Category: Hadithi

MSUVA ATHIBITISHA KUPATA OFA KIBAO ULAYA 

NA WINFRIDA MTOI WINGA wa zamani wa Yanga anayekipiga katika timu ya Difaa El Jadida ya nchini Morocco, Simon Msuva, ameweka wazi kuwa safari yake ya kwenda kucheza soka la kulipwa Ulaya imekaribia kutokana na ofa anazozidi kupata. Kwa muda mrefu Msuva alikuwa akihusishwa na timu mbalimbali za Ulaya ikiwamo za nchini Hispania kutokana na kiwango anachokionyesha katika timu yake […]

ZAHERA ACHIMBA MKWARA YANGA

NA TIMA SIKILO KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera, amewachimba mkwara mzito nyota wake akisema kwamba, kitendo cha mchezaji kutofanya kazi yake ipasavyo akiwa uwanjani na kumbebesha majukumu kipa, kitawafanya wengi wa kikosi cha kwanza kusugua benchi. Kauli hiyo ameitoa kutokana na baadhi ya wachezaji kushindwa kufanya kile wanachotakiwa, badala yake kumbebesha mzigo kipa ambaye naye ana kazi kubwa langoni. Akizungumza […]

TAJIRI WA MASIKINI (14)

NA EMAN FISIMA      |         Ilipoishia Rumia alizidi kuona tofauti yangu na unyonge wangu, naye alianza kuingiwa na wasiwasi.  Siku ya pili alishangaa kuona sijaenda shambani kama ilivyo kawaida ya siku zote. Kawaida ilikuwa nikipumzika Jumapili tu lakini siku hiyo ilikuwa Jumatano.  Aliponiuliza nilimwambia kuwa napumzika kwa sababu nilikuwa nimefanya sana kazi pindi nilipokuwa jijini Port […]

TAJIRI WA MASIKINI – 10

NA EMAN FISIMA   Ilipoishia Watu wengi walikuwa wakiendelea kuteseka na kuishi maisha ya shida kama vile walikuwa wakimbizi, maana wao hawakuweza kuuza mazao yao jijini Port Villa na kwingineko. Wengine hawakuweza kufanya kilimo rahisi kwa sababu hawakuwa na pampu za maji, hivyo waliishi kwa kilimo kidogo kisicho na hata tija ndogo. Watoto walikufa sana kwa ugonjwa wa utapiamlo, malaria […]

TAJIRI WA MASIKINI – 5

Na Eman Fisima, +255 654 076 265   Ilipoishia Maana ni kweli sura yangu ilikuwa imejawa na huzuni na mashaka makubwa kutokana na kukutana na mpenzi wake wa zamani aliyeniambia maneno yenye ukweli fulani. Nilishindwa kumjibu, alifunikia samaki kwenye sufuria akiiacha inachemka na kuja pale nilipokaa. Alikaa juu ya mkono wa kochi, kochi nililokalia mimi akanishika shavu na kuniuliza tena. […]

WACHEZAJI MBAO FC WANYANG’ANYWA SIMU

NA DAMIAN MASYENENE, MWANZA KIPIGO cha mabao 3-2 walichokipata Mbao FC dhidi ya Simba Aprili 10, mwaka jana katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kinaonekana bado kinawanyima usingizi viongozi wa klabu hiyo hasa kutokana na mchezo wao wa leo. Katika mchezo huo, Mbao waliokuwa wenyeji walikuwa wanaongoza kwa mabao 2-0 hadi dakika ya 82 yaliyofungwa na Evarigestus Mujwahuki na […]

ZAHERA KUTUMIA MIKANDA YA VIDEO KUIUA MTIBWA

NA WINFRIDA MTOI KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga, Mwinyi Zahera, amesema anatarajia kukaa na wachezaji wake leo kuangalia video za mchezo wao wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger ili waone makosa waliyofanya kabla ya kuvaana na Mtibwa Sugar. Juzi Yanga walicharuka na kutamba nyumbani baada ya kuwafunga waarabu hao kutoka nchini Algeria […]

TONTO DIKEH AKANA ‘KUBANJUA’ AMRI YA SITA NA MCHUNGAJI

LAGOS, Nigeria BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu kujibu shutuma zinazomkabili  kuhusu kuingia katika uhusiano wa kimapenzi na mchungaji, staa  mahiri katika tasnia ya filamu nchini Nigeria,  Tonto Dikeh, ameibuka na kukanusha madai hayo akisema ukimya wake alikuwa akitafuta  jinsi ya kijisafisha. Hivi karibuni kimwana huyo alishutumiwa na vyombo vya habari na watu mbalimbali wakidai kuwa staa huyo ameingilia […]

TABIA HIZI ZINAPUNGUZA HISIA ZA UPENDO KWA MWENZAKO

RAMADHANI MASENGA UNAISHI vipi na mwenzako? Namna unavyoishi naye kuna mchango mkubwa sana ima wa kuongeza ama kupunguza kiwango chake cha upendo kwako. Kama ambavyo nimewahi kusema, kitendo cha kupendwa si kazi sana ila kazi nzito ni kufanya anayekupenda leo aendelee kukupenda kila siku. Hapa ndipo kwenye mtihani na vijana wengi wameshindwa. Tathmini inaonesha wengi huingia katika uhusiano wakiwa wanapendana […]