Category: Maoni

KLABU ZITUNZE KUMBUKUMBU ZA WACHEZAJI

SIMBA imenusurika kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho (FA), baada ya Polisi Dar es Salaam kuwasilisha rufaa kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wakipinga kumchezesha beki wa timu hiyo, Novat Lufunga, katika mchezo uliochezwa Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Uhuru. Polisi Dar es Salaam walichukua uamuzi huo, baada ya kufungwa mabao 2-0, lakini wakiwa na ushahidi kuhusu rufaa yao […]

SABABU TATU ZA WENYEJI GABON KUONDOLEWA MAPEMA AFCON

LIBREVILLE, Gabon USIKU wa Jumapili ya wikiendi iliyopita, kikosi cha timu ya taifa ya Gabon kilikuwa ni cha kwanza kutolewa hatua ya makundi ya Afcon, baada ya kulazimishwa suluhu na Cameroon, ambapo mara ya mwisho kwa mwenyeji kutolewa hatua hiyo ni Tunisia mwaka 1994. Unajua sababu zilizosababisha wenyeji hao wanaoongozwa na nahodha wao mshambuliaji hatari wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang? […]

WAAMUZI WASIPINDISHE SHERIA 17 ZA SOKA

MWAMUZI Hussein Athumani kutoka mkoani Katavi, ameondolewa katika orodha ya waamuzi wanaochezesha Ligi Kuu Tanzania Bara, kwa maelekezo kwamba alishindwa kasi ya mchezo kati ya Majimaji na Yanga. Mchezo huo ulimalizika kwa Yanga kushinda bao 1-0 uliochezwa hivi karibuni kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea na Athumani kuonekana kushindwa kabisa kwenda na kasi ya mchezo. Mwamuzi huyo anadaiwa kuchezesha mchezo […]

TATIZO NI TOFAUTI YA VIPAUMBELE VYA KOCHA NA VIONGOZI TFF

NA LEONARD MANG’OHA SIKU kadhaa zilizopita Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilisitisha mkataba wa aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwassa “Master.” Kusitishwa kwa mkataba wa Mkwassa kulionekana kuibua hisia na maswali kadhaa miongoni mwa wapenda soka wengi nchini, wengine wakihusisha uamuzi huo na misimamo ya kocha huyo ambayo amekuwa akiionyesha akiwa kocha wa Stars. […]

MALINZI USIMWONEE SONI KIM PAULSEN

NA HONORIUS MPANGALA KUNA mambo hayawezekani katika maisha ya kila siku ya binadamu, lakini kwa sababu ya misimamo kwenye soka tuliko sisi inawezekana, sidhani kama waliotalikiana wanaweza kurejeana kirahisi kwa sababu ya maendeleo ya mmoja wao, kinachotokea ni kumwombea mabaya mwenzako avurunde zaidi ili kesho aje kukusujudia na wewe kujiona umepatia kufanya maamuzi. Mchezo wa soka ni kati ya michezo […]

PAYET JIANGALIE, HAWA WENZAKO WALIJUTIA MAAMUZI YAO BAADAYE

LONDON, England SUALA la mchezaji kulazimisha kuondoka ndani ya klabu yake na kuanzisha visa huwa ni nadra kutokea na iwapo likitokea, ni lazima kuwe na mizozo inayosababisha timu husika kupoteza mwelekeo katika ligi. Aidha, mzozo huo hauwezi kuwa mkubwa iwapo mchezaji ambaye analazimisha kuondoka hana nyota ya kupendwa ndani ya klabu. Ni lazima awe staa anayetegemewa kutokana na nafasi yake […]

SIMBU, MAGDALENA WAKIWEZESHWA MAPEMA TANZANIA ITANG’ARA LONDON

NA HASSAN DAUDI FILBERT Bayi ni miongoni mwa wanariadha wachache waliowahi kuipeperusha vema bendera ya Tanzania katika michuano ya kimataifa. Mwaka 1973 akawa mshindi wa mbio za mita 1500 katika michuano ya All-Africa Games kabla ya kutetea ubingwa wake miaka mitano baadaye. Bayi mzaliwa wa Arusha, alitwaa medali ya dhahabu katika michuano ya Jumuiya ya Madola na hiyo ilikuwa mwaka […]

MAANDALIZI YA KWENDA CAMEROON YAANZE

FAINALI zijazo za Kombe la Afrika (Afcon) zimepangwa kufanyika  mwaka 2019 nchini Cameroon, huku Tanzania ikiwa kwenye Kundi L pamoja na Uganda, Lesotho na Cape Verde. Katika fainali zinazoendelea nchini Gabon, Tanzania ilishindwa kufuzu baada ya kufanya vibaya kwenye kundi lao G lililoundwa na Misri, Nigeria na Chad ambao baadaye walijitoa. Tanzania ilianza vibaya kuwania kufuzu fainali zinazofanyika Gabon, baada […]

AFCON ILITUHITAJI TANZANIA NA ITATUSUBIRI CAMEROON 2019- 1

WIKIENDI ya soka ilianzia pale Libreville, Gabon, kabla ya utamu wake kumalizikia Old Trafford, Manchester, England… Barani kwetu Afrika, Pierre-Emerick Aubameyang, akiwa kama nahodha mkuu wa timu ya taifa ya soka ya Gabon, aliwakaribisha mastaa wenzake katika fainali za Mataifa Afrika. Ni michuano ya kumsaka bingwa wa Afrika. Karibu Afrika! Nilimkumbuka babu Hassan Shehata, mkongwe wa soka la Afrika aliyewapa […]

NI WAKATI WA KUANZISHA MASHINDANO YA KUDANSI KITAIFA 2O17

HERI ya Mwaka Mpya msomaji wangu mpenzi, naamini umeuona mwaka kwa uzuri na kwa matumaini mapya juu ya malengo uliyojiwekea. Tumekutana tena leo kwenye makala haya kujadili masuala ya sanaa ya kudansi na ile ya maonesho kwa ujumla. Leo nataka niwakumbushe wadau wote wa sanaa hii ya kudansi kwamba kuna sehemu tumekosea. Labda niwape kumbukizi kidogo ili wasomaji wangu muweze […]