Category: michezo kimataifa

KOMBE LA DUNIA 2018… ITALIA ILIKOSAJE SAFARI YA URUSI?

MILAN, Italia TAIFA zima la Italia limeamka asubuhi nyingine ya leo na kugundua kwamba ni kweli michuano ya Kombe la Dunia itatimua vumbi mwakani bila timu yao ya soka kuwepo. Italia inayoongozwa na kocha Gian Piero Ventura, ilishindwa kukata tiketi ya kushiriki michuano hiyo inayotegemewa kufanyika nchini Urusi miezi kadhaa ijayo, baada ya kupoteza mechi za mchujo dhidi ya Sweden […]

DROGBA KUTUNDIKA DALUGA MWAKANI

LOS ANGELES, Marekani MPACHIKAJI mabao wa zamani wa Chelsea na timu ya Taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba, ametangaza kuwa ataachana na soka hapo mwakani. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 39, ambaye anaichezea Phoenix Rising, ambayo pia ana hisa zake klabuni hapo, aliichezea Chelsea mechi 381 kwa misimu miwili aliyokaa England, akiifungia mabao 164. Akiwa na Blues, pia alishinda […]

HII YA FELLAINI KUSEPA MAN UNITED IKOJE?

MANCHESTER, England KWA sasa ni kama mustakabali wa kiungo Marouane Fellaini katika klabu ya Manchester United haueleweki. Ataondoka au atabaki? Hilo ndilo swali lililo vichwani mwa mashabiki wa Man United. Miezi 12 iliyopita, hakukuwa na shabiki wa Mashetani Wekundu aliyekuwa anamtamani Fellaini, hasa baada ya kusababisha penalti dhidi ya Everton. Hata hivyo, Kocha Jose Mourinho aliendelea kumkingia kifua, akiamini ataimarika […]

KITAELEWEKA TU NI AUBAMEYANG, MANE AU SALAH MCHEZAJI BORA AFRIKA 2017?

CAIRO, Misri ZIMEBAKI wiki kadhaa kabla ya macho na masikio ya mashabiki wa soka kuelekezwa kwenye hafla ya utoaji tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa mwaka huu. Kwa mujibu wa taarifa ya wadhamini wa tuzo hiyo ambao ni Shirika la Habari la Uingereza (BBC), mshindi anatarajiwa kutangazwa Desemba 11. Mwaka jana, ilitua kwa winga wa Leicester City na timu […]

ACHA SILVA, HATA HAWA WALITAFUTIWA SABABU YA KUTOSWA

LONDON, England IMEBAINIKA kuwa klabu ya Arsenal ilikuwa na nafasi ya kumsajili kiungo mahiri wa Man City, David Silva, alipokuwa akisakata soka nchini Hispania lakini ilimpotezea kwa kuhisi asingeweza kuhimili presha ya Ligi Kuu England. Silva ambaye ni mshindi wa Kombe la Dunia, tangu atue England na kusaini Man City, amedhihirisha kipaji chake ambapo huwezi kutaja viungo wachezeshaji mahiri duniani […]

VITA YA RONALDO NA MESSI KWENYE TUZO BINAFSI IKOJE?

  LONDON, England KWA takribani miaka 10 Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, wamechuana vikali ndani na nje ya uwanja na hadi kufikia sasa wamefikisha idadi ya kushangaza ya tuzo binafsi. Staa wa Real Madrid, Ronaldo, aliijumuisha tuzo ya mchezaji bora wa kiume ya FIFA katika kabati lake lililojaa tuzo binafsi ‘kibao’ kwa kumpiku Messi. Hiyo ilikuwa ni habari mbaya kwa […]

HIZI HAZISHIKIKI BARANI ULAYA MSIMU HUU

  LONDON, England MSIMU huu wa 2017-18 umeanza vizuri kwa baadhi ya timu barani Ulaya, zikionekana kuwa moto wa kuotea mbali na hata kuwapa jeuri mashabiki wake. Makala haya yameziangazia timu hizo ambazo kwa kiasi kikubwa zinazitikisa klabu kubwa tano Ulaya kutokana na mwenendo wao, japo ni mapema mno kuzitabiria ubingwa. RB Leipzig (Bundesliga) Kikosi cha timu hiyo kinaundwa na […]

MULLER AMREJESHA ANCELOTTI BAYERN

MUNICH, Ujerumani LICHA ya kuwa tayari ameshafukuzwa, jina la kocha Carlo Ancelotti limeendelea kutajwa katika klabu ya Bayern Munich, na safari hii ni straika Thomas Muller. Muller, raia wa Ujerumani, alisema Ancelotti hapaswi kufanywa mbuzi wa kafara kwa mwenendo mbovu wa Bayern. Bayern waliamua kumtimua Ancelotti baada ya kikosi hicho kuchapwa mabao 3-0 na PSG, katika mchezo wa Ligi ya […]

MURRAY, DJOKOVIC KUNOGESHA AUSTRALIAN OPEN

CANBERRA, Australia VINARA wa tenisi kwa upande wa wanaume na wanawake, Andy Murray  na  Novak Djokovic   watashiriki michuano ya  Australian Open ambayo itafanyika Januari mwakani. Mkurugenzi Mkuu wa michuano hiyo,  Craig Tiley, alisema jana kwamba nyota hao watashiriki michuano hiyo, baada ya kuwa nje ya uwanja kutokana na sababu mbalimbali. Alizitaja sababu hizo kuwa Mwingereza anayeshika nafasi ya kwanza kwa […]