Category: michezo kimataifa

Wameng’ara lakini ubingwa wa ligi wanausikia bombani

LONDON, England RAHA ya soka ni pale unaposhinda mechi na kutwaa ubingwa, lakini jambo hilo mara nyingi huwa si kazi rahisi kutokana na kwamba, mwisho wa siku ni timu moja tu ambayo inaweza kutwaa ubingwa wa mashindano yoyote na ya ligi. Kutokana na jambo hilo kuna baadhi ya wachezaji nyota katika historia ya soka ambao wameshawahi kutwaa mataji makubwa wakiwa […]

Zidane: Simtaki Neymar wala Mbappe

MADRID, Hispania ZINEDINE Zidane hakubaliani na harakati za Real Madrid chini ya Rais, Florentino Perez, kuzisaka saini za mastaa wa PSG, Neymar na Kylian Mbappe. Huku uongozi wa Madrid ukiamini safu yake ya ushambuliaji inahitaji kuongezewa nguvu, Zidane aliibuka na kumsifia Karim Benzema ikiwa ni kuua dili la nyota hao. Madrid wametajwa kuandaa mpunga wa maana kuwasajili Neymar na Mbappe […]

Rais: Messi, Barca ndoa ya milele

CATALUNYA, Hispania NDICHO alichokisema Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu, kwamba hakuna uwezekano wa siku moja Lionel Messi kuichezea klabu nyingine na sasa wanafikiria kumpa mkataba mpya. Messi alimwaga wino mwaka 2017 mkataba utakaomalizika 2021, lakini bado Barca wanataka kumfunga zaidi mshindi huyo mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or. “Tunataka awe na maisha marefu ya soka hapa ili tuendelee […]

Bingwa EPL kupatikana mechi ya mwisho kama misimu hii?

LONDON, England TANGU michuano ya Ligi Kuu England ianzishwe mwaka 1992, kumekuwapo mchuano mkali wa kuwania ubingwa kiasi cha kwamba inafikia hatua hadi mechi za mwisho bingwa hajajulikana. Hali hii ndiyo inayojitokeza tena msimu huu ambapo timu za Liverpool na  Manchester City zinachuana vikali kuwania taji hilo na huku  Tottenham wakifanya kila waliwezalo ili kuwafikia vigogo hao. Katika msimu huu, […]

FAGIO LA CHUMA

*Solskjaer aamua kuanza upya, mshahara wa Sanchez kupunguzwa, watano kuondolewa Man United MANCHESTER, England YUPO ‘siriaz’, unaweza kusema hivyo, baada ya kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, kuamua kuijenga tena timu hiyo huku tetesi zikidai kuwa wachezaji watano ndani ya kikosi hicho wataondoka mwishoni mwa msimu huu. Solskjaer ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa Manchester United, alisaini mkataba wa miaka […]

Sancho afananishwa na Ribery

MUNICH, Ujerumani KOCHA wa zamani wa Borussia Dortmund, Ottmar Hitzfeld, amekunwa vilivyo na kiwango kinachooneshwa msimu huu na winga, Jadon Sancho, kiasi cha kumfananisha na Franck Ribery, aliyekuwa anachipukia Bayern Munich. Hadi kufikia sasa, Sancho, amefanikiwa kutoa pasi 13 za mabao msimu huu wa Bundesliga, pia akizifumania nyavu mara nane, kiwango kilichompa umaarufu mkubwa tangu atue Dortmund akitokea Man City. […]

Baba na mwana Mastaa ambao waliwahi kufundishwa na baba zao

MADRID, Hispania MWISHONI mwa wiki Kocha Zinedine Zidane alimwanzisha mwanawe, Luca, katika kikosi cha kwanza cha Real Madrid ambacho kiliivaa timu ya Huesca, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania, La Liga. Hatua hiyo imemfanya kocha huyo kuwa mwingine ambaye anafundisha timu ambayo anaichezea mwanawe. Katika makala haya tutaangalia baadhi ya wachezaji wa soka la kulipwa ambao wamewahi kufundishwa na […]

NGOMA NZITO

Solskjaer akiri kuwa na mtihani mgumu Man U MANCHESTER, England KICHAPO cha mabao 2-1 nyumbani kwa Wolves, kimempa kazi ngumu kocha, Ole Gunnar Solskjaer ya kuhakikisha Manchester United inamaliza msimu huu wa Ligi Kuu England ndani ya nafasi nne bora za juu. Baada ya kushindwa kunyakua pointi tatu katika mechi hiyo iliyochezwa usiku wa kuamkia jana, Solskjaer sasa ana kibarua […]

Arsenal wakifanya haya mbona msimu ujao mtawapenda

LONDON, England MSIMU huu Arsenal wanaonekana kuwa kwenye ubora ikilinganishwa na uliopita, baada ya kocha wao, Unai Emery, kufanya kazi kubwa na kuiwezesha Gunners kuondokana na matatizo iliyokuwa nayo misimu miwili ikiwa chini ya Arsene Wenger. Hata hivyo, pamoja na kuwa kwenye ubora kikosi hicho cha Arsenal, bado haijawa tishio kubwa kwa timu zinazoshika nafasi sita za juu kwenye msimamo […]