Category: Maoni

Hongera Yanga, ‘vidonge’ vya Mzee Kikwete visipuuzwe

UKUMBI wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam, ulikuwa wa aina yake juzi, kwa mashabiki, wanachama, wachezaji wa Yanga, viongozi wa klabu hiyo na serikali pamoja na wadau wa soka nchini. Kwa watu wa Yanga, ilikuwa siku ya kipekee kwao ambapo waliitumia kuendesha harambee iliyolenga kuchangisha fedha za kuisadia klabu yao, hasa kipindi hiki cha usajili. BINGWA tukiwa kama wadau […]

Dk. Mwakyembe amewakumbusha jambo muhimu TFF

NA WINFRIDA MTOI RATIBA ni moja ya changamoto kubwa iliyojitokeza katika msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2018/2019, uliomalizika hivi karibuni, Simba wakitawazwa kuwa mabingwa kwa mara ya pili mfululizo. Changamoto hiyo ilionekana kumgusa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ambaye ameonya Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), kuitafutia ufumbuzi. Dk. Mwakyembe alionekana kukerwa na ratiba ya msimu […]

UAMUZI WA AMUNIKE UHESHIMIWE

NA MWANDISHIN WETU JUZI, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, alitangaza kikosi cha mwisho cha kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon), itakayoanza Juni 21, mwaka huu, nchini Misri. Awali, Amunike aliita kikosi cha wachezaji 39 kujiandaa na michuano hiyo, kabla ya kufanyika kwa mchujo na kuwaondoa nyota saba, wakiwamo Jonas Mkunde  (Simba) na […]

KAGERA, MWADUI ‘PLAY OFF’ IWE FUNZO

NA MWANDISHI WETU TIMU za Kagera Sugar na Mwadui, zitaendelea kuwamo Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao, baada ya juzi kupata ushindi katika michezo ya ‘play off’ iliyochezwa juzi kwenye viwanja viwili tofauti nchini. Kagera Sugar ilishika nafasi ya 18 na Mwadui ikimaliza nafasi ya 17 katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, hivyo kuangukia kapu la ‘play off’ kucheza na […]

Solskjaer akiiba kengele aweke pamba masikioni

NA AYOUB HINJO NI kwenye matatizo pekee ndipo mwanadamu hufahamu nguvu na uwezo ulio ndani yake. Usiyachukie wala usichukie kwanini wewe umepata tatizo, Mungu hajawahi kumpa mja wake mzigo asioweza kuubeba. Linapokuja tatizo, furahi, kwa maana wakati wako wa kuigundua nguvu iliyo ndani yako umewadia. Mwandishi wa vitabu Mmarekani, Hellen Keller, akiwa na miezi 19 tu duniani, alipata ulemavu wa […]

YANGA SC WASIPUUZIE USHAURI WA SERIKALI

N A MWANDISHI WETU JUZI, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini, Harrison Mwakyembe, alitoa ushauri kwa uongozi mpya wa Yanga kuhakikisha wanaiongoza klabu hiyo kwa weledi mkubwa. Yanga ilipata uongozi mpya Mei 5, mwaka huu, baada ya kufanyika uchaguzi mkuu katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu […]

Ishu ya nafasi nne CAF ilianzia hapa

Na KELVIN LYAMUYA BILA shaka unakumbuka Simba ilivyofanikiwa kutinga robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita, baada ya kuvuka salama kwenye kundi lao, ikiungana na Al Ahly ya Misri. Simba ilifanikiwa kuwa timu ya kwanza kutoka Tanzania kucheza robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika tangu ilipoboreshwa mwaka 1997. Kiwango kilichooneshwa na Simba kitabaki kwenye historia ya soka la Tanzania. […]

Tukianzia hapo kwa Samatta, Kiba itapendeza zaidi

NA HASSAN DAUDI JUZI, mashabiki wa soka na burudani nchini walikuwa ‘bize’ kwa dakika 90 za mtanange wa hisani kati ya timu zilizoundwa na mastaa Mbwana Samatta na Ali Kiba. Haukuwa mtanange wa Ligi Kuu au mashindano yoyote, bali vita ya pande mbili hizo ililenga kuchangisha fedha kwa ajili ya walemavu. Akiwa na kikosi chake, Samatta anayeichezea Genk ya Ligi […]

Wachezaji wasikurupuke kusaini mikataba mipya

DIRISHA kubwa la usajili kwa ajili ya msimu ujao wa  Ligi Kuu Tanzania Bara, limeanza kunukia baada ya baadhi ya klabu kuingia katika mawindo ya kusaka nyota wa kuwasajili. Licha ya kwamba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) halijatangaza rasmi kuanza kwa msimu mpya wa usajili, tayari baadhi ya klabu zimeanza usajili wa awali kwa lengo la kuboresha vikosi vyao. Usajili […]

Simba wasibweteke, Yanga wanaweza kutikisa usajili 

NA WINFRIDA MTOI PAZIA la Ligi Kuu Tanzania Bara linatarajia kufungwa kesho kwa timu zote 20 zinazoshiriki ligi hiyo kushuka dimbani katika viwanja tofauti nchini. Ligi hiyo iliyoanza Agosti mwaka jana, imekuwa na matukio mbalimbali yaliyojitokeza kubwa likiwa ni ukata  kwa  klabu nyingi kutokana na kukosa  mdhamini mkuu kama ilivyozoeleka. Kwa muda mrefu, Simba na Yanga wamekuwa ni watawala wa […]