Category: michezo kimataifa

UCHAWI WA MAMA YAKE CHANZO ADEBAYOR KUPOTEA KWENYE SOKA?

LONDON, England EMMANUEL Adebayor alipoondoka Arsenal mwaka 2010, alikuwa amefunga mabao 46 katika mechi 104 pekee. Alipokwenda Manchester City akapasia nyavu mara 15 katika michezo 34. Hata hivyo, makali yake hayakuwa ya muda mrefu kwani msimu wake wa mwisho kuwa kwenye ubora wake ulikuwa wa 2013-14 ambapo alifunga mabao 13 na kutoa ‘asisti’ nne akiwa na kikosi cha Tottenham. Kipindi […]

HAWA NDIO WACHEZAJI WALIOPO SOKONI ILA WANACHUNIWA

LONDON, England JOTO la usajili barani Ulaya limepamba moto kwa kiasi kikubwa kwa klabu mbalimbali kujibebea wachezaji waliowasaka ili waweze kuwatumia kwa msimu mpya wa ligi zao. Hadi sasa ni wachezaji wengi waliokwishatangazwa kusaini mikataba ya kuhamia timu mpya, huku wengine wakisaini mikataba ya kubaki na timu zao. Leo tumekuandalia orodha ya wakali 10 wanaotafuta timu za kuchezea msimu ujao, […]

BARCELONA YAMZUIA NEYMAR JR KWENDA PSG

MIAMBA ya soka nchini Hispania, FC Barcelona imekata mzizi wa fitna juu ya tetesi za usajili wa nyota wake Neymar Jr, baada ya kusema kwamba nyota huyo raia wa Brazil hataondoka Camp Nou. Neymar amekuwa akihusishwa kuhamia  kwa magwiji wa soka nchini Ufaransa katika klabu ya Paris Saint Germain (PSG). Hata hiyo Makamu wa Raisi wa Barca, Jordi Mestre amekata […]

RAPA DMX JELA MIAKA 44 KWA UKWEPAJI KODI

NEW YORK, Marekani RAPA wa Marekani, DMX, kwa sasa ameingia kwenye matatizo na Serikali ya nchi hiyo baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kukwepa kodi kiasi cha dola milioni 1.7. Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa rapa huyo alikuwa akificha mapato yake kwa miaka kadhaa. DMX alitajwa kukwepa kutumia akaunti zake binafsi na kutumia zile mbadala. Rapa huyo pia alilipwa kiasi […]

NONDO NNE ZA: MAYWEATHER V MCGREGOR

  LAS VEGAS, Marekani   BAADA ya bondia Floyd Mayweather na Conor McGregor kutambiana kwenye mkutano na waandishi wa habari wiki iliyopita, sasa wakali hao wamerudi ‘gym’ kuendelea na mazoezi kabla ya pambano lao litakalopigwa Agosti 26, mwaka huu. Ukiachana na fujo, utani na kejeli walizotoleana wakali hao wakiwa kwenye miji ya Los Angeles, Toronto, New York na London, kuna […]

POLE NOURI: JANGA ALILOPATA LIMEUSIKITISHA ULIMWENGU WA SOKA, SI AJAX TU

AMSTERDARM, Uholanzi TAARIFA zilizotoka kuhusu kinda la miaka 20 la klabu ya Ajax, Abdelhak Nouri, kuwa kilichomfanya aanguke uwanjani wiki iliyopita ni tatizo la ubongo, zimeitikisa klabu yake hiyo. Baada ya kinda huyo kupewa huduma ya kwanza uwanjani hapo wakati Ajax ilipokuwa ikicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Werder Bremen na ikaonekana anahitaji huduma ya kihospitali zaidi, taarifa zaidi zikathibitisha […]

LACAZETTE, KOLASINAC KUMBE WENGER AMELAMBA DUME

LONDON, England JUZI Arsenal ilianza maandalizi ya msimu ujao kwa ushindi wa mabao 2-0  dhidi ya Sydney FC, huku  mastaa wawili waliosajiliwa na Gunners wakicheza mechi yao ya kwanza. Katika mchezo huo, beki wao mpya Sead Kolasinac, aliweza kuanza kipindi cha kwanza na huku mashabiki wa timu hiyo wakilazimika kusubiri hadi dakika ya 68 ili kumshuhudia straika wao mpya aliyesajiliwa […]

WATAPATA NAFASI VIKOSI VYA KWANZA AMA WATAISHIA KUSUGUA BENCHI 2017/18

MADRID, Hispania WAKATI mashabiki wa soka wakiwa wanausubiri kwa hamu msimu mpya wa soka wa 2017/18, imekuwa ikishuhudiwa klabu kubwa Ulaya zikipigana vikumbo ili kusuka vikosi vyake. Katika mshikemshike huo tayari kuna ambazo zimeshanasa vifaa muhimu ambavyo zilikuwa zikivihitaji na nyingine zikiwa bado zina safari ndefu ya kuwafukuzia mastaa ambao wataweza kuwapa mafanikio katika msimu huo mpya ujao. Katika makala […]

TIEMOUE BAKAYOKO YAYA TOURE MPYA NDANI YA STAMFORD BRIDGE

LONDON, England MABOSI wa Chelsea wamekubali kutoa Pauni milioni 40 zilizokuwa zikitakiwa na Monaco ili wamruhusu kiungo wao, Tiemoue Bakayoko, kutua Stamford Bridge. Mbali na Chelsea, saini yake ilikuwa ikifukuziwa na klabu kadhaa za Ulaya, zikiwamo za Ligi Kuu England kama vile Manchester United, Arsenal na Liverpool. Biashara ya staa huyo ni nzuri kwa kocha Antonio Conte, ambaye ana wasiwasi […]