Category: Latest News

Kerr alia na Tambwe

KOCHA Mkuu wa Simba, Dylan Kerr, amelia na bao la mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe kuwa ndilo lililowanyong’onyesha na kujikuta wakipoteza mchezo dhidi ya watani wao hao wa jadi Jumamosi iliyopita. Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga ilishinda mabao 2-0, jingine likiwekwa kimiani na Malimi Busungu. Akizungumzia mchezo huo, […]

Pluijm: Tutavunja mwiko Moro J5

BAADA ya juzi kufanikiwa kuwalaza Simba mabao 2-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm, amesema kikosi chake kipo kamili kuvunja mwiko wa kufungwa na Mtibwa Sugar ya Morogoro. Yanga watashuka kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kuwavaa Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu […]

SIRI YA MAUAJI SIMBA

WACHEZAJI wanne wa Yanga wamehusika moja kwa moja katika ushindi wa mabao 2-0 walioupata juzi dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Pamoja na ukweli kwamba kikosi cha Yanga kiliundwa na wachezaji 14 siku hiyo wakiwamo watatu walioingia kipindi cha pili, bado wapo ambao kile walichokifanya kwa muda waliokuwapo […]

HAZARD, COUTINHO WAWINDWA HISPANIA

KLABU kongwe la La Liga, Real Madrid na Barcelona wanajiandaa kwa ajili ya kuwanasa nyota wawili kutoka Ligi Kuu England, Eden Hazard na Philippe Coutinho. Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari nchini Hispania, Real Madrid wanamtaka Hazard kutoka Chelsea, wakati Barca wanamfukuzia Coutinho wa Liverpool, huku klabu hiyo ya Nou Camp wakidaiwa kumtumia mchezaji mwenzake wa Brazil, Neymar ili […]

UNAKUMBUKA: Dua alikata kilimilimi cha Yanga 1993

KATIKA safu ya unakumbuka wiki hii tunajikumbusha tukio moja lililofanywa na mshambuliaji mahiri wa zamani wa Simba, Dua Said la kukata kilimilimi cha Yanga baada ya kuifungia timu yake bao 1-0. Dua baada ya kufunga bao hilo ilikuwa ni kulipiza kisasi cha timu yake kufungwa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza. Mechi hiyo ambayo ilikuwa ni kali na ya kusisimua […]