Category: Habari

Tambwe aenda Oktoba mosi na siri nzito

NA HUSSEIN OMAR ZIKIWA zimebaki siku chache kabla ya Yanga kuivaa Simba, straika nyota wa timu hiyo Mrundi, Amissi Tambwe,  amesema amekiona kikosi cha Simba,  lakini ana siri nzito moyoni kuelekea katika pambano hilo litakalopigwa Oktoba mosi mwaka huu kwenye  Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Yanga kabla ya kukutana na watani wa jadi Simba watacheza na Stand United […]

Kipingu ajivunia kutoa sita Kilimanjaro Queens

HAPPYGLORY URASSA (DSJ) NA REGINA GEORGE (TUDARCO) MKURUGENZI wa Shule ya Sekondari ya Lord Baden Memorial, iliyopo wilayani Bagamoyo, Pwani, Kanali mstaafu Iddi Kipingu, amejivunia kuwa na wachezaji sita katika kikosi cha timu ya soka ya wanawake Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Queens’, kilichotwaa ubingwa wa Kombe la Chalenji, nchini Uganda mapema wiki hii. Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, […]

Wachezaji 20 kushiriki taekwondo Kenya

NA JACKLINE LAIZER, ARUSHA WACHEZAJI 20 wa Taekwondo wa Shule ya Sekondari ya Edmund Rice, iliyopo mkoani hapa, wanatarajiwa kushiriki michuano ya wazi itakayofanyika kesho jijini Nairobi, nchini Kenya. Michuano hiyo inayojulikana kama ‘Loreto Valley Road Tekwondo Championship and National Cadet & Team Build up’, itashirikisha wachezaji waliochini ya umri wa miaka 13-18. Akizungumza mkoani hapa jana, Mkurugenzi wa Ufundi […]

Majembe mawili Simba kuikosa Majimaji

NA MARTIN MAZUGWA SIMBA wanatarajia kuwakosa wachezaji wawili tegemeo, kiungo  Mwinyi Kazimoto na beki wa kati, Method Mwanjale, katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Majimaji, itakayochezwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Mwanjale alipata mchubuko wa nyama katika paja kwenye mechi iliyopita dhidi ya Azam, iliyochezwa Uwanja wa Uhuru na wao kushinda […]

Beki Yanga awataka Ajib, Mavugo Okt. mosi

NA HUSSEIN OMAR BEKI wa Yanga, Pato Ngonyani,  amewaangalia washambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajib na Laudit Mavugo na kujiridhisha ataweza kuwazuia katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itakayochezwa Oktoba mosi, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Ngonyani, ambaye  hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza cha kocha mkuu wa […]

Winga machachari Simba  amtibua nyongo Omog

NA ONESMO KAPINGA WAKATI  joto la pambano la watani wa jadi, Simba na Yanga likizidi kupanda, winga machachari wa Simba, Jamal Mnyate, ametibua nyongo ya kocha mkuu wa timu hiyo, Joseph Omog, kutokana na kushindwa kuelewa maelekezo  yake katika mazoezi yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Boko Veterani,  jijini Dar es Salaam. Simba walifanya mazoezi hayo kujiandaa na mchezo wa Ligi […]

Ni vita Ngoma, Mwanjali Oktoba mosi

NA ZAITUNI KIBWANA ZIKIWA zimebaki siku chache ili tuweze kuona pambano la watani wa jadi, Simba na Yanga, homa ya pambano hilo inazidi kupanda kila kukicha. Ni mechi ambayo inavuta hisia za mashabiki na watu wengine kwa ujumla ambapo kwa mwaka huu kila timu inaonekana kujipanga kisawasawa kwa ajili ya kuibuka kidedea kwenye mchezo huo. Kuelekea mchezo huo utakaochezwa Oktoba […]