Category: Maoni

DANISE UMEZAA KIPENZI CHA WENGI MILTON KEYNEYS

NA HALID MTUMBUKA MATATIZO yaliyotokana na unywaji wa pombe yaliitesa sana afya ya mwanamama wa Kiingereza, Danise. Licha ya raha zote zilizopo katika mitaa ya Jiji la Milton Keynes, sifikiri kwamba baada ya matatizo hayo aliifurahia Milton Keynes kama alivyokuwa na kipenzi chake Kenny kutoka nchini Nigeria. Wakati wakiwa wapenzi hakuwahi kuwaza kama ipo siku atakuja kuteseka kiasi alichoteseka, fimbo […]

ETI ONYANGO AMECHUKUA TUZO, KASEJA, MAPUNDA WAMEZEEKA!

NA HUSSEIN OMAR HATIMAYE ile hafla ya utoaji tuzo za Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) ilifanyika juzi jijini Abuja, Nigeria. Staa wa Leicester City, Riyard Mahrez, ndiye aliyenyakua tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika ambapo mshindi wake alikuwa akisubiriwa kwa hamu na idadi kubwa ya mashabiki wa kandanda. Winga huyo wa Leicester alitwaa tuzo hiyo akiwapiku Pierre-Emerick Aubameyang na […]

HEBU TUJARIBU BAHATI YETU KWENYE NDONDI

PAMOJA na ukweli kuwa soka ndio mchezo unaopendwa zaidi duniani, kwa hapa nchini umeshindwa kuwatendea haki Watanzania kutokana na timu zetu, kuanzia zile za klabu hadi za Taifa, kuboronga katika mashindano ya kimataifa. Tangu timu yetu ya Taifa, Taifa Stars ilipofuzu fainali za Afrika mwaka 1980, haijawahi kufika mbali kwenye anga ya kimataifa zaidi ya kuishia hatua za awali. Hali […]

WAPYA VPL WAONYESHE MAKALI MAPINDUZI CUP

NA WINFRIDA MTOI KOMBE la Mapinduzi ni moja ya michuano  ambayo imekuwa na mvuto mkubwa hivi sasa. Michuano hii imekuwa moja ya matukio makubwa ya soka hapa Tanzania kutokana na kushirikisha timu mchanganyiko. Michuano hii imejipenyeza katikati ya ligi mbili za Tanzania Bara na Visiwani na hatimaye sasa imepata nafasi yake, kwani ligi zote mbili zimeamua kuipisha inayochezwa kwa siku […]

YOTE KHERI

>>Mambo matano muhimu yaliyojitokeza Arsenal vs B’mouth >>Edie Howe alimnyanyasa Arsene Wenger na Arsenal yake >>Je, Arsenal wamepoteza matumaini ya ubingwa? LONDON, England MATUMAINI ya ubingwa wa Ligi Kuu England kwa klabu ya Arsenal msimu huu yanaanza kufifia baada ya kupata matokeo ya sare ya mabao 3-3 dhidi ya Bournemouth katika mchezo uliochezwa usiku wa kuamkia jana kwenye dimba la […]

TIBA YA WAAMUZI WABOVU IPO KUANZIA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI

 NA HASSAN DAUDI KUBORONGA kwa waamuzi ni ugonjwa sugu kwenye soka la Bongo. Hakuna anayeweza kulikataa hilo. Ni nadra kutosikia malalamiko ya uchezeshaji mbovu wa waamuzi kila baada ya mchezo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara (VPL). Mbali na ligi kuu, kumekuwa na kelele nyingi kutoka kwa makocha na viongozi wa timu za madaraja ya chini kuhusu waamuzi kushindwa kuzitafsiri […]

UKIONA WAMEHAMA TIMU ZAO JANUARI USISHANGAE

LONDON, England HIVI sasa vichwa vya makocha wa timu mbalimbali havijatulia kabisa. Tayari presha ya dirisha dogo la usajili la Januari imeshaanza. Mauricio Pochrettino amejinasibu kuwa hatafanya usajili lakini huenda akabadili mawazo yake kadiri siku zinavyokwenda. Jose Mourinho naye ametangaza kuwa hataongeza straika mpya kwenye kikosi chake. Hata hivyo, naye Mourinho hatabiriki. Lakini pia, tayari Arsenal wameshamkosa Julian Draxler ambaye […]

NI AIBU Z’BAR KUWA WASINDIKIZAJI MAPINDUZI CUP

MACHO na masikio ya mashabiki wengi wa soka hapa nchini yameelekezwa visiwani Zanzibar ambako kuna michuano ya Kombe la Mapinduzi. Michuano hiyo iliyoanza rasmi mwaka 2007, hakuna ubishi kuwa imekuwa msaada mkubwa kwa soka letu tangu kuanzishwa kwake. Moja kati ya sababu ambayo imekuwa ikitajwa na wadau wengi wa soka juu ya kushuka kwa soka letu ni kuwapo kwa idadi […]

SANAA INAELEKEA KUWA MWAJIRI MKUU, MIUNDOMBINU IBORESHWE

NA CHRISTOPHER MSEKENA NADHANI utakuwa umewahi kusikia habari za roboti kufanya huduma ya kusambaza vyakula kwenye migahawa  fulani iliyopo katika Bara la Asia hasa nchini China. Ni mafanikio yanayowafurahisha wanasayansi duniani kote huku kundi kubwa la vijana wenye taaluma ya uhudumu wa hoteli wakilia kwa kuwa vibarua vyao vipo shakani kutwaliwa na roboti hao. Ni dalili mbaya kwa wote wanaotegemea […]

KUNA SIKU MZEE BAKHRESA ATAUCHUKIA MPIRA!

NA OSCAR OSCAR HAKUNA jambo baya katika maisha ya mwanadamu kama kukata tamaa. Hatua hii hufikiwa pale mwanadamu anapojaribu kila njia kufanikisha jambo lakini matokeo yanakuwa kinyume na matarajio. Inasikitisha sana kuona miaka nane ya Azam FC kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara wakitwaa ubingwa mara moja. Inasikitisha kuona nguvu anazotumia mmiliki wa klabu hiyo, mzee Said Bakhresa, katika uwekezaji hazizai […]