Category: Makala

HAWA NI MWAROBAINI WA KIUNGO WA ULINZI YANGA

NA MWANDISHI WETU VIUNGO wanaocheza chini ndio kiunganishi cha safu ya ulinzi na ushambuliaji katika timu na kama wakishindwa kufanya kazi yao vizuri mpira huwa unapoteza ladha kabisa. Timu inashambuliwa mara nyingi na hata kuwa katika hatari ya kupoteza mchezo. Kwa muda mrefu sasa kikosi cha Yanga kimekosa kiungo asilia wa chini, yaani namba sita au kiungo wa ulinzi. Eneo […]

Kwanini kukosekana kwa Ibrahimovic ni habari mbaya kwa mashabiki wa Arsenal

MANCHESTER, England MANCHESTER United watamkosa Zlatan Ibrahimovic watakapopambana na Arsenal, mchana wa leo, lakini hii inaweza kuwa habari njema kwa mashabiki wao. Unajua ni kwanini? Kinda Marcos Rashford ataanza kwenye eneo la ushambuliaji akiwa straika wa kati. Hii itakuwa kumbukumbu kwa kinda huyo, aliyeanza pambano lake la kwanza la Premier League dhidi ya Arsenal msimu uliopita na kufunga mabao mawili […]

HIMID MAO, MZABE KIBAO MUDATHIR YAHYA

NA HALID MTUMBUKA NI mchezaji wa kipekee sana, ni binadamu mwenye nidhamu kimwonekano hadi kimchezo. Mara nyingi hucheza huku jezi yake ikiwa imechomekewa kwa dakika zote tisini, yupo mmoja tu anayeweza kuishi hivi kwa dakika zote uwanjani. Aliwahi kuulizwa juu ya kucheza bila jezi yake kuchomoka kwa dakika zote uwanjani, alichokijibu kilikuwa ni rahisi tu, alisema huwa hajui kama jezi […]

Kwa heri Wawa soka la bongo ‘litakumiss’

NI mara chache kwenye soka la bongo mchezaji wa kimataifa ametokea na kukubalika kwenye macho ya wadau na mashabiki wote wa soka nchini. Licha ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kuvutia wachezaji wengi wa kigeni, lakini wale ambao wamefanikiwa kubaki kwenye akili za wengi ni wachache sana (hii inatokana na 10% zinazopigwa mara kwa mara kwenye usajili). Na […]

Miaka 10 VPL… Bado wapo wapo sana

NA ZAINAB IDDY MZUNGUKO wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2016/17, umemalizika huku baadhi ya wachezaji chipukizi wakionekana kufanya vizuri sana kwenye timu zao. Licha ya vijana kutawala soka nchini, lakini kama waswahili wasemavyo ‘hakuna kijiji kisichokuwa na wazee’ na siku zote sehemu yenye wakongwe hakuna kinachoharibika, ndivyo hali ilivyo VPL kutokana na uwepo […]

Tusimchukulie poa yule ‘chotara wa Zimbabwe’

HARARE, Zimbabwe MOJA kati ya matukio ya dharau kabisa mtu anaweza kukufanyia kwenye soka ni kukupiga bonge la bao, halafu anashangilia kama Cristiano Ronaldo kisha anaomba ‘sub’. Wazimbabwe wametufanyia hivi! Dakika ya 55, Matthew Rusike akiwa nje kidogo ya eneo la 18, alipokea pasi safi kutoka kwa Nyasha Mushekwi na kuamua kunyoosha msuli wake, akaachia bonge la shuti. Nina hakika […]

Wachezaji waulizwe kinachoimaliza Stars

NA HASSAN DAUD WENGI tumekuwa bize sana siku hizi kutokana na ugumu wa maisha. Hasa sisi wadau wa soka, huenda tumekuwa tukipitwa na baadhi ya matukio muhimu ya mchezo huo kutokana na hali hiyo. Kuna matukio mawili ambayo yametokea katika siku za hivi karibuni ambayo si rahisi kukwepa kuyazungumzia, licha ya ubize wetu. Kwanza, ilitoka orodha ya viwango vya ubora […]

Sababu za Ronaldo kuanza majukumu akiwa mdogo

Madrid, Hispania MALEZI ya nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, yalikuwa na changamoto nyingi na yalihitaji uvumilivu ambao leo unamlipa na anafaidi matunda yake. Mchezaji huyo wa Ureno aliyezaliwa kitongoji cha Santo Antonio katika kisiwa cha Madeira, alipewa jina la ‘Ronaldo’ ambalo ni jina la Rais wa zamani wa Marekani, Ronald Reagan, kwa kuwa baba yake mzazi, Jose Dinis Aveiro, […]

Balotelli huyu wa Nice achana naye

NICE, Ufaransa KOCHA wa Nice, Lucien Favre, alimpumzisha Mario Balotelli katika mchezo dhidi ya Nantes siku 10 zilizopita, lakini mchezaji huyo wa Italia alitoka akiwa na tabasamu kubwa. Kumtoa dakika ya 75 ndio ilikuwa njia pekee ya kuweza kumpima Balotelli, ambapo kipimo hicho kilionyesha kwamba ana furaha sana kuwapo Nice. Pia kumekuwa na mabadiliko makubwa hata katika maisha yake ya […]

Je, ni kweli Ulimwengu ulikataa ofa Mazembe?

NA SELEMAN SHINENI MDOGO wangu Thomas Ulimwengu, nakumbuka wakati ukiwa TP Mazembe pamoja na ‘pacha’ wako Mbwana Samatta, kila Mtanzania aliwataja nyinyi kama mfano wa wanasoka vijana nchini. Nyinyi ndiyo mlikuwa alama ya soka la Tanzania ambalo miaka nenda rudi limeshindwa kuzalisha wachezaji wa kutikisa nje ya mipaka ya taifa letu na tuliamini kuwa kwa weledi mliokuwa nao siku moja […]