Category: Maoni

TUMEMALIZA MWAKA, UBABAISHAJI TFF UKIENDELEA

NA ONESMO KAPINGA MCHEZAJI wa African Lyon, Venance Ludovick, ametufungia mwaka na kutukaribisha mwaka mpya wa 2017 huku ubabaishaji ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ukiendelea kama kawa. Usajili wa Ludovick katika klabu ya African Lyon unaonekana wa utata baada ya kubainika kwamba ana leseni ya timu mbili, yaani Mbao FC na African Lyon zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara. […]

MWAKA 2017 UWE MWOKOZI WA BONGO MOVIE

NA HASSAN DAUDI MWENYEZI Mungu pekee ndiye anayepaswa kushukuriwa kwa kutuwezesha kutuvusha katika mwaka mwingine wa 2017. Pamoja na changamoto nyingine za kimaisha, kuwa miongoni mwa watu waliofanikiwa kuona mwaka mpya ni jambo la heri. Lakini  tukianza kukimbizana na mipango yetu ya mwaka huu mpya, bado tunapaswa kuendelea kutathmini pia miezi 12 iliyopita. Nikiri wazi kuwa mwaka 2016 ulikuwa wa […]

AZAM FC WASIRUDIE KOSA HILI

TIMU ya Azam inatarajia kuiwakilisha nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika itakayoanza mwezi ujao. Azam inatarajia kushiriki michuano huku wakiwa wametimua benchi lote la ufundi lililokuwa likiongozwa na kocha Mhispania Zeben Harnendez. Tunaweza kuona uamuzi wa Azam ulikuwa sahihi wa kutimua benchi la ufundi baada ya kuona timu yao haifanyi vizuri Ligi Kuu Tanzania Bara. Lakini Azam […]

HIKI NDICHO KINACHOMFANYA IBRAHIMOVIC AZIDI KUNG’ARA

LONDON, England UWEZO alionao straika wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic, bado unawashangaza wengi, licha ya kuwa na umri mkubwa. Uwezo wa nyota huyo umekuwa ukiongezeka zaidi kadri umri wa nyota huyo unavyozidi kwenda na bao alilofunga  siku ya `Boxing Day` dhidi ya  Sunderland lilikuwa la 12 kwa mshambuliaji huyo katika Ligi ya England na bao la 17 katika mashindano yote […]

AZAM, YANGA MSIWAPE VISINGIZIO AKINA NGOMA

NA HASSAN DAUDI IMEKUWA ni kama kawaida kila timu zetu zinapoboronga kwenye michuano ya kimataifa sababu kubwa inayotajwa ni maandalizi mabovu. Ni sababu ambayo imeshakuwa sehemu ya maisha ya klabu za hapa nchini kila zinapovurunda kimataifa. Mara nyingi madai hayo huibuka pale zinapoondoshwa kwenye mashindano ya nje ya nchi. Ni utamaduni ambao umeshazoeleka kwenye soka la Bongo. Hivi karibuni ratiba […]

2017 HATUNA HAJA YA ‘CHENGA TWAWALA’

LEO saa 6:00 usiku tunatarajia kuhitimisha mwaka huu wa 2016 na kuukaribisha 2017, huku kila mpenzi wa michezo na burudani nchini akiwa na lake moyoni. Lakini kwa ujumla wote hao wanajiuliza ni kipi wanamichezo na wasanii wetu watakuja nacho mwaka ujao angalau kuendelea na pale tulipofikia kama si kupiga hatua zaidi. Kwa upande wa wanamichezo bado wanaonekana kuwa gizani kutokana […]

UNAHITAJI MUDA ZAIDI KUIELEWA MIPANGO YA BEN POL

NA CHRISTOPHER MSEKENA HUTAWEZA kuipata sauti ya Ben Pol kwenye wimbo wako kama hujatenga fungu la dola za Kimarekani 5,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 10 za Tanzania huku akidhamiria gharama hiyo ianze kutumika mapema mwakani. Anakuwa ni msanii wa kwanza kuweka hadharani kiwango ambacho atahitaji alipwe ili aweze kuingiza sauti yake kwenye wimbo anaotaka kushirikishwa, wengi huwa hawafanyi […]

TUPO VIZURI KISANAA ILA MWAKA 2017 TUREKEBISHE HAYA

MWAKA 2016 umekuwa wa mafanikio kwenye sekta ya burudani Tanzania. Wasanii, wakishirikiana na wadau wa sanaa kwa nguvu kubwa kutoka kwa wewe shabiki, wamefanya makubwa tunayoweza kujivunia. Tukianza kwenye tasnia ya muziki wa kizazi kipya, tumeshuhudia maendeleo makubwa kuwahi kutokea. Hatua za kwenda mbele zimepigwa na wasanii wetu na wameweza kuliteka soko la muziki wa Afrika. Hivi sasa chati kubwa […]

HAWA KWA KUCHEKA NA NYAVU ‘BOXING DAY’ USIPIME

LONDON, England SIKU ya pili ya Krismasi, maarufu kama ‘Boxing Day’, ni siku ambayo huwa ni ya ya watu kutoa zawadi maalumu ama kwa rafiki yako au ndugu.  Utamaduni huo umekuwapo tangu miaka mingi iliyopita na utaendelea kuwapo hadi mwisho wa dunia.  Licha ya kuwa utamaduni wa kupeana zawadi, pia unaonekana kuwa kwenye michezo, hususan soka, ambapo wachezaji huwa wakijitahidi […]

WALIOHUSIKA KUWACHEZESHA WACHEZAJI BILA VIBALI WASIACHWE

NA WINFRIDA MTOI GUMZO kubwa wiki hii katika mchezo wa soka, lilikuwa ni juu ya kukosekana kwa vibali kwa wachezaji wa kigeni waliosajiliwa kwenye klabu tatu kubwa  hapa nchini. Suala hilo liliibuliwa na viongozi wa timu ya Ndanda FC baada ya kutoa malalamiko kwa kudai kuwa Simba wamewatumia wachezaji wa kigeni wasiokuwa na vibali katika mchezo wao wa kufungua pazia […]