Category: michezo kimataifa

RONALDO ACHEKELEA USHINDI LIGI YA MABINGWA

  MADRID, Hispania KWA lugha nyingine unaweza kusema ni kama anachekelea ushindi baada ya straika, Cristiano Ronaldo, kusema michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ndiyo saizi yao, baada ya usiku wa kuamkia jana kuanza vyema kutetea taji lao katika michuano hiyo. Katika mchezo huo mshindi huyo wa tuzo ya Ballon d’Or, alifanikiwa kufunga mabao mawili ambayo yaliwafanya wenyeji hao kuondoka […]

UKITAKA KUSHUHUDIA ‘LIVE’ FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA BEI YA TIKETI HII HAPA

  ZURICH, Uswisi SHIRIKISHO la Soka Duniani (FIFA), limeweka hadharani viingilio vitakavyotumika kununua tiketi katika michezo ya Kombe la Dunia itakayopigwa nchini Urusi mwakani. Viingilio hivyo vimepanda gharama tofauti na ilivyokuwa kwenye Kombe la Dunia ambazo zilifanyika nchini Brazil mwaka 2014. Hata hivyo, viwango hivyo vinaonekana kulalamikiwa na wadau wengi wakidai ni vikubwa ikizingatiwa uchumi wa dunia umeporomoka. Gharama ya […]

CONTE: AZPILICUETA HUYU SI WA MCHEZO MCHEZO

KOCHA Antonio Conte ni kama amemvulia kofia staa wake, Cesar Azpilicueta, akisema si wa mchezo mchezo, baada ya kusema kuwa ni kati ya mabeki bora wa kati duniani. Staa huyo wa timu ya Taifa ya Hispania kwa sasa anaonekana kuwa roho katika safu ya ulinzi na pia juzi alikuwa miongoni mwa wafungaji walioipa ushindi  Chelsea wa mabao  6-0  dhidi ya […]

KUMBE ARSENAL WANA JESHI LIGI YA MABINGWA

LONDON,England MSIMU huu timu ya  Arsenal haitashiriki katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwa 1997. Hii ni kutokana na kwamba, Gunners walishindwa kufuzu michuano hiyo baada ya kushika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu England msimu uliopita. Kwa kushika nafasi hiyo msimu huu, kocha wao,  Arsene Wenger, atakiongoza kikosi hicho kwenye […]

KASI YA OKWI YAWATISHA WANAJESHI

NA WINFRIDA MTOI UCHEZAJI wa mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi, umeonekana kuwatisha wengi, kikiwamo kikosi cha timu inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa, Ruvu Shooting.   Hivi karibuni Okwi alifanya mambo makubwa akiwa na timu yake ya Taifa ya Uganda, alipoifungia bao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Misri, kwenye mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia […]

TSHISHIMBI AWA MTAJI YANGA

NA EZEKIEL TENDWA KILA mtu ana nyota yake hapa duniani, kama ilivyo kwa kiungo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi, ambaye amegeuka kuwa mtaji kwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kutokana na kandanda lake alilolionyesha tangu alipotua Jangwani. Unajiuliza kivipi? Iko hivi! Tangu aliposajiliwa na Yanga, kiungo huyo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), amekuwa dili […]

HAPONI MTU

  NA EZEKIEL TENDWA HAPA Okwi, Niyonzima na Bocco, unaponaje kwa mfano? Lakini vipi kwa upande wa Azam, kule wakiwa na Mbaraka Yusuph, huku Himid Mao na pale Yahaya Mohamed, inakuwaje hapo? Ni wazi haponi mtu kwenye Uwanja wa Azam Complex, jijini Dar es Salaam leo. Hivyo ndivyo hali itakavyokuwa kwenye uwanja huo, unaomilikiwa na Azam FC, pale wenyeji watakapowakabili […]

MASTAA WATAKAOYABEBA MATAIFA YALIYOFUZU KOMBE LA DUNIA 2018

LONDON, England MPAKA sasa mataifa tisa yameshajihakikishia kushiriki fainali za Kombe la Dunia za mwakani zitakazofanyika nchini Urusi. Mbali na wenyeji ambao hupita moja kwa moja, kuna Brazil, washindi mara tano wa fainali hizo, Ubelgiji, Iran, Mexico, Japan, Saudi Arabia, Hispania na Korea Kusini, ambao hii ni mara yao ya tisa mfululizo. Lakini je, ni wachezaji gani waliofanya kazi kubwa […]

WALIKATAA OFA NONO KISA WANAZIPENDA TIMU ZAO

LONDON, England KATIKA soko la usajili lililopita, yapo yaliyokuwa gumzo hasa filamu ya Barcelona na Philipe Coutinho, PSG na Neymar na hata ile iliyomhusisha kinda Kylian Mbappe na timu vigogo. Mbrazil Neymar alifanikiwa kutimkia Ufaransa kujiunga na mabosi wa jijini Paris, PSG, ambapo pia wamemchukua Mbappe mwenye umri wa miaka 18, huku Coutinho akifeli katika mpango wake wa kulazimisha kuondoka […]