Category: Makala

SOKA LETU NA HATIMA YETU

NA HONORIUS MPANGALA BINADAMU mara baada ya kuzaliwa kitu pekee anachoweza kukijua kilicho mbele yake ni kifo tu, mengine yaliyobakia inakuwa majaliwa ya Mwenyezi Mungu kuyafanikisha au kuyafikia. Nani anamkumbuka Iddi Mtiginjora kwa nyakati hizi? Ameshasahaulika vichwani mwa wadau wa soka, lakini kwangu ni kama stelingi aliyekufa mwanzo wa picha na kuacha majambazi wakisonga. Mtiginjora aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya […]

UKWELI WA KILICHOMFANYA OSCAR AKUBALI KWENDA CHINA

BILA shaka habari inayotikisa vichwa vya wapenzi wa soka duniani kwa sasa ni uhamisho wa Mbrazil Oscar aliyeihama Chelsea na kutimkia katika klabu ya Shanghai SIPG inayoshiriki ligi kuu nchini China. Mbrazil huyu amesajiliwa kwa dau la pauni mil 60 na atakuwa akipokea mshahara wa pauni 400,000 kwa wiki, kiwango kinachomfanya alipwe zaidi ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo. Kila […]

JOE SMITH JR. ALIVYOMSTAAFISHA NGUMI HOPKINS

NEW YORK, Marekani MARA nyingi huwa ni ndoto za kila mwanamichezo kustaafu pindi anapokuwa amepata mafanikio kiasi cha kutosha. Jambo hilo limekuwa likishuhudiwa hata katika mchezo wa masumbwi, ambapo bondia huwa anaamua kucheza pambano lake la mwisho kabla ya kutundika glovu zake kwa ushindi. Hata hivyo, wakati mwingine mambo huwa yanakuwa tofauti na malengo ya bondia anapojikuta akiambulia kipigo na […]

KUMBE USHAURI WA CAPELLO NDIO UNAOMBEBA CONTE

KWA sasa kocha wa Chelsea, Antonio Conte, ndiye habari ya mjini, baada ya kuiwezesha timu hiyo kucheza michezo 11 bila kufungwa. Rekodi hiyo imekuja ikiwa ni baada ya msimu uliopita timu hiyo kufanya vibaya na huku ikiuanza msimu huu kwa kuchapwa na Liverpool na Arsenal. Hata hivyo, baada ya kocha huyo kubadili mfumo na kuanza kutumia wa 3-4-3, timu hiyo […]

KUMKOSOA OZIL UNAKOSEA

LONDON, England ANGALIA jinsi anavyogusa mpira na anavyomtoka mpinzani wake, hayo ni baadhi ya mambo yanayomfanya Mesut Ozil atajwe kama namba 10 bora duniani. Ozil aliwasili Arsenal akitokea klabu bora duniani ya Real Madrid kwa dau la pauni milioni 42.5 mwaka 2013. Kumekuwa na ukosoaji sana juu ya mchango wake tangu atue Arsenal mara ya kwanza, huku mwandishi mmoja akimshutumu […]

SIRI YA WACHINA KUTEKA ULIMWENGU WA SOKA HII HAPA

BEIJING, China WIKI iliyopita timu ya Shanghai SIPG ilikubali kuilipa Chelsea pauni milioni 58 kumchukua Oscar, baada ya  Carlos Tevez kuamua kuiaga klabu yake  kipenzi ya Boca Juniors na kwenda kujiunga na timu ya Shanghai Shenhua kwa ajili ya kuicheza kuanzia msimu ujao. Katika makubaliano hayo, Oscar atakuwa miongoni mwa wachezaji wanaolipwa fedha nyingi kutokana na kuwa atakuwa akilipwa pauni […]

MATUKIO YA MICHEZO YALIYOTIKISA AGOSTI 2016

NA MWANDISHI WETU, AGOSTI ilikuwa mwezi wa Olimpiki na kama taifa tulipeleka wawakilishi wetu, je, tuna cha kujivunia? BINGWA leo linakuletea matukio ya michezo yaliyotikisa Agosti 2016 hii ikiwa ni mwendelezo wa kujikumbusha matukio muhimu tunapokaribia kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017. Simba na Simba Day yao Katika kusherehekea miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Klabu ya Simba, timu hiyo […]

TBBF WAGEUKIA VYUO VIKUU

NA ZAINAB IDDY PENGINE kama kuna mchezo ambao nao uliwahi kupendwa katika miaka ya 1990, ni ule wa kutunisha misuli kwani ulitajwa kila kona kiasi cha kupata wadhamini lukuki. Katika kipindi hicho, vilifunguliwa vituo vingi vya mazoezi ya viungo (gym) na kuanzishwa pia mashindano katika wilaya, mkoa na taifa. Kwa miaka ya hivi karibuni, hali imekuwa tofauti kwani licha ya […]

MATUKIO YA MICHEZO YALIYOTIKISA JULAI 2016

NA MWANDISHI WETU ANAYEFANYA kazi nzuri hupokea zawadi na Julai, hususan katika Ligi Kuu Bara, tulishuhudia tuzo zikitolewa. Hii ni moja kati ya matokeo mengi ya michezo yaliyotokea Julai na BINGWA leo linakuletea matukio ya michezo yaliyojiri Julai 2016, tukijiandaa kuukaribisha mwaka 2017. *Serengeti Boys si ya mchezo mchezo Timu ya soka ya taifa ya vijana wenye umri chini ya […]

BENTEKE UKIMSAJILI TU, IMEKULA KWAKO

LONDON, England KIBONGO bongo, Christian Benteke, angesugua sana kwenye mechi za mtaani, hakuna kocha wa ligi kuu ambaye angekuwa na ujasiri wa kumsajili. Unajua kwanini? Katika timu tatu zote ambazo straika huyu wa Ubelgiji amezichezea, makocha waliomsajili vibarua vyao viliota nyasi. Benteke alijiunga na Aston Villa mwaka 2012, kisha akahamia Liverpool miaka mitatu baadaye na sasa anakipiga katika klabu ya […]