Category: Hadithi

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU [63]

Ilipoishia jana RAMONA Ndege ya shirika la Qatar Airways ilikuwa inatua Uwanja wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere, jijini Dar es Salaam nchini Tanzania. Ramona alishuka akiwa pamoja na walinzi wake watano. Alikuwa na moyo ule ule moyo wa ajabu uliotaka kwenda kumwambia mama yake na Roika juu ya kilichompata mwanaye na kumwomba msamaha. SASA ENDELEA Ramona hakujali kuwa mama […]

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Ilipoishia jana JIJINI CAIRO Roika alikuwa amekwisha shuka jijini Cairo nchini Misri, akiwa anatokea Tanzania, alikokwenda kumuomba mama yake damu, damu itakayomuinua tena Shazayi binti wa Rais asipatwe na umauti. SASA ENDELEA Sasa alikuwa anakata tiketi ya ndege ya kuelekea nchini Pakistan. Hiyo ikiwa ni siku ya pili na masaa kadhaa, tokea alipoondoka Pakistan na kuelekea Tanzania na baadae kufika […]

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Ilipoishia Jumanne Ramona hakuwa na uwezo tena wa kuendelea kuongea na kiongozi huyo, aliingia kwenye chumba kimojawapo na kujifungia. Huko alilia kama mtu aliyefiwa na wazazi wote wawili kwa wakati mmoja. Alihisi dunia yote ameibeba yeye. SASA ENDELEA Kwani kuchomwa moto kwa mwili wa Roika kulimaanisha kuwa, Roika alikufa kifo kibaya sana. Yaani hakutambulika wala kuheshimiwa kama ni binadamu. “Roika […]

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Ilipoishia jana Aliwasha gari kuelekea kaskazini mwa jiji la Dar es Salaam, kunako uwanja wa ndege, Uwanja wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere. SASA ENDELEA Kwa kutumia njia za vichochoroni ili kuepuka foleni, Roika alifika uwanjani ikiwa ni  baada ya dakika 25. Haraka alikataa tiketi ya kuelekea Cairo nchini Misri. Na baada ya dakika 15 ndege ya Qatar Airways ilikuwa […]

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Ilipoishia Jumamosi “MAMA tuachane na habari hizo za Ramona na Biyanah. Sasa  naomba unitazame mwanao kupitia kioo cha Shazayi. Mwanamke ambaye naamini Mungu ameniletea kutoka katika hazina yake ya mbinguni.” SASA ENDELEA “Roika mwanangu, upo katika hatari kubwa, endapo wazazi wake watajua kuwa binti yao amehatarisha maisha yake kwa sababu yako, lazima wakufunge au kukuua kabisa.” “Mama achana kwanza na […]

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Ilipoishia jana MACHO yalimtoka baada ya kumuona mwanawe akiwa amesimama mlangoni. Akiwa analia sana. SASA ENDELEA… Mama Roika hakushtuka kumuona mwanaye akiwa nyumbani kwao, maana pale ni sehemu alipokulia na kulelewa. Kilichomshtua ni kuona mwanaye akilia. Akitokwa na machozi mengi sana. Alianza kuogopa. Akauweka mwiko chini na kuzima jiko la umeme, huku akimtazama mwanaye kwa majonzi makubwa. Wakati akipiga hatua […]

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Ilipoishia jana “Tafadhali nisaidie kuokoa maisha ya mwanamke mwenzio,” aliongea Roika kwa machozi mengi. Hakuwahi kulia ila siku hiyo alilia. SASA ENDELEA Maneno ya Roika yalimuingia yule muuguzi, huruma ilimjaa, akamtazama Roika kwa dakika moja ya ukimya na kisha akamuuliza: “Sawa, lakini nitakusaidiaje ilhali una pingu kitandani?” “Tafuta waya mwembamba uliopinda mbele.” Haraka muuguzi alielekea kwenye vyombo vya tiba na […]

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Ilipoishia jana Hakika Roika alizidi kuchanganyikiwa, kwani tayari yeye alishakuwa na nguvu, lakini Shazayi hakuwa na nguvu na ilionekana kuwa muda si mrefu hali ya huzuni itakwenda kutokea. Taratibu huku machozi yakimtoka, Roika aliusogeza mdomo wake karibu kabisa na mdomo wa Shazayi, akambusu. Shazayi alitabasamu na kisha akasema.  “Thank you Roika.” (asante Roika). Aliposema hivyo, alifumba macho. SASA ENDELEA Roika […]

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU [52]

Ilipoishia Jana “Mimi ndio nimeamua kufa au kupona, lolote litakalokuwa, nataka Roika apone sawa, haya ingiza sindano kwenye mishipa au unataka nijitoe mwenyewe.” SASA ENDELEA “Madam namuogopa sana baba yako. Hivi akijua kuwa nimetekeleza zoezi la kukutoa damu unafikiri itakuwaje? Nitakuwa sina kazi mimi na huenda nitanyongwa. Nina familia ya watoto wanne na ndugu sita, wote wananitegemea. TafadhaLi muache Roika […]

LWANDAMINA AONYESHA VITU ADIMU YANGA

NA HUSSEIN OMAR KOCHA wa Yanga, George Lwandamina, ameendelea kuonyesha vitu adimu kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika jana jioni kwenye Uwanja wa Gymkhana uliopo Posta jijini Dar es Salaam. Katika mazoezi hayo, Lwandamina alionyesha kuwa si mtu wa mchezo mchezo kutokana na kutoa vitu vya kipekee kwa nyota wa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. […]