Category: michezo kimataifa

ALICHOFUATA KEPA CHELSEA NI MATAJI

LONDON, England KIPA mpya aliyesajiliwa kwa dau la rekodi ya dunia, Kepa Arrizabalaga, amesema anataka kuhakikisha anashinda mataji katika klabu hiyo iliyomnyakua kwa pauni milioni 71.6 kutoka Athletic Bilbao. Arrizabalaga, alichukuwa nafasi ya kipa Mbelgiji, Thibaut Courtois, ambaye alitangazwa kuwa mchezaji mpya wa Real Madrid juzi Jumatano. Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 23, aliichezea Bilbao mechi 57 za […]

MAJERAHA YAMHARIBIA ‘FUNDI’ MPYA PALACE

LONDON, England KIUNGO mpya wa Kijerumani aliyesaini Crystal Palace, Max Meyer, huenda asiitumikie timu yake hiyo katika mechi za kwanza msimu wa Ligi Kuu England 2018-19. Meyer alisaini Palace wiki iliyopita lakini bado yupo kwenye hatua za awali za mazoezi ya kujiandaa na msimu na hayupo tayari kucheza dhidi ya Fulham kesho. Kabla ya kusajiliwa na timu hiyo, Meyer alikuwa […]

GUARDIOLA: NYIE HANGAIKENI TU, NITAWANYOOSHA

MANCHESTER, England WAKATI timu pinzani zilizoshindwa kuizuia vema Manchester City isichukue ubingwa msimu uliopita zikiwa zimejiandaa vilivyo kuwapa upinzani, kocha wa timu hiyo, Pep Guardiola, ametoa onyo kali akisema msimu huu amejiimarisha zaidi. Man City walivunja rekodi za Ligi Kuu England msimu uliopita ambao waliumaliza na pointi 100, wakiwaacha wapinzani wao wa jadi, Manchester United kwa tofauti ya pointi 19. […]

POCHETTINO ANA HOFU SANA

LONDON, England KOCHA wa Tottenham, Mauricio Pochettino, amesema ana wasiwasi na kikosi chake kufanya vizuri msimu huu baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-1 na Girona katika mchezo wa kirafiki. Pochettino atawakosa nyota wake waliokuwa katika vikosi vya timu za Taifa kama Harry Kane, Hugo Lloris, Delle Ali na wengine wengi. “Nafurahi tumemaliza michezo yetu ya kujiandaa na msimu lakini […]

LAMPARD: WAPINZANI WATAJUTA

DERBYSHIRE, England KOCHA wa Derby County, Frank Lampard, ametoa tahadhari kwa wapinzani wake atakaokutana nao katika michezo ya Ligi Daraja la Kwanza. Lampard alifanikiwa kushinda mchezo wake wa kwanza wa ligi baada ya kuinyuka Reading mabao 2-1 akiamini timu hiyo itamaliza wakiwa wa kwanza. “Tumejipanga vizuri kuwakabili wapinzani wetu, naamini tutamaliza kwa kasi hii na kufanikiwa kupanda daraja,” alisema kocha […]

KOULIBALY AIKATA MAINI CHELSEA

NAPLES, Italia BEKI wa kati wa Napoli, Kalidou Koulibaly, amesaini mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia timu hiyo akifuta ndoto za Chelsea kukihitaji kisiki hicho cha Senegal. Tangu zama za Antonio Conte alionekana kuvutiwa na beki huyo aliyefanya vizuri katika fainali za Kombe la Dunia na kikosi cha Senegal. Wengi walitegemea kuona akiungana na Maurizio Sarri kwa mara nyingine tena […]

ROONEY AANZA KUFANYA YAKE D.C. UNITED

WASHINGTON, Marekani STRAIKA Wayne Rooney ameanza kufanya yake katika Ligi Kuu ya Marekani, MLS, baada ya kupachika bao katika mchezo wake wa kwanza akiwa na timu yake mpya ya D.C. United ambalo liliwasaidia kuondoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya  Colorado Rapids. Katika mchezo huo ambao ulipigwa usiku wa kuamkia jana, Rooney (32) ambaye anashika nafasi ya pili kwa […]

KAVURUGWA

NEW YORK, Marekani Martial azidi kumchanganya Mourinho KOCHA Jose Mourinho amesema alitarajia nyota wake, Anthony Martial, anatakiwa kuwa amesharejea kwenye kikosi cha Manchester United, baada ya kwenda kumshuhudia mwanae aliyezaliwa na huku akionekana kuchanganyikiwa zaidi baada ya kutangaza kuwa staa wake mwingine, Nemanja Matic, atalazimika kuzikosa mechi za kwanza msimu ujao kutokana  na kuwa amefanyiwa upasuaji. Straika huyo aliondoka katika […]