, moja ya FA na nyingine ya Ligi Kuu England dhidi ya […]

CARRAGHER ‘AMVAMIA’ MMILIKI WA LIVERPOOL

MERSEYSIDE, Liverpool MMILIKI wa klabu ya Liverpool, John Henry, ameanza kuonja joto ya jiwe kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo waliochukizwa na kutoona mchezaji yeyote akisajiliwa kwenye dirisha dogo la usajili la Januari. Bosi huyo wa Kimarekani aliwakera zaidi wanazi wa Liver pale walipoona ‘tweet’ yake kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, ikihusu mchezo wa Super Bowl unaochezwa nchini Marekani, […]