Category: Makala

De Rossi ; Nahodha shupavu anayeacha historia nzito AS Roma

ROME, Italia MSIMU huu umekuwa mgumu kwa timu ya AS Roma, ingawa ni jambo linalotegemewa katika mchezo wa soka. Kitu pekee ambacho Waitaliano hao hawakukitarajia ni kuondoka kwa nahodha wao, Daniele De Rossi. De Rossi ambaye amedumu na ‘Giallorossi’ hao kwa muda wa miaka 18, akiitumikia katika michezo zaidi ya 600, alitangaza kuwa ataiacha klabu yake hiyo ifikapo mwishoni mwa […]

Solskjaer akiiba kengele aweke pamba masikioni

NA AYOUB HINJO NI kwenye matatizo pekee ndipo mwanadamu hufahamu nguvu na uwezo ulio ndani yake. Usiyachukie wala usichukie kwanini wewe umepata tatizo, Mungu hajawahi kumpa mja mzigo asioweza kuubeba. Linapokuja tatizo, furahi, kwa maana wakati wako wa kuigundua nguvu iliyo ndani yako umewadia. Mwandishi wa vitabu Mmarekani, Hellen Keller, akiwa na miezi 19 tu duniani, alipata ulemavu wa macho […]

Kumbe usajili wa Domayo Azam ulitaka kumtoa roho Jemedari 

NA ABDULAH MKEYENGE SIMULIZI ya usajili wa kiungo wa Azam FC, Frank Domayo ‘Chumvi’, kujiunga na timu hiyo mwaka 2014 akitokea Yanga haikuwa nyepesi hata kidogo, ilikuwa ni jasho na damu. Usajili huo uliowakera mashabiki wa Yanga na kumpa wakati mgumu aliyekuwa meneja wa kikosi hicho, Jemedari Said ambaye ndiye aliyecheza sinema nzima ya ‘kininja’ kuhakikisha Domayo anakuwa mchezaji wa […]

Timu hizi zilisubiri hadi siku ya mwisho kutwaa taji EPL

LONDON, England BAO murua la nahodha wa Manchester City, Vincent Kompany, lilirudisha matumaini ya timu hiyo kutwaa taji la Ligi Kuu ya England msimu huu. Ulikuwa usiku ambao kocha wa kikosi hicho, Pep Guardiola, alifufua hisia mpya za kuamini kuwa wana uwezo wa kutwaa taji hilo kwa mara ya pili mfululizo, huku ikiwa ni mara ya kwanza kwa Manchester City […]

NDIYO ZAO Barca kitu gani, mbona Liverpool kupindua meza kawaida tu!

MERSEYSIDE, England UKWELI ni kwamba hakuna aliyekitarajia kilichotokea usiku wa kuamkia jana pale Anfield, wakati Liverpool wakifanikiwa kuingia fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Baada ya kuchapwa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza kule Hispania, wengi walisubiri kuiona safari ya Liver ikiishia Uingereza mbele ya wakali Barcelona. Badala yake, Liver wakiwa bila mastaa wake wawili, Roberto Firmino na Mohamed Salah, […]

GARI LIMEWAKA Samatta ameibeba tuzo iliyowatoa wakali kibao Ulaya

NA HASSAN DAUDI NYOTA ya nahodha wa Taifa Stars imezidi kung’ara huko barani Ulaya na hiyo ni baada ya juzi kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora kwa Wanasoka wenye asili ya Afrika, katika Ligi Kuu ya Ubelgiji. Samatta mwenye umri wa miaka 26, aliinyakua tuzo hiyo kutokana na mchango wake mkubwa kwa kikosi cha Genk msimu huu, akiwa […]

Simba kucheza na Sevilla ya LaLiga ni historia ya aina yake

NA MWANDISHI WETU MEI 23, mwaka huu ni siku ambayo inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa timu ya Simba na soka la Tanzania kwa ujumla kutokana na mechi moja kubwa ya kirafiki ya kimataifa itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mechi hiyo ya kirafiki ya kimataifa imeandaliwa na Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa ambayo itawaleta nchini mabingwa […]

Uwanja wa Kaunda usitumike kwenye kampeni

NA ZAITUNI KIBWANA MIAKA nenda rudi uwanja wa Yanga unaotajwa mara kwa mara kuwa utajengwa Jangwani, umekuwa ni kama kampeni ya watu kuchaguliwa uongozi katika klabu hiyo. Ni zaidi ya miaka saba, Yanga wanaongelea kujenga Uwanja wa Kaunda, lakini utakuwa ni moto moto kujengwa unapofikia uchaguzi wa klabu hiyo. Lakini uchaguzi wa klabu hiyo ukipita mipango ya kujenga uwanja huo […]

Dusan Tadic; Jembe linalofaa kumrithi Sanchez Old Trafford

LONDON, England HATIMA ya Alexis Sanchez katika kikosi cha Manchester United iko shakani, ikielezwa kuwa anaweza kuondoka zake wakati wa majira ya kiangazi. Hali ni mbaya kwa nyota huyo wa zamani wa Arsenal kwani tangu kuanza kwa msimu huu, amefunga bao moja pekee katika mechi za Ligi Kuu, licha ya mshahara mnono wa pauni 400,000 anaolipwa kwa wiki pale Old […]

Huko EPL zimebaki mechi mbili tu, nani kutwaa ubingwa, kushuka daraja, kuingia ‘top four’ au kufuzu Europa?

LONDON, England MAMBO yanazidi kunoga katika Ligi Kuu ya England, mbio za ubingwa si rahisi kuzitabiri, upande mwingine zipo timu zinajinasua kushuka daraja msimu huu, pia wapo wanaohitaji kuingia ‘top four’ ili kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Ukiacha vyote hivyo, kuna timu ambazo zitapambana kwa ajili ya kutafuta tiketi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Europa kwa msimu […]