Category: michezo kimataifa

Klopp: Sijawahi kupinga uwezo wa Sturridge

MERSEYSIDE, England KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp, amedai kuwa hajawahi kutilia shaka kipaji cha straika wake, Daniel Sturridge, ambaye juzi alipachika mabao mawili katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Tottenham. Mabao ya staa huyo mwenye umri wa miaka 27 ndiyo yaliyoiwezesha Liver kuingia hatua ya robo fainali ya Kombe la Ligi. Mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Anfield ulikuwa […]

Rooney ashauriwa kuondoka Man Utd

MANCHESTER, England MHARIRI wa Michezo wa mtandao wa Sun, Charlie Wyett, amemshauri mshambuliaji wa Manchester United, Wyane Rooney, kuondoka kwenye klabu hiyo na kujiunga na timu ambayo atacheza kama kiungo wa kati. Rooney alizomewa katika mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia kati ya England na Malta, ambapo Three Lions walishinda mabao 2-0 katika Uwanja wa Wembley, mwishoni mwa […]

Guardiola kuongeza vifaa vitatu

LONDON, England HII sasa sifa. Hivi ndivyo unavyoweza kukielezea kitendo cha Kocha wa Manchester City,  Pep Guardiola, kuamua kupanga kutumia kitita kingine cha pauni milioni 150 ili kuhakikisha anawanasa straika  Aubameyang na mabeki Bellerin  na Bonucci wakati wa usajili wa majira ya baridi yajayo. Msimu uliopita Man City walimkabidhi Guardiola pauni milioni 175 kwa ajili ya kufanya usajili mkubwa na […]

Kocha Brazil ammwagia sifa Neymar

RIO DE JANEIRO, Brazil KOCHA wa timu ya Taifa ya Brazil, Adenor Bacchi ‘Tite’ amemsifu straika wake, Neymar, kwa kiwango alichokionesha kwenye mchezo kati ya Bolivia na kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 , lakini akamuonya staa huyo kujifunza kutoka kwenye kadi ya njano aliyopata ambayo itamuacha nje kwenye mechi dhidi ya Venezuela. Staa huyo wa Barcelona aliifungia timu yake […]

Lingard amkingia kifua Rooney

LONDON, England STAA Jesse Lingard amemkingia kifua Nahodha wa Manchester United na Timu ya Taifa ya England, Wayne Rooney, akisema hakuna anayepaswa kumkosoa kwa sababu ya matokeo waliyoyapata. Winga huyo ameitwa kwenye kikosi cha taifa cha England, huku akitegemea timu yake hiyo ya taifa kuifunga Malta Jumamosi hii ili kutafuta nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia. Rooney amepoteza […]

Majeraha kumnyima Robben mechi mbili

MUNICH, Ujerumani STAA wa kimataifa wa Uholanzi, Arjen Robben, atalazimika kuikosa baadhi ya michezo ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2018. Kocha Danny Blind amemtema nyota huyo wa Bayern Munich katika kikosi cha sasa na kuna uwezekano mkubwa wa kukosa mechi mbili zijazo. Winga huyo hatokuwa sehemu ya kikosi cha Uholanzi kitakachocheza michezo dhidi ya Belarus […]

Zidane ajishuku kufukuzwa Bernabeu

MADRID, Hispania KOCHA wa Real Madrid, Zinedine Zidane, amedai kuwa haogopi kutimuliwa katika klabu hiyo. Zidane amesema hahofii suala hilo kwani anajua wazi kuwa hawezi kuliepuka katika kipindi chake chote cha maisha ya soka. Zidane alichukua nafasi hiyo baada ya Rafael Benitez kutimuliwa na aliiongoza Madrid kuchukua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Hata hivyo, alishindwa kuipa Madrid ubingwa wa […]

SONG AKIMBIZWA HOSPITALI, UGONJWA WA KIHARUSI WATISHIA UHAI WAKE

YAOUNDE, CAMEROON STAA wa zamani wa timu ya Taifa ya Cameroon, Rigobert Song, juzi alikimbizwa hospitalini baada ya kukumbwa na ugonjwa wa kiharusi. Nguli huyo mwenye umri wa miaka 40 ambaye ni mjomba wa staa wa zamani wa Arsenal, Alex Song, alionekana kuzidiwa na ugonjwa huo hatari ndipo alipopelekwa ‘fasta’ kwenye hospitali moja ya jijini Yaounde. Kwa mujibu wa taarifa […]