Category: Latest News

Sharapova ajiweka pembeni French Open

PARIS, Ufaransa NYOTA hatari wa mchezo wa tenisi kwa upande wa wanawake, Maria Sharapova, amejitoa katika michuano ya mwaka huu ya French Open. Bibiye huyo mwenye umri wa miaka 32, aliutangaza uamuzi wake huo juzi, akieleza kuwa umetokana na tatizo lake la bega. Mapema mwaka huu, Sharapova anayeshika nafasi ya 35 katika viwango vya ubora duniani alifanyiwa matibabu lakini inaonekana […]

Berahino kitanzini kwa ulevi

LONDON, England MWANASOKA anayeichezea Stoke City, Saido Berahino, ameingia matatani baada ya kunaswa akiendesha gari akiwa amekunywa pombe. Mkali huyo alikuwa amezidisha mara tatu ya kiwango kinachotakiwa wakati akiwa ndani ya Range Rover yake katika mitaa ya jijini London. Tayari ameshafungiwa kuendesha usafiri huo kwa miezi 30, adhabu iliyokwenda sambamba na faini ya pauni 75,000.

Griezmann amchefua bosi Atletico

MADRID, Hispania RAIS wa Atletico Madrid, Enrique Cerezo, ameeleza kusikitishwa kwake na uamuzi wa Antoine Griezmann, kusema ataondoka klabuni hapo. Griezmann aliitangaza hatua yake hiyo, akisema huu utakuwa msimu wake wa mwisho akiwa na Atletico aliyojiunga nayo mwaka 2014 akitokea Real Sociedad. “Ni zaidi ya hasira, nimesikitishwa. Nilifikiri Antoine angekuwa na muda mrefu Atletico,” alisema bosi huyo.

Ugonjwa wa tumbo wamkosesha Sarri safari ya Marekani

LONDON, England KOCHA Maurizio Sarri amelazimika kuikosa safari ya Chelsea kwenda kutembelea jumba la makumbusho la Holocaust Memorial lililopo nchini Marekani, baada ya kukumbwa na ugonjwa wa tumbo. Sarri alikutana na hali hiyo wakati timu yake hiyo ya Chelsea ikianza ziara ya kujiandaa na msimu ujao, ambapo mapema wiki hii walikipiga na New England Revolution katika mchezo wa krafiki. Hata […]

De Jong aagwa kifalme Ajax

AMSTERDAM, Uholanzi KIUNGO wa Ajax, Frenkie de Jong, ameagwa kifalme na mashabiki wa timu hiyo wakati akijiandaa kwenda kujiunga na klabu yake mpya ya Barcelona. Kiungo huyo Mholanzi alikuwa na mchango mkubwa hadi Ajax ilipofanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya nchi hiyo, Eredivisie, na aliiwezesha kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Ulaya. Wakati ada yake ya usajili ya pauni […]

Vidal anasa kwa kimwana mtunisha misuli

MADRID, Hispania NYOTA wa Barcelona, Arturo Vidal, amenasa kwa kimwana mtunisha misuli raia wa  Colombia, Sonia Isaza, wakionekana kuponda raha katika fukwe za kifahari nchini Marekani. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, kimwana huyo alitupia picha juzi kwenye mtandao wake wa kijamii wa Istagram akiwa na nyota huyo wakiwa wanaota jua katika ufukwe mmoja uliopo California. Vidal alishawahi kutangaza kutengana […]