Category: Habari

Wozniacki aibuka mbabe Pan Pacific Open

TOKYO, Japan MKALI wa tenisi aliyewahi kuongoza kwa viwango vya dunia, Caroline Wozniacki, aliibuka mbabe kwenye mashindano ya wazi ya tenisi ya Pan Pacific dhidi ya mwenyeji wake, Naomi Osaka, ukiwa ni ubingwa wake wa kwanza tangu Februari 2015. Wozniacki raia wa Denmark, ambaye amekumbwa na mfululizo wa majeraha mwaka huu, alianza kwa kasi mno kwenye pambano hilo dhidi ya […]

Malale alia ukame wa mabao JKT Ruvu

NA ESTHER GEORGE KOCHA Mkuu wa JKT Ruvu, Malale Hamsini, amelia na ukame wa mabao kutokana na washambuliaji wake kupoteza nafasi za kufunga Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. JKT Ruvu waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City katika mechi iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, lakini Malale amesema walikosa mabao mengi. Malale alisema amegundua […]

Tamasha la Bagamoyo kuanza leo

NA STELLA KANYARI, TUDARCO TAMASHA la kimataifa la Sanaa na Utamaduni la Bagamoyo, linaanza leo mjini Bagamoyo huku Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, akitarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa tamasha hilo. Tamasha hilo kongwe la sanaa za maonyesho katika ukanda wa Afrika Mashariki hufanyika kila mwaka na litafanyika kwenye viwanja vya Taasisi ya Sanaa na […]

Kichuya: Mtanielewa Oktoba mosi

NA ZAINAB IDDY MSHAMBULIAJI wa pembeni wa Simba, Shiza Kichuya, amesema mashabiki wa Yanga watamwelewa Oktoba mosi mwaka huu, baada ya dakika 90 ya mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara  itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Akizungumza na BINGWA jana, Kichuya alisema hana shaka kabisa kuelekea mechi hiyo, kwani lazima kitaeleweka ndani ya dakika hizo. […]

Wabunge Yanga walipa 5 za timu yao kwa Simba

NA ZAITUNI KIBWANA TIMU ya wabunge wa Yanga,  imeibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Simba, katika mchezo wa kirafiki wa kuchangia maafa ya tetemeko la ardhi  mkoani Kagera uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Mabao ya wabunge hao wa Yanga yalifungwa na Jadif Hamisi, Mohammed Machengerwa, aliyefunga mawili na Mwigulu Nchemba aliyefunga mawili. Kwa […]

Kamusoko, Mkude vita ya mafundi Oktoba mosi

NA ZAITUNI KIBWANA HAKUNA asiyejua kuwa kiungo wa Yanga, Thaban Kamusoko, alisajiliwa kwa hela ndefu tu pale Jangwani akitokea FC Platinum ambapo kuelekea ‘derby’ ya Simba na Yanga, atakuwa na kibarua kizito cha kupambana na  Johas Mkude ambaye alisajiliwa kwa dau la milioni 60 pale Msimbazi. Viungo hawa wote ni mafundi na wanaweza kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani. Wakicheza […]

Njooni Taifa Tuwanyooshe

NA ZAITUNI KIBWANA USHINDI wa mabao 4-0 walioupata Simba kwenye mchezo wao juzi dhidi ya Majimaji, umewapa kiburi timu hiyo na kuamua kuwaita mashabiki wa Yanga kwenda kwa wingi Uwanja wa Taifa Oktoba mosi, timu hizo zitakapokutana. Wito huo umetolewa na Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Manyanja, ambaye aliwataka mashabiki hao wa Yanga kuhudhuria kwa wingi mpambano huo. Akizungumzia maandalizi […]

Yanga yapatwa Shinyanga

REBECCA LUZUNYA SHINYANGA YANGA jana ilipatwa mjini hapa baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wenyeji Stand United na kuzima ndoto za kuondoka na pointi sita mkoani hapa. Bao pekee lililofungwa na Pastory Athanas, lilitosha kuipa ushindi  Stand United  ambayo sasa imekwea hadi nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya Soka ya Vodacom Tanzania. Mechi  hiyo […]

Dangote Bilionea anayenyimwa kutuliza kiu ya kuinunua Arsenal

LONDON, England MFANYABIASHARA maarufu nchini Nigeria, Aliko Dangote, anatajwa kuwa mbioni kuinunua klabu ya Arsenal. Dangote anataka kuhakikisha Arsenal inakuwa yake katika kipindi kisichozidi miaka minne kwa sasa. Kwa mara ya kwanza, taarifa za tajiri huyo kuitaka Arsenal zilianza kuvuma mwaka uliopita, lakini sasa ameonekana kuwa ‘siriazi’ kidogo. Imeripotiwa kuwa Dangote ameufufua mpango huo baada ya Arsenal kuisambaratisha Hull City […]