Category: michezo kimataifa

MESSI, RONALDO WAKITELEZA TU KANE KAPETA

LONDON, England KWA sasa katika ulimwengu wa soka kuna wachezaji wawili ambao wanautikisa ulimwengu kwa kupata mafanikio ya hali ya juu wakiwa na klabu zao na hata timu za mataifa wanayotoka.   Nyota hao ni mastraika Cristiano Ronaldo ambaye anaichezea Real Madrid na timu ya Taifa ya Ureno na Lionel Messi wa Barcelona, ambaye pia ni nahodha wa timu ya […]

UMELISIKIA KOMBORA LA OZIL KWA WAKONGWE ARSENAL?

  LONDON, England NYOTA Mesut Ozil amewafungukia ‘live’ wachezaji wa zamani wa Arsenal ambao wamekuwa wakiiponda timu, akiwaambia waache kuropoka na badala yake waiunge mkono klabu hiyo. Arsenal wameanza vibaya msimu huu wa Ligi Kuu England, hasa baada ya kichapo cha mabao 4-0 walichokipata katika mchezo uliopita dhidi ya Liverpool. Matokeo hayo yamewafanya Gunners kubaki kwenye nafasi ya 16, wakiachwa […]

ZIFAHAM KLABU ZILIZOVUNJA REKODI SOKO LA USAJILI

  LONDON, England KIPINDI cha majira ya kiangazi mwaka huu kimetuonesha jinsi gani mchezo wa soka ulivyoingia kwenye zama mpya kabisa za usajili wa wachezaji baada ya Neymar kuwa nyota ghali duniani aliyesajiliwa kwa kiasi cha fedha chenye tarakimu tatu (100+) kabla Ousmane Dembele na Kylian Mbappe hawajafuatia. Wakati kukiwa hamna timu yoyote ya Ligi Kuu England iliyofanya usajili wa […]

MAJANGA HAYA HAYATAWAACHA BARCA SALAMA

CATALONIA, Hispania DIRISHA la usajili wa majira haya ya kiangazi limekuwa chungu sana kwa klabu ya Barcelona na pigo kubwa zaidi ni jinsi ilivyoshindikana kusajili staa yeyote katika siku ya mwisho ya usajili. Kwa muda wote wa dirisha la usajili, Barca ilikuwa ikikiona cha moto kwa wachezaji ambao walikuwa wakiwatamani na kama hiyo haitoshi wakashuhudia Neymar akisepa zake PSG bila […]

CHAMBERLAIN ACHEKELEA KUTUA LIVERPOOL, KLOPP AKUMBUSHIA BALAA LAKE

MERSEYSIDE, Liverpool BAADA ya kukamilisha dili la uhamisho wake wa kutua katika klabu ya Liverpool akitokea Arsenal, kiungo Alex Oxlade-Chamberlain, ameonesha wazi furaha yake ya kutinga uzi wa majogoo hao msimu huu. Chamberlain alitangazwa rasmi kuwa mchezaji halali wa Liverpool jana mchana, baada ya klabu hiyo kukubali kulipa pauni milioni 35 za uhamisho wake, akisaini mkataba wa miaka mitano ambapo […]

TETESI ULAYA; GUARDIOLA AMTEGEA SANCHEZ MWAKANI

Guardiola amtegea Sanchez mwakani MANCHESTER, England KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola, amemkosa Alexis Sanchez, lakini amepanga kumrudia pindi dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa mwakani. Taarifa zilizopo ni kwamba, Man City watajaribu kumsajili Sanchez kwa mkopo Januari. Bado kidogo Everton wangembeba Vermaelen MERSYSIDE, England EVERTON walitaka kumchukua beki wa Barcelona, Thomas Vermaelen, lakini wababe hao wa La Liga waligoma. Imeripotiwa kwamba, Everton walimtaka […]

ZIZZOU CHANZO MADRID KUMKOSA MBAPPE

MADRID, Hispania HUENDA nyota Kylian Mbappe angekuwa mchezaji wa Real Madrid kwa sasa kama si Zinedine Zidane kutolewa kwenye majukumu ya kukinoa kikosi cha vijana klabuni hapo. Zizou alihamishwa kutoka kwenye benchi la ufundi la makinda wa Castila na kupewa majukumu ya kuwa msaidizi wa Carlo Ancelotti, jambo ambalo lilisababisha Mbappe kusita kwenda Madrid. “Kama Zidane angebaki na kuwatazama makinda […]

MKONGWE ALDO AMFUATA MCGREGOR KISA MAYWEATHER

LONDON, England BINGWA wa zamani wa ‘kick boxing’, Jose Aldo, amepanga kuhamishia makali yake katika ulingo wa ‘boxing’ kama alivyofanya Conor McGregor. McGregor, ambaye ni staa wa ngumi na mateke, hivi karibuni alipigana pambano lake la kwanza la boxing dhidi ya Floyd Mayweather, licha ya kupoteza katika raundi ya 10. Pambano hilo limemvutia Aldo, ambaye anaamini hata yeye anaweza kupanda […]

SHARAPOVA ATINGA RAUNDI YA TATU US OPEN

WASHINGTON, Marekani STAA wa tenisi, Maria Sharapova, ametinga raundi ya tatu ya michuano ya US Open kwa kumfunga Timea Babos. Katika mchezo huo, Sharapova aliibuka kidedea kwa ushindi wa seti 6-7 (4-7) 6-4 6-1. Sharapova, aliyekuwa na skendo ya kutumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni, alilazimika kutumia nguvu ya ziada kumshinda Babos, ambaye alionekana kujipanga. Baada ya ushindi huo, mwanadada Sharapova […]

KUMBE HATA FERGUSON ANAIOGOA MADRID

MADRID, Hispania KIKOSI cha sasa cha Real Madrid kimeonekana kumtisha kocha wa zamani wa Manchester United, ambapo amesema haitakuwa rahisi kwa timu nyingine kutamba kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Katika michuano ya mwaka huu, Madrid wamepangwa na Kundi H wakiwa na Borussia Dortmund, Tottenham na APOEL. Ferguson alisema ni kweli Juventus wako sawa kwa sasa, lakini kuivua Madrid taji la […]