Category: Latest News

Pochettino presha tupu Kane kuibeba Spurs UEFA

LONDON, England KOCHA wa  Tottenham, Mauricio Pochettino, amekiri kwamba, ana wasiwasi kama atamwanzisha staa wake,  Harry Kane, katika mechi ya fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, atawasaidia kuifunga Liverpool. Nahodha huyo wa timu ya Taifa ya England, hajawahi kupangwa kwenye kikosi hicho cha Spurs tangu alipopata majeraha ya enka wakati wa mechi ya kwanza ya robo fainali ya […]

MKALI WA MABAO YA ADHABU HUYOO YANGA

NA ZAINAB IDDY MKALI wa mabao ya mipira ya adhabu aliyewatesa makipa kadhaa Ligi Kuu Tanzania Bara, Haruna Shamte, yupo mbioni kutua Yanga akitokea Lipuli FC ya Iringa, huku vifaa zaidi vikizidi kumiminika Jangwani. Miongoni mwa makipa ambao hawatamsahau Shamte msimu huu, yupo kipa wa Yanga, Klaus Kindoki ambaye alitunguliwa na beki huyo katika moja ya mechi za timu zao […]

Ubingwa wa Simba umetoka kwa Adel Zrane

UNA AYOUB HINJO PONGEZI kwa kikosi cha Simba kufanikiwa kutetea taji la Ligi Kuu Tanzania Bara, ilikuwa safari ndefu kwao, hasa mwezi mmoja huu baada ya kucheza michezo zaidi ya 10, wala si kazi rahisi. Ni rahisi kuona kila kinachoendelea katika kikosi cha Simba wanapokuwa uwanjani, wanacheza soka safi, wachezaji wazuri na wenye uwezo wanaunda timu hiyo huku wakiongozwa na […]

Abramovich ateketeza mabilioni kuwatimua makocha

LONDON,England BILIONEA Roman Abramovich anaripotiwa kupoteza zaidi ya pauni milioni 92.9 sawa na zaidi ya Shilingi bilioni  270.2 za Kitanzania  kwa kuwalipa makocha aliowafukuza tangu aanze kuimiliki klabu ya  Chelsea mwaka  2003. Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, tangu kibopa huyo ainunue  Blues, kutoka  kwa aliyekuwa mmiliki wake, Ken Bates, tayari makocha  11 wameshakuja na kuondoka chini ya utawala […]

Amri Said aiwaza mechi ya Simba

NA WINFRIDA MTOI KOCHA Mkuu wa Biashara United, Amri Said, anapiga hesabu kali ili waweze kuvuna pointi tatu dhidi ya wapinzani wao Simba na kujinasua katika janga la kushuka daraja msimu huu. Kikosi cha Biashara United kinachoshika nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kikiwa na pointi 43, kinatarajia kukutana na Simba kesho kwenye Uwanja wa Uhuru, […]

Simba yaishangaza Sevilla

NA TIMA SIKILO  MABINGWA wa Ligi Kuu Bara, Simba, walionyesha kandanda safi katika mchezo wa jana usiku uliotambulika kama La Liga World SportPesa Challenge dhidi ya Sevilla kutoka Hispania licha ya kufungwa mabao 5-4 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.  Mchezo huo maalumu wa kimataifa wa kirafiki chini ya udhamini wa kampuni ya michezo ya kubahatisha, SportPesa, ilionyeshwa […]

Naiona Sevilla ikimfaidisha Dk. Kigwangalla kuliko TFF, Simba, Yanga

NA HASSAN DAUDI  HATIMAYE Sevilla iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu iliwasili mapema wiki hii. Nawazungumzia mabingwa mara tano wa taji la Ligi ya Europa, michuano ambayo kwa msimu huu ni Arsenal na Chelsea ndizo zitakazokwaana fainali Mei 29, mwaka huu. Sidhani kama muda na nafasi hii inatosha kukumbushia kilichowaleta wazungu hao nchini, nikiamini inatosha kusema jana walikuwa jijini Dar es […]

Kutinyu njia nyeupee Yanga

NA WINFRIDA MTOI KIUNGO wa Azam FC, raia wa Zimbabwe, Tafadzwa Kutinyu, ameonyeshwa njia ya kutokea baada ya uongozi wa klabu hiyo kuweka wazi kutomwongezea mkataba, hivyo kuwa huru kwenda kokote, ikiwamo Yanga wanaodaiwa kumtaka. Kutinyu, aliyesajiliwa na Azam FC msimu huu akitokea Singida United, anamaliza mkataba wake Mei 30, mwaka huu na tayari ameshatimkia nchini kwao Zimbabwe. Akizungumza na […]

Shindano la keki lawavutia Shilole, Esha Buheti

NA KYALAA SEHEYE WAREMBO wanaofanya vizuri kwenye muziki na filamu ambao pia ni wajasiriamali wa chakula, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na Esha Buheti, wamevutiwa na shindano la keki linaloandaliwa na Zena Sharif ‘Anazelitta’. Wawili hao, wamesema kwa kuwa nao ni wajasiriamali basi haina ubaya kuiga mazuri yanayofanywa na mjasiriamali mwenzao ili kuzidi kuinua wengine na wao pia kujitangaza. “Mimi huwa sijali […]