Category: Habari

Wazee wa Yanga Sc wapinga kukodishwa kwa klabu yao

KATIBU mkuu wa Baraza la Wazee wa klabu ya Yanga, Ibrahim Akilimali pamoja na wenzake, wamepinga suala la klabu yao kuingia makubaliano na Kampuni ya Yanga yetu kwa ajili ya kukodisha klabu hiyo kwa miaka 10. Wakizungumza na waandishi wa Habari jana kwenye Ukumbi wa Habari Maelezo, Akilimali alisema, mkataba huyo uliosainiwa na lilalotajwa kuwa ni baraza la wadhamini ni […]

Jjuuko atajwa Yanga, Niyonzima Simba

NA EZEKIEL TENDWA KUNA kila dalili za kumwona beki wa kati wa Simba, Jjuuko Murushid, akikipiga Yanga msimu ujao na kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, akivaa uzi mwekundu. Taarifa ambazo BINGWA linazo zinadai kuwa Simba wapo kwenye mawindo makubwa kuitaka saini ya Niyonzima ambaye inadaiwa amechoshwa na kusugulishwa benchi. Wakati Simba wakiwa bize na kumfuatilia Niyonzima, taarifa nyingine zinadai kuwa Yanga […]

Akilimali mkutanoni Jumapili kama kawa

NA HUSSEIN OMAR KATIBU wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahimu Akilimali, amesisitiza atahudhuria Mkutano Mkuu wa dharura wa wanachama wa klabu hiyo ambao umepangwa kufanyika Oktoba 23 mwaka huu. Tayari uongozi wa klabu hiyo umeweka hadharani ajenda 14 za mkutano utakaofanyika Jumapili katika ukumbi wa klabu hiyo. Akilimali atashiriki mkutano huo akiwa na hoja nyingi za msingi zitakazohusu ukodishwaji […]

Soma hii umchukie zaidi Shiza Kichuya

NA WINFRIDA MTOI WALE wanaomchukia winga machachari wa Simba, Shiza Kichuya, bila shaka watazidi kuumia zaidi kutokana na mchezaji huyo kutinga katika rekodi ya aina yake akiwa analingana mabao na vinara wa kucheka na nyavu wa ligi za Ulaya. Ukiangalia orodha ya wafungaji mabao katika ligi maarufu duniani kama England, Ujerumani, Italia, Hispania na Ufaransa, wanaoongoza kwa kucheka na nyavu […]

Siri nzito yafichuka Pluijm vs Niyonzima

NA MWANDISHI WETU WAKATI mashabiki wa Yanga wakitofautiana juu ya kitendo cha mchezaji wao kipenzi, Haruna Niyonzima, kutopangwa au kuingizwa dakika za mwisho katika mechi za hivi karibuni, BINGWA limebaini kinachoendelea kati yake na kocha mkuu wa timu hiyo, Hans van der Pluijm. Kiungo huyo wa kutumainiwa wa Yanga na timu ya Taifa ya Rwanda, mwishoni mwa mwaka jana aliingia […]

Yanga yaonyesha dharau ya karne

NA HUSSEIN OMAR JAPO wapo mashabiki wa soka nchini wanaoamini Yanga haina nafasi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kutokana na mwenendo wao katika ligi hiyo, mabingwa hao watetezi wa kipute hicho, wameonyesha jeuri ya aina yake kwa kudai kuwa wanajua wanalolifanya, huku wakitoa angalizo kwa wanaowabeza kusubiri Mei mwakani kujua kwanini Wanajangwani hao wanajiita […]

KWA MECHI ILE YA AZAM, YANGA…….SIMBA HAINA MPINZANI 2016

HUSSEIN OMAR NA EZEKIEL TENDWA UKIAMUA kusema Simba mabingwa wa msimu wa 2016/17, bila shaka utakuwa hujakosea sana hasa iwapo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga pamoja na Azam FC wataendelea kuonyesha kiwango duni kama ilivyokuwa katika mchezo baina yao mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Dalili za ubingwa kuelekea kwa Wekundu wa […]

Mayanja akenua meno 32 Simba

NA SALMA MPELI, KOCHA Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, amechekelea kuongoza katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuwaacha mbali watani wao wa jadi, Yanga. Simba wanaongoza katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi 23, wakifuatiwa na  Stand United ambao wana pointi 20, huku Majimaji wakiendelea kuburuza mkia kwa pointi tatu. Akizungumza na BINGWA jana, […]