Category: michezo kimataifa

Dili zinazosubiriwa kutikisa usajili kiangazi

LONDON, England HIKI ni kipindi kibaya sana kwa makocha na mabosi wa klabu mbalimbali barani Ulaya, hasa zile zinazohaha kuwazuia mastaa wake wanaotolewa macho na vigogo wengine. Hata hivyo, hakuna namna ya kutenganisha kipindi hiki na tetesi ambazo kwa upande mwingine zina mvuto mkubwa kwa mashabiki wanaotaka kujua wachezaji wanaowaniwa na timu zao. Kwa upande mwingine, ni kawaida kwa kila […]

De Rossi ; Nahodha shupavu anayeacha historia nzito AS Roma

ROME, Italia MSIMU huu umekuwa mgumu kwa timu ya AS Roma, ingawa ni jambo linalotegemewa katika mchezo wa soka. Kitu pekee ambacho Waitaliano hao hawakukitarajia ni kuondoka kwa nahodha wao, Daniele De Rossi. De Rossi ambaye amedumu na ‘Giallorossi’ hao kwa muda wa miaka 18, akiitumikia katika michezo zaidi ya 600, alitangaza kuwa ataiacha klabu yake hiyo ifikapo mwishoni mwa […]

Solskjaer akiiba kengele aweke pamba masikioni

NA AYOUB HINJO NI kwenye matatizo pekee ndipo mwanadamu hufahamu nguvu na uwezo ulio ndani yake. Usiyachukie wala usichukie kwanini wewe umepata tatizo, Mungu hajawahi kumpa mja mzigo asioweza kuubeba. Linapokuja tatizo, furahi, kwa maana wakati wako wa kuigundua nguvu iliyo ndani yako umewadia. Mwandishi wa vitabu Mmarekani, Hellen Keller, akiwa na miezi 19 tu duniani, alipata ulemavu wa macho […]

Sharapova ajiweka pembeni French Open

PARIS, Ufaransa NYOTA hatari wa mchezo wa tenisi kwa upande wa wanawake, Maria Sharapova, amejitoa katika michuano ya mwaka huu ya French Open. Bibiye huyo mwenye umri wa miaka 32, aliutangaza uamuzi wake huo juzi, akieleza kuwa umetokana na tatizo lake la bega. Mapema mwaka huu, Sharapova anayeshika nafasi ya 35 katika viwango vya ubora duniani alifanyiwa matibabu lakini inaonekana […]

Berahino kitanzini kwa ulevi

LONDON, England MWANASOKA anayeichezea Stoke City, Saido Berahino, ameingia matatani baada ya kunaswa akiendesha gari akiwa amekunywa pombe. Mkali huyo alikuwa amezidisha mara tatu ya kiwango kinachotakiwa wakati akiwa ndani ya Range Rover yake katika mitaa ya jijini London. Tayari ameshafungiwa kuendesha usafiri huo kwa miezi 30, adhabu iliyokwenda sambamba na faini ya pauni 75,000.

Griezmann amchefua bosi Atletico

MADRID, Hispania RAIS wa Atletico Madrid, Enrique Cerezo, ameeleza kusikitishwa kwake na uamuzi wa Antoine Griezmann, kusema ataondoka klabuni hapo. Griezmann aliitangaza hatua yake hiyo, akisema huu utakuwa msimu wake wa mwisho akiwa na Atletico aliyojiunga nayo mwaka 2014 akitokea Real Sociedad. “Ni zaidi ya hasira, nimesikitishwa. Nilifikiri Antoine angekuwa na muda mrefu Atletico,” alisema bosi huyo.