Category: Kolamu

Usimsubirie mwenzako, anza kufanya hivi ili ufurahie mahusiano yako

ASILIMIA 70 ya furaha katika uhusiano wako inakutegemea wewe na asilimia 30 inamtegemea mwenzako. Ila bahati mbaya sana watu wengi katika uhusiano hutafuta furaha zao kupitia wenzao, wakisahau wao ndio hasa chimbuko la kusababisha furaha katika uhusiano wao. Iko hivi. Ndani ya mahusiano furaha huibuka kutokana na matendo yako kwa mwenzako. Kutokana na matendo yako mazuri mwenzako hupata uchangamfu, amani […]

Kuna Jjuuko Simba, Jjuuko Uganda

NA EZEKIEL TENDWA BAADA ya timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’, kukubali kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Taifa Stars, mjadala mkubwa umeibuka kwa mashabiki wakiuliza ni kwanini kocha hakumpanga Jjuuko Murshid. Mitandao ya kijamii ilikuwa ikielezea namna Jjuuko alivyowekwa benchi wakiamini kwamba angekuwepo wakina Simon Msuva wasingeweza kuipenya ngome yao na kufungwa mabao hayo. Licha ya Uganda kufuzu […]

KWA HALI ILIVYO HUU MJEZI WA AJIB INABIDI UFULIWE NA MAJI YA ULAYA

DOMO LA MFUA JEZI BASI iko hivi kama mlikuwa hamjui acha niwaambie, Shirikisho la Soka kule nchini Lesoto, wameanza kuhaha na kutafuta namna ya kumdhibiti Ibrahim Ajib, maana wameshapata taarifa kwamba atakuwepo kwenye kikosi cha Stars teh teh……. Ajib amekuwa moto wa kuotea mbali kwa sasa katika Ligi Kuu Bara, huku akifunga mibao ya ajabu kwenye mechi za hivi karibuni […]

TUNALITUMBUKIZA SOKA LETU SHIMONI TUKIWA TUNAONA

NA EZEKIEL TENDWA AGOSTI 29 mwaka huu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini, Wilfred Kidau, alijitokeza mbele ya Watanzania akitangaza maamuzi ya Emmanuel Amunike, kuwapiga pini wachezaji sita wa Simba kati ya saba, kwenye kikosi cha Stars. Wachezaji hao wa Simba, walipigwa ‘stop’ kutokana na kuchelewa kuripoti kambini kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na kocha, Amunike, ambaye ndiye mwenye […]

RONALDO AMVUNJA PUA MLINDA MLANGO CHIEVO

ROMA,Italia STRAIKA Cristiano Ronaldo, ameanza na balaa katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu ya Italia, Serie A, baada ya kumvunja  pua  mlinda mlango wa timu ya Chievo, Stefano Sorrentino walipogongana katika harakati za kuwania mpira. Tukio hilo limetokea juzi, katika Uwanja wa Marc’Antonio Bentegodi , baada ya mlinda mlango huyo kutoka nje ya eneo la hatari ili kuwahi […]

MIAKA MINNE? LIONEL MESSI ANA NINI KIPYA?

LIONEL Messi, mchezaji bora duniani, amekubali kutoliacha kasri lake la kifalme la Nou Camp baada ya kukubali kusaini mkataba mpya wa kubaki Barcelona hadi mwaka 2021. Siku chache baada ya kusherehekea miaka yake 30 ya kuzaliwa, mchawi wa soka ameibariki ndoa yake na Barca. Ameahidi kuwa nao katika shida na raha nyingine. Umri aliofikia Messi ndio ule ambao mastaa wengi […]

ULITAKA LUKAKU AFANYE NINI ZAIDI?

NA OSCAR OSCAR ASIKWAMBIE mtu kitu, Manchester United si klabu ya kawaida nchini England na hata barani Ulaya. Huwezi kutaja klabu za soka tajiri duniani ukaiacha Manchester United. Huwezi kutaja klabu zenye mashabiki wengi duniani ukaiacha Manchester United. Hii ni aina ya klabu ambayo wachezaji wengi duniani hutaka kutimiza ndoto zao kwa kucheza hapo. Endapo utakuwa umesahau, Manchester United ndiyo […]

JKT RUVU IMEFUNGA HESABU ZA KUSHUKA DARAJA

NA ONESMO KAPINGA LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara imebaki katika ushindani wa timu zitakazochukua ubingwa na zile zitakazoshuka daraja msimu huu. Ni timu mbili za Simba na Yanga ndizo zenye nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa wa msimu huu, zinazoshika nafasi za juu katika msimamo wa ligi hiyo. Simba ndio wanaoongoza katika msimamo huo kutokana na pointi 62  baada ya […]

UDAMBWIDAMBWI WA MARCELO

Na MARKUS MPANGALA JINA lake ni Marcelo Vieira da Silva Junior. Tamka Machelo. Anavaa jezi namba 12 mgongoni. Ni Mbrazil aliyerithi beki tatu kutoka kwa Roberto Carlos. Kabla ya Zinedine Zidane kubadilisha mbinu za kumtumia Cristiano Ronaldo kutoka winga ya kushoto au kulia hadi mshambuliaji wa kati, kuna jambo moja ambalo linatokea kila siku. Kama Ronaldo akipangwa winga ya kushoto […]