Category: Hadithi

BUSHIR AFUATA NJIA ZA OMOG

NA MAREGES NYAMAKA KOCHA mkuu mpya wa Mwadui, Ally Bushir, amekula sahani moja na kocha wa Simba, Joseph Omog, baada ya kushinda mechi tatu mfululizo za mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Bushir aliyeanza kuifundisha timu hiyo mzunguko wa pili baada ya kocha mkuu aliyemtangulia Jamhuri Kihwelu ‘Julio’,  kuachia ngazi, ameonekana kuanza vizuri baada ya kuiwezesha kupata pointi […]

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Ilipoishia Jumamosi ALIAMUA kuingia chumba cha silaha na kuchukua bastola aina ya Short Vizic. Akapandisha gauni lake na kuichomeka kwenye paja lake la kulia. Alimini kuwa akikutana na Biyanah lazima kuwe na vita. SASA ENDELEA… Ramona hakuwa na mtu mwingine wa kumfikiria zaidi ya Biyanah. Akili yake yote ilishakuwa imemchunguza Biyanah vya kutosha. Majibu aliyokuwa nayo ni kwamba, Biyanah alikuwa […]

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Ilipoishia jana Akiwa anapanda ngazi mpiganaji mmoja wa kikundi cha Swaba alimwita na kumwomba waongee. Mpiganaji huyo ndiye yule aliyekuwa ametumwa akauchome moto mwili wa Roika. SASA ENDELEA Siku ile baada ya Ramona kumpiga risasi Roika, kiongozi wa kikundi cha Swaba, Zahil Bin Shaq, alikuwa amemwagiza mpiganaji wake aende akauchome moto mwili wa Roika. Lakini hakufanikiwa kwa sababu mwili wa […]

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU [72]

Ilipoishia jana Ramona aliposikia hivyo, alianza kulia tena, maana maneno hayo yalizidi kumuumiza yeye kama muuaji wa mmoja wa familia ile.”  “Usilie mwanangu, tayari tumekwisha sameheana. Ninachotaka tu binti yangu asijue lililompata kaka yake.”  “Mama najiona ni mwenye dhambi. Naumia pindi napowatazama wewe na huyu mwanao. Kwa kuwa mimi ni chanzo cha nyie kuishi bila Roika,” aliongea Ramona. SASA ENDELEA […]

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Ilipoishia Jumanne MOYO wake ulimdunda zaidi ya ngoma, mwili wake ulitetemeka. Taratibu alianza kuusogeza uso wake kuelekea kwa Shazayi. Hakika ilikuwa ni siku ya muujiza. Shazayi alikuwa anamtazama Roika kwa tabasamu zuri ajabu. Macho yake mazuri mithili ya malaika mtoto, yalikuwa yakitokwa na machozi. Hakika Shazayi aliionekana ni mwanamke mzuri kama mtu aliyetokwa kuzaliwa upya. SASA ENDELEA Licha ya uchomvu […]

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Ilipoishia jana PAKISTANI BIYANAH mwanamke bilionea alikuwa kwenye wakati mgumu usiolezeka. Maisha yake yalianza kumtofautisha yeye na utajiri aliokuwa nao. Kwani alikuwa analia kila siku. Hakujua hadi muda huo Roika alikuwa amekwenda wapi. Aliamua kuongea na uongozi wa hoteli ya Alashak  ambapo walikaa na kuulizana kuhusu mahali alipo kijana huyo. SASA ENDELEA Biyanah aliutaka uongozi wa hoteli utoe taarifa polisi […]

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU [69]

Ilipoishia Jumamosi “MAMA nisamehe, mama sikufiria kufanya hivyo, najutia dhambi yangu,” aliongea Ramona huku akiwa ameishika miguu ya mama Roika, akilia kupita kiasi.” Kilio kikubwa kilikuwa kimetawala mle ndani, kila mmoja aliendelea kulia. Lakini kilio cha mama Roika kilikuwa ni kilio cha kuigiza kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa  akifahamu kuwa mwanaye yuko wapi na anafanya nini kwa muda huo. Lakini […]

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Ilipoishia jana MACHO yalimtoka mama Roika pindi alipomuona mrembo wa dunia Ramona Fika pale sebuleni. Upesi kichwa chake kilifikiria kwa haraka mambo mengi aliyosimuliwa na mwanaye, kuhusu mrembo huyo na kilichompata Pakistani. Alijiuliza ni nini kilikuwa kimemleta pale nyumbani kwao. Alianza kujawa na woga kwa sababu alimfahamu Ramona kuwa ni mtu hatari. Macho ya Ramona yalimtazama mama Roika kwa woga […]

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Ilipoishia jana Kikundi cha kigaidi cha Swaba kilitoa mkanda wa video, kikisema kuwa kinamshikilia mtoto wa Rais, Shazayi binti Galim. Jambo ambalo lilikuwa si la kweli. Mkanda huo ulisema uongo mtupu. Swaba waliamua kutoa uzushi huo kwa maslahi yao binafsi, ikiwamo kuitishia Serikali ya Rais Galim na kuitaka itoe kiasi kikubwa cha pesa na kukipa eneo la Ramadan Kash, lenye […]

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Ilipoishia Jumanne Kwa furaha kubwa na machozi, Roika alimkumbatia Dk. Sufian, akaelekea kitandani alikolala Shazayi akamshika kichwani na kumbusu. Alijawa na furaha isiyoelezeka kwa urahisi. SASA ENDELEA FURAHA ilikuwa kubwa ndani ya Hospitali ya Mohamed Words, si Roika tu aliyefurahia kupona kwa Shazayi, bali hata Dk. Sufian na wafanyakazi wake wote wa hospitali hiyo walizipokea taarifa hizo kama muujiza kwao. […]