Category: Maoni

KLINIKI YA WACHEZAJI AIRTEL ILETE TIJA

WACHEZAJI bora walioibuka katika mashindano ya Airtel Rising Stars, leo wanatarajiwa kuanza kliniki ya wiki moja ya mafunzo maalumu kuhusiana na masuala ya soka  yatakayofanyika jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yameandaliwa na Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), yaliyolenga kuibua vipaji chipukizi vya soka nchini. Nyota 65 wa mashindano hayo […]

TUNA KILA SABABU YA KUIFUATILIA AFCON 2017

LIBREVILLE, Gabon PAZIA la michuano ya AFCON kwa mwaka 2017 litafunguliwa leo kwa wenyeji Gabon kuvaana na Guinea-Bissau kwenye mchezo wa kwanza wa Kundi A. Tayari kila mmoja amekuwa akiongea la kwake kuhusu mataifa 16 yatakayoumana kuwania taji hilo kubwa kwa upande wa soka barani Afrika. Makala haya yamekuletea dondoo baadhi kuelekea kwenye fainali hizo zinazotarajiwa kuwa kali na za […]

ROONEY, JICHO LAKO LISITAZAME SURA ZAO BALI MIOYO YAO

NA HALID MTUMBUKA KUNA ukweli mmoja tu kwa sasa juu ya Wayne Rooney na Manchester United. Ukweli wenyewe ni kwamba, ameifikia ile rekodi aliyokuwa akiiwazia ingawa mwenyewe hakuwahi kuweka wazi juu ya kuwa na hamu ya jambo hilo, rekodi ya kumfikia Sir Bobby Charlton ya kuwa mfungaji bora wa muda wote ndani ya Manchester United. Bao lake dhidi ya Reading […]

AFCON 2019 TUSIPOANGALIA TUTAWAKILISHWA NA ALI KIBA AU DOGO JANJA

NA EZEKIEL TENDWA RATIBA ya kutafuta kufuzu kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka 2019 itakayofanyika nchini Cameroon, imeshatoka na Tanzania imeshajua itakaokutana nao kwenye kundi L ambalo ndilo walilopangiwa. Katika kundi hilo, timu yetu ya Taifa ‘Taifa Stars’ imepangwa sambamba na Cape Verde, Lesotho pamoja na Uganda ambao kwa bahati nzuri wao watashiriki michuano ya mwaka […]

TUMSAIDIE MALINZI MAANDALIZI FAINALI ZA U-17 MWAKA 2019

TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa fainali za vijana wenye umri chini ya miaka 17 (U-17) za Afrika zitakazofanyika hapa nchini mwaka 2019. Nafasi hiyo ya kuandaa fainali hizo, imepatikana baada ya jitihada zilizofanywa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi pamoja na viongozi wenzake, ikiwa ni sehemu ya kuamsha msisimko wa mchezo wa soka nchini ambao kwa […]

MWANZA UCHAGUZI UMEKWISHA PIGENI KAZI

NA HUSSEIN OMAR MWISHONI mwa wiki iliyopita Chama cha Soka Mkoa Mwanza (MZFA), kilifanya uchaguzi wake na kuwapata viongozi wao wapya watakaokiongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka minne ijayo ya kuletea maendeleo ya soka mkoani humo. Katika uchaguzi huo, Vedastus Lufano amepewa dhamana ya kuwa Mwenyekiti mpya wa MZFA baada ya kumbwaga Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha […]

YANGA, AZAM ZIELEKEZE NGUVU MICHUANO YA AFRIKA

YANGA imepata uzoefu  kwa kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea viwasini Zanzibar, licha ya kutolewa na Simba  kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 4-2 kufuatia sare tasa ndani ya dakika 90  katika  mchezo wa  hatua ya Nusu Fainali uliochezwa juzi usiku kwenye Uwanja wa Amaan. Kombe hilo la Mapinduzi lililoshirikisha timu tatu zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara; Azam, Simba […]

ZULU ‘MKATA UMEME’ KAMA JAJA TU!

NA ONESMO KAPINGA BILA shaka kichapo cha mabao 4-0 walichokipata Yanga kutoka kwa Azam FC katika mchezo wa makundi wa Kombe la Mapinduzi uliochezwa juzi usiku kwenye Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar, kitakuwa kimewakasirisha mashabiki wao. Ni kipigo kikubwa kwa timu kama  Yanga inayoundwa na nyota wengi wakiwamo wazawa na wageni wanajua kucheza mpira hasa ukizingatia walitoka kumpiga mtu mabao […]

TFF KAZENI MACHO FDL KUMEANZA KUHARIBIKA

LIGI Daraja la Kwanza imeshika kasi na sasa ipo katika mzunguko wa pili. Ligi hiyo inayochezwa katika makundi matatu ndiyo itatoa timu tatu zitakazopanda kucheza Ligi Kuu soka Tanzania Bara msimu ujao. Mshindi wa kila kundi kwenye ligi hiyo inayoshirikisha timu 24 zilizogawanywa kwenye makundi ya timu nane kila kindi, inapata nafasi ya kucheza Ligi Kuu. Hali ya kutaka kupanda […]

KICHUYA MWINGINE APATIKANE KOMBE LA MAPINDUZI

NA WINFRIDA MTOI KOMBE la Mapinduzi ni moja ya michuano yenye mvuto, kutokana na kushirikisha timu mbalimbali na inafanyika wakati ambao  Ligi Kuu ya Tanzania Bara imepamba moto. Hali hiyo inazifanya timu za Bara  kuingia kwenye michuano hiyo zikiwa na  nguvu kubwa ya kutaka kuchukua kombe hilo ili kuwa na chachu ya kufukuzia ubingwa wa Ligi Kuu Bara, pia timu […]