Category: michezo kimataifa

VIDAL ARUDI NYUMBANI KUOA

CATALUNYA, Hispania MWISHONI mwa wiki iliyopita, staa wa kimataifa wa Almeria anayekipiga Barcelona, Aleix Vidal, alirudi nchi humo kufunga ndoa. Imeripotiwa kuwa kocha wa Barca, Luis Enrique, alimruhusu Vidal kuondoka Catalunya na hakushiriki mazoezi ya pamoja ya timu hiyo. Wakati anaondoka, uongozi wa klabu hiyo ulitangaza kuwa Vidal anakwenda Almeria kwa sababu binafsi na hakukuwa na taarifa hizo za harusi. […]

WENGER AMEINGIA ‘CHAKA’ KUTOA PAUNI MIL 34?

LONDON, England WAKATI wa dirisha la usajili la majira ya kiangazi, Arsenal waliweka kando utamaduni wao wa ubahili na kumsajili kiungo Granit Xhaka. Arsenal walitoa pauni milioni 34 kuinasa saini ya Granit Xhaka. Kabla ya hapo, Xhaka alikuwa akiitoa udenda Arsenal kwa muda mrefu na kocha Arsene Wenger alikuwa akijitaja kuwa shabiki mkubwa wa kiungo huyo. Licha ya uhamisho wake […]

BABU ROBINSON ALIVYOITIKISA TWITTER

LONDON, England MASHABIKI wa Ligi Kuu England walishangazwa mno kumwona tena mlinda mlango mkongwe, Paul Robinson akiidakia klabu ya Burnley dhidi ya Manchester City katika mchezo wa ligi uliopigwa wikiendi iliyopita. Robinson aliyewahi kuzichezea klabu za Leeds, Tottenham, Blackburn na timu ya taifa ya England, alichukua nafasi ya mlinda mlango mahiri Tom Heaton aliye majeruhi. Robinson mwenye umri wa miaka […]

KWANINI MADRID WALIVAA JEZI ZA PLASTIKI?

MADRID, Hispania MABINGWA mara 11 wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid, mapema wikiendi iliyopita waliwaacha watu na maswali juu ya jezi walizotumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu Hispania dhidi ya Sporting Gijon. Mtanange huo uliomalizika kwa Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, ulikuwa na kitu kigeni machoni mwa wadau wa timu hiyo ambapo jezi zilionekana kuwa ni nyepesi […]

MIAKA MIWILI YA MATESO KWA KOMPANY

MANCHESTER, England NI dhahiri kwamba majeraha ya mara kwa mara yanahatarisha maisha ya soka la nahodha wa Manchester City, Vincent Kompany, kwani hadi sasa amekamilisha takribani miaka miwili na nusu ya kuwa majeruhi tangu alipojiunga na klabu hiyo. Kabla ya mchezo dhidi ya Borussia Monchengladbach wiki iliyopita, kocha wa City, Pep Guardiola aliweka wazi kuwa beki wake huyo anasumbuliwa na […]

ROONEY AZIDI KULIA NA VYOMBO VYA HABARI

LONDON, England NAHODHA wa Manchester United, Wayne Rooney, bado ameendelea kupinga taarifa zinazozunguka maisha yake binafsi, ikiwa ni baada ya kuweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa Ulaya katika historia ya timu hiyo. Katika mchezo huo uliopigwa usiku wa kuamkia jana, nahodha huyo alifunga bao lake la 39 dhidi ya  Feyenoord na hivyo kumpita  Ruud van Nistelrooy. Hata hivyo, badala […]

PIQUE, SHAKIRA WASHEREHEKEA USHINDI WA BARCA

MADRID, Hispania WANANDOA Gerard Pique na Shakira waliamua kula bata wakisherehekea ushindi wa  Barcelona ambao iliupata juzi dhidi ya Celtic, katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kufanikiwa kutinga hatua ya 16 bora. Beki huyo na nyota huyo wa muziki wa miondoko ya  pop star wanasemekana kujirusha juzi ambapo katika picha aliyoituma  Shakira  katika mtandao wake wa kijamii wa […]

IMEBUMA ARSENAL WASHUSHWA KILELENI, MAN CITY WATINGA 16 BORA

LONDON, England MATUMAINI ya Arsenal kuongoza Kundi A yamebuma, baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya PSG katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliopigwa jana usiku kwenye Uwanja wa Emirates. PSG ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza likifungwa na Edinson Cavani dakika ya 21. Lakini Arsenal walisawazisha kwa penalti kabla ya mapumziko, baada ya beki […]

FBI WAMWOKOA BRAD PITT KWA ANGELINA JOLIE

NEW YORK, Marekani SHIRIKA la Upelelezi (FBI) wamekamilisha uchunguzi wa kesi iliyomkabili mwigizaji Brad Pitt kwa kudaiwa kumpiga mwanawe Maddox. Brad ambaye ana watoto sita pamoja na mke wake mwigizaji Angelina Jolie, amedaiwa hakufanya kosa lolote baada ya shutuma zilizotolewa na mkewe huyo mwanzoni mwa Septemba mwaka huu. Mke wa mwigizaji huyo, Angelina alidai talaka akisema nyota huyo ananyanyasa watoto, […]

UMRI WA MURRAY NI MDOGO KUITWA SIR?

Edinburgh, Scotland MCHEZA tenisi namba moja kwa ubora duniani, Andy Murray, ameanza kukwepa kupewa heshima ya kuitwa Sir Andy, akisema bado ana umri mdogo. Murray amekuwa na mwaka mzuri kwenye tenisi kwa kushika namba moja kwa kumshinda Novak Djokovic kwa seti mbili (6-3 6-4) kwenye Uwanja wa O2 Arena mjini London mwishoni mwa wiki iliyopita. Murray mwenye umri wa miaka […]