Category: Maoni

Anachofanya Samatta kiwe funzo kwa wengine

NA MWANDISHI WETU HONGERA Mbwana Samatta kwa mchango wako katika klabu ya KRC Genk ambayo mwishoni mwa wiki ilikabidhiwa kombe, baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Ubelgiji. Dalili za Genk kutwaa ubingwa huo kwa mara ya nne sasa, ilianza kuonekana tangu Septemba mwaka jana walipoongoza msimamo wa Ligi ya Ubelgiji. Wamekaa kileleni kwa muda mrefu na hata katika hatua […]

Wagombea Yanga wafanye kampeni za kiustaarabu

WAGOMBEA wa Yanga leo wataanza kujinadi kwa wanachama kwa lengo la kuomba kura ili waweze kuchaguliwa katika uchaguzi utakaofanyika Jumapili kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam. Katika uchaguzi huo, nafasi ya mwenyekiti inayowaniwa na Jonas Tiboroha na Mbaraka Igangula na  Mshindo Msolla, ndiyo itakayokuwa na ushindani mkali. Tunasema hivyo kutokana na mwenyekiti ni […]

TFF waangalie utaratibu uteuzi wa vikosi vya Taifa

NA MWANDISHI WETU WAKATI fainali ya michuano ya vijana Afrika chini ya umri miaka 17 ikitarajia kuchezwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa, wadau wa soka nchini wamelaumu uteuzi wa timu ya Serengeti Boys. Serengeti Boys ilitolewa katika hatua ya makundi baada ya kufanya vibaya michezo yote mitatu iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Baadhi ya wadau wa Zanzibar […]

Wizara izikumbuke sanaa za ufundi na ubunifu

NA CHRISTOPHER MSEKENA HIVI karibuni hotuba ya makadirio ya bajeti ya mwaka 2019/20 ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ilisomwa bungeni jijini Dodoma na Waziri Dk. Harrison Mwakyembe. Miongoni mwa mambo yaliyoibuka katika hotuba hiyo ni wasanii marehemu kama Steven Kanumba na Mzee Majuto kulipwa fedha zao za fidia baada ya upitiaji upya wa mikataba ya kazi walizowahi […]

Kama unaishangaa Serengeti Boys huwezi kuzipongeza Simba, Stars

NA HASSAN DAUDI USHINDI wa mechi mbili tu ungetosha kuipeleka Tanzania katika fainali za Kombe la Dunia za vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitakazofanyika mwaka huu nchini Brazil. Kuiweka vizuri, ndani ya mwaka mmoja, historia tatu zingekuwa zimeandikwa kwani tayari Simba na Stars zilishachukua nafasi. Wekundu wa Msimbazi walitinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara […]

Hapa Simba watakuwa wameimaliza kabisa TP Mazembe

NA HASSAN DAUDI YAPO mengi yanayoendelea nchini, vikiwamo vituko vya Pierre Liquid huko mitandaoni, lakini yote yatawekwa kando saa chache zijazo, wakati Simba SC watakaposhuka dimbani kumenyana na TP Mazembe. Ni dakika 90 za mtanange wa kwanza wa hatua ya robo fainali ya mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Afrika, michuano mikubwa zaidi kwa ngazi ya klabu barani humu. Kwa ufupi, […]

Kivuli cha Taifa Stars kinaweza kuibeba Tanzania Mbio za Nyika

NA WINFRIDA MTOI JUMLA ya wanariadha16, wanatarajia kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Mbio za Nyika ‘World Cross Country Championships’ yanayotarajia kutimua vumbi kesho nchini Denmark. Wanariadha hao ni Marko Monko, Faraja Damas, Joseph Panga, Emmanuel Giniki, Gabriel Geay, Francis Damiano, Yohana Elisante, Failuna Matanga, Magdalena Shauri, Angelina Tsere, Cecilia Ginoka, Marselina Mbua, Amina Mgoo, Anastazia Dolomongo, Aisha Malengani na Natalia […]

TUMEFUZU AFCON, SASA TUJIPANGE

TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imefanikiwa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon 2019) zitakazofanyika mwaka huu nchini Misri, baada ya kuifunga mabao 3-0 Uganda katika mchezo wa marudiano wa  Kundi L, uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Tanzania imeungana na Uganda iliyotangulia kufuzu michuano hiyo, baada ya timu nyingine kwenye kundi hilo, Cape Verde […]

Chonde wachezaji Stars wasituangushe Jumapili

TIMU ya Taifa, Taifa Stars, inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterani, jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kusaka tiketi ya kufuzu fainali ya Mataifa ya Afrika (Afcon). Taifa Stars ambayo iko Kundi L pamoja na Lesotho, Uganda na Cape Verde, inajiandaa kucheza na Waganda katika mchezo wa marudiano utakaochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa […]