Category: michezo kimataifa

Sterling amwagiwa sifa kibao

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, amepewa sifa kibao na mchambuzi wa kituo cha Sky Sports, Ian Wright, baada ya mchezaji huyo kufunga mabao mawili dhidi ya Crystal Palace. Timu hiyo inayonolewa na Pep Guardiola, walishinda mabao 3-1 huku Gabriel Jesus akifunga bao jingine kati ya hayo, lakini Sterling alionekana kumfurahisha zaidi mchambuzi huyo. “Kila siku anakuwa mpya […]

WANATOKA

W*Solskjaer apanga kufanya maajabu Camp Nou, kocha Barca ampiga kijembe *Ajax ‘full’ mzuka unaambiwa, Juve kukomaa mwanzo-mwisho CATALUNYA, Hispania USIKU wa Ulaya umerejea tena, moto ni uleule katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa vigogo wa nchini England, Manchester United, kushuka uwanjani leo watakapokuwa wageni wa Barcelona. Wiki iliyopita timu hizo zilipokutana, Barcelona walifanikiwa kushinda bao 1-0 […]

Liver, Man City zazidi kunyukana ubingwa EPL

LONDON,England TIMU za Liverpool na Manchester City zimeendelea kuchuana vikali katika vita ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England, baada ya jana kila moja kuondoka na ushindi  dhidi ya wapinzani wao. Michezo hiyo iliyopigwa katika viwanja vya Selhurst Park na Anfield, Man City wakiwa ugenini waliweza kuondoka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Crystal Palace, huku Liver wakiwa nyumbani […]

Simeone ampa tano Oblak

MADRID, Hispania KOCHA Diego Simeone amempa tano mlinda mlango wake, Jan Oblak, akimwelezea kuwa ndiye bora duniani baada ya staa huyo kuiwezesha Atletico Madrid kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya  Celta Vigo katika michuano ya Ligi Kuu ya Hispania. Katika mchezo huo wa juzi, Atletico waliweza kuzinduka katika kipigo cha wiki iliyopita cha mabao  2-0 kutoka kwa Barcelona na […]

Guardiola: Siwezi kumpiku Hodgson

 LONDON, England KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola, amesema kwamba anavyoamini hawezi kumpiku mwenzake wa  Crystal Palace, Roy Hodgson na kuendelea kubaki kwenye soka hadi kufikia umri wa miaka  71. Jana Hodgson na timu yake ya Palace walikuwa wakiwakaribisha vijana wa Guardiola masaa mawili kabla ya vinara wa Ligi Kuu England, Liverpool kuikaribisha Chelsea katika Uwanja wa Anfield. Mbio za […]

Mourinho: McTominay muhimu zaidi Man United

MANCHESTER, England KOCHA wa zamani wa Manchester United, Jose Mourinho, amesema kuwa kiungo chipukizi wa kikosi hicho, Scott McTominay, kwa sasa ni mchezaji muhimu ndani ya timu hiyo inayonolewa na Ole Gunnar Solskjaer. Mourinho ambaye alimpa nafasi chipukizi huyo wa miaka 22, kwa mara ya kwanza msimu uliopita alisema kuwa Barcelona walishindwa kutamba sababu ya kiungo huyo mwenye umbo kubwa. […]

NAHARIBU

MERSEYSIDE, England LIGI Kuu ya England imefika patamu, hapo kesho katika Uwanja wa Anfield, Liverpool watakuwa wenyeji wa Chelsea ambao wamedhamiria kuharibu sherehe za ubingwa ili kuweka matumaini ya kuingia ‘top four’ hai. Liverpool wanaongoza Ligi Kuu ya England kwa pointi 82, baada ya kucheza michezo 33, wakifuatiwa na Manchester City ambao wanazo 80 na mechi 32 pungufu ya mchezo […]

Arsenal kupindua meza kibabe

LONDON, England UNAAMBIWA kocha wa Arsenal, Unai Emery, amewaambia mabosi wake kuwa wafanye juu chini wapate saini ya kiungo wa Manchester United, Ander Herrera. Taarifa zinadai kuwa kiungo huyo raia wa Hispania amekubali kujiunga na vigogo wa Ufaransa, PSG lakini Emery anataka kuhakikisha hilo linashindikana mwishoni mwa msimu huu. Ripoti zinasema kocha huyo wa Arsenal anamtaka Herrera ili kuziba nafasi […]

Kane, Dele wamtia wazimu Pochettino

LONDON, England HALI imezidi kuwa ngumu ndani ya kikosi cha Tottenham, baada ya mastaa wawili wa timu hiyo, Harry Kane na Dele Alli, kukumbwa na majeraha katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya waliocheza dhidi ya Manchester City. Tottenham walishinda bao 1-0 katika mchezo huo, lakini kocha wa kikosi hicho, Mauricio Pochettino, hakufurahishwa na taarifa za nyota hao wawili raia […]

HAWATAAMINI

HUSSEIN OMAR NA EZEKIEL TENDWA KAMA TP Mazembe walidhani watapata mteremko dhidi ya Simba leo kisa wanacheza kwao, wanaweza wakapata aibu ya mwaka kutokana na Wekundu wa Msimbazi walivyotega mitego yao. Simba watakuwa wageni wa wakali hao wa Afrika katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali, utakaochezwa kwenye Uwanja wa TP Mazembe, nchini DR […]