Category: michezo kimataifa

CHEKI YALIYOITEKA BALLON D’OR 2017

LONDON, England UKIIANGALIA orodha ya nyota 30 waliochaguliwa kuwania tuzo ya Ballon d’Or mwaka huu, ni sawa na kusema itakuwa vita ya wakali wote, kwani takribani majina ya wachezaji wote wakubwa yapo mule. Ingawa sio kitu cha kushtusha sana kusikia majina kama Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Neymar, Luis Suarez, Gianluigi Buffon, Sergio Ramos na Kylian Mbappe yakiwemo kwani tuzo hiyo […]

MWAMUZI ADUI WA MOURINHO KATIKATI YA UWANJA

MERSEYSIDE, Liverpool NI wazi taarifa za kwamba mwamuzi, Martin Atkinson, atakuwa katikati mwa wanaume 22 wa Liverpool na Man United wikiendi hii, hazitapokelewa vizuri na Jose Mourinho. Unajua kwanini? Sikia hii. Atkinson, mwenye makazi yake mitaa ya Bradford, Yorkshire Magharibi, England, alikuwa mwamuzi kwenye mtanange wa ufunguzi Ligi Kuu England baina ya Red Devils hao na West Ham, lakini mashabiki […]

MAJERUHI MANE KUSUGUA BENCHI WIKI SITA

LONDON, England KLABU ya Liverpool imebainisha kuwa straika wao, Sadio Mane, anaweza kukosa wiki sita zijazo msimu huu kutokana na majeraha ya misuli. Mane alipata majeraha akiwa na timu ya Taifa ya Senegal ambayo mwishoni mwa wiki iliyopita iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Visiwa vya Cape Verde. “Sadio Mane hataweza kucheza baada ya kupata majeraha ya misuli […]

WAKALI HAWA HUENDA WAKAKOSEKANA URUSI MWAKANI

AMSTERDAM, Uholanzi MECHI za kufuzu kushiriki Kombe la Dunia kwa mataifa kutoka Ulaya ndio zinakaribia kumalizika, huku nyota kadhaa wale bora wa Ulaya wakiumiza kichwa kuhusu hatima ya mataifa yao. Hata hivyo, kuna baadhi ya mataifa makubwa ya Ulaya huenda yakakosa tiketi ya kushiriki michuano hiyo, kitu kitakachopeleka mastaa hawa kukosekana.   Arjen Robben Kabla ya mechi za jana, Uholanzi […]

HAO NAPOLI NI NOMA SERIE A

NAPLES, Italia KOCHA Maurizio Sarri, anaonekana kufanya kazi nzuri sana ndani ya kikosi chake cha Napoli kwa sasa, akiwa amewaimarisha mno vijana wake hasa kwenye mashambulizi. Hivi sasa ndiyo timu inayoongoza kwa kushambulia nchini Italia na ni moja ya klabu zinazoongoza kwa kuwa na mashambulizi makali duniani. Ni kwa jinsi gani wanavyofanya mashambulizi yao? Twende sawa upate madini. Mfumo wao […]

RIBERY APEWA ZA USO NA BABBEL

MUNICH, Ujerumani MKONGWE wa Bayern Munich, Markus Babbel, amemjia juu staa Franck Ribery, akiwaambia hata siku moja asijilinganishe na wakali Cristiano Ronaldo na Lionel Messi. Ribery yuko nje ya uwanja akiuguza majeraha yake ya goti aliyoyapata katika mchezo wa Bundesliga dhidi ya Hertha Berlin na amekuwa akitajwa kuhusika katika sakata la kufukuzwa kazi kwa kocha Carlo Ancelotti. Ancelotti alitimuliwa baada […]

KWA TAKWIMU HIZI, GUARDIOLA, MOURINHO HAWAMWACHI MTU EPL

MANCHESTER, England MAKOCHA hao ndio wanaozungumziwa sana kwa sasa kwenye mbio za kuwania taji la Ligi Kuu England, kwani timu zao zinakabana koo kileleni zikilingana pointi. Pep Guardiola na Man City yake wanaongoza ligi kwa bao moja tu la kufunga. Timu hizo za jijini Manchester zimeiacha Tottenham inayoshika nafasi ya tatu kwa pointi tano. Jose Mourinho wa Man United bado […]

MOURINHO AJIACHIA NA MASHABIKI WA LIVERPOOL

MOSCOW, Urussi KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho, juzi alijiachia na mashabiki wa Liverpool kwa kupiga nao picha. Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mirror, kocha huyo alifanya hivyo  kabla ya mechi ya Ligi ya  Mabingwa Ulaya kati ya Liver na Spartkak Moscow, iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1. Liver na Man United walikuwa nchini Urusi kwa ajili ya michuano […]

KENYA WALIVYOIKOSA CHAN 2018

NAIROBI, Kenya HATIMAYE Kenya haitakuwa mwenyeji wa fainali za Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (Chan) zilizotarajiwa kufanyika mwakani. Uamuzi huo umetokana na kikao cha siku moja cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka barani Afrika (Caf), kilichofanyika mjini Accra, Ghana, kikiongozwa na Rais Ahmad Ahmad. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Caf, wamefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha […]