Category: Habari

TSAA: Mshiriki mashindano ya Mashua

NA WINFRIDA NGONYANI CHAMA cha Mashua Tanzania (TSAA), kimewataka Watanzania kujitokeza kushiriki mchezo huo ambao kwa kiasi kikubwa umetawaliwa na wageni. Wito huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa TSAA, Philemon Nassary, ambaye alisema mchezo huo umekosa umaarufu kwa kuwa umekuwa ukichezwa zaidi na watu kutoka nje ya nchi hususani Wazungu. “Watanzania wajitokeze kucheza ili utambulike na tuutumie katika kuiwakilisha nchi […]

Mkude: Dakika 90 zitaamua nani kidume

NA SALMA MPELI NAHODHA wa Simba, Jonas Mkude, amesema  hawezi kuizungumzia sana mechi yao dhidi ya Yanga, kwani anaamini  dakika 90 za mchezo huo ndizo zitakazoamua nani mshindi kwenye pambano hilo. Yanga na Simba zitashuka dimbani Oktoba mosi mwaka huu kuumana katika pambano litakalopigwa kwenye Uwanja wa Taifa. Akizungumza na BINGWA, Mkude alisema anaamini Yanga wanafanya maandalizi ya nguvu kwa […]

Siri ya kudorora kwa Azam yafichuka

ZAINAB IDDY NA SALMA MPELI BAADA ya Azam FC kupoteza michezo miwili mfululizo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, imedaiwa kuwa moja ya vitu vilivyosababisha kupoteza morali kwa wachezaji wao ni kukosa posho tangu kuanza kwa msimu huu. Tangu kuanza kwa ligi msimu huu, Azam imekuwa na mwendo wa kinyonga jambo ambalo limesababisha kujikuta wakipata matokeo yasiyoridhisha kwenye mechi zake. Katika […]

Ibra alitaka kumvunja mguu wakala wa Pogba

MACHESTER, England ZLATAN Ibrahimovic amefanikiwa kucheza pamoja na Paul Pogba kwenye klabu ya Manchester United, ikiwa ni baada ya mbinu zake za kumtishia kumvunja mguu wakala, Mino Raiola. Nyota huyo wa Sweden mwenye umri wa miaka 34, aliungana na Jose Mourinho, Julai 1 mwaka huu na kusubiri wiki kadhaa kupita hadi dili la Pogba kutoka Juventus kukamilika. Raiola ambaye ni […]

Kitendo cha Sakho chamtatiza Klopp

MERSEYSIDE, Liverpool MAPEMA wikiendi hii, beki wa Liverpool, Mamadou Sakho, alituma picha kwenye mtandao wa kijamii wa Snapchat zikiwa na maneno yanayoelezea namna anavyoshindwa kuelewa kwanini hatumiwi kwenye kikosi cha kocha, Jurgen Klopp, msimu huu, lakini kitendo hicho kimemtatiza kocha wake huyo. Beki huyo hajacheza tangu alipopata majeraha  April mwaka huu, na hatima yake kwenye kikosi cha Liverpool imeonekana kuwa […]

Jezi iliyovaliwa na Ozil yampagawisha shabiki mtoto wa Arsenal

LONDON, England KIUNGO mbunifu wa klabu ya Arsenal, Mesut Ozil, amemfanya shabiki mtoto wa timu hiyo kuwa na furaha isiyoelezeka, baada ya kumpa jezi yake aliyoivua mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Chelsea ambao ulimalizika kwa ‘The Gunners’ hao kuibuka na ushindi wa mabao 3-0. Ozil pamoja na wenzake walionesha kiwango cha hali ya […]

Bekele aonesha uwezo mbio ndefu za Berlin

BERLIN, Ujerumani MWANARIADHA mahiri kutoka Ethiopia, Kenenisa Bekele, alifanya kazi kubwa kuibuka mshindi kwenye mbio ndefu za Berlin mapema Jumapili ya wikiendi iliyopita ambapo alimpiku mpinzani wake mkubwa, Wilson Kipsang wa Kenya. Bekele ambaye ni bingwa wa Olimpiki mara tatu anayeshikilia rekodi ya kushinda kwenye mbio za mita 5,000 na 10,000, alikuwa na vita kubwa dhidi ya Kipsang, lakini alifanikiwa […]

Wozniacki aibuka mbabe Pan Pacific Open

TOKYO, Japan MKALI wa tenisi aliyewahi kuongoza kwa viwango vya dunia, Caroline Wozniacki, aliibuka mbabe kwenye mashindano ya wazi ya tenisi ya Pan Pacific dhidi ya mwenyeji wake, Naomi Osaka, ukiwa ni ubingwa wake wa kwanza tangu Februari 2015. Wozniacki raia wa Denmark, ambaye amekumbwa na mfululizo wa majeraha mwaka huu, alianza kwa kasi mno kwenye pambano hilo dhidi ya […]

Malale alia ukame wa mabao JKT Ruvu

NA ESTHER GEORGE KOCHA Mkuu wa JKT Ruvu, Malale Hamsini, amelia na ukame wa mabao kutokana na washambuliaji wake kupoteza nafasi za kufunga Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. JKT Ruvu waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City katika mechi iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, lakini Malale amesema walikosa mabao mengi. Malale alisema amegundua […]