Category: Habari

BANDA AFICHUA SIRI YAKE NA OMOG

NA SAADA SALIM, BAADA ya kusota benchi kwa muda mrefu, kiraka wa Simba, Abdi Banda, anaamini mambo yatamwendea vizuri mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara, kwani tayari kocha wake, Joseph Omog amemwelewa. Akizungumza na BINGWA, Banda alisema atahakikisha anaingia kwenye kikosi cha kwanza cha Wekundu hao baada ya mzunguko wa kwanza kuwa mbaya kwa upande wake. Alisema anaamini kocha […]

JUMA LUIZIO AMCHAMBUA ‘MKATA UMEME’ WA YANGA

NA SAADA SALIM, MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Juma Luizio, aliyekuwa akikipiga katika klabu ya ZESCO United ya Zambia, aliyetua Simba kwa mkopo, amemchambua kiungo wa Yanga, Jastine Zulu, kwamba ni mchezaji mzuri, lakini anayetakiwa kupewa muda ili kujenga uhusiano na wenzake. Yanga imemsajili Zulu, ambaye amechukua nafasi ya Meshack Chaila, ambaye ilikuwa chaguo la kwanza la kocha George Lwandamina, […]

SIMBA YAIPIGA YANGA BAO LA FUNGA MWAKA

NA SAADA SALIM, SIMBA imezidi kuipiga bao Yanga baada ya kuwa wa kwanza kuzipokea Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC) za wachezaji wao wapya wa kigeni, Waghana Daniel Agyei (kipa) na James Kotei (kiungo), huku ile ya Mzambia, Justine Zulu wa watani wao hao wa jadi, ikiwasili jana mchana. Ikumbukwe kuwa, Yanga ndio waliokuwa wa kwanza kumleta Zulu nchini, lakini […]

NIYONZIMA, KAMUSOKO, ZULU WAREJESHA KAMPA KAMPA TENA JANGWANI

SAADA AKIDA NA HUSSEIN OMAR, INARUDI. Unaikumbuka Yanga ile iliyokuwa ikitoa dozi ya hadi mabao 7-0 katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara na hata zile za kimataifa? Kwa walioisahau, ilikuwa ni moto wa kuotea mbali, kutokana na kuwa na safu hatari ya kiungo iliyokuwa ikiwarahisishia kazi washambuliaji. Safu ya kiungo ya wakati huo, msimu wa 2013/14, ilikuwa ikiundwa na […]

LEGEND AMAINDI KANYE KUKUTANA NA DONALD TRUMP

NEW YORK, Marekani MWIMBAJI Jonh Legend, hana furaha na rafiki yake wa siku nyingi, Kanye West, baada ya rapa huyo kukutana na Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump. Rapa huyo maarufu alikutana na Trump kujadili masuala ya kitamaduni, ambapo baada ya kukutana aliendelea kusisitiza mpango wake wa kuwania urais mwaka 2024. Baada ya tukio hilo, msanii huyo mwenye umri wa […]

JOSHUA ANAAMINI AKIMPIGA WLADIMIR ATAKUWA RONALDO

MANCHESTER, England Bondia Anthony Joshua (AJ), amekusudia kuwa Cristiano Ronaldo wa masumbwi. Bingwa huyo wa uzito wa juu wa IBF, Joshua amekusudia kuwa gwiji wa masumbwi kama alivyo nyota wa Real Madrid na Ureno, Ronaldo. AJ amesema anaweza kuanza umaarufu wake kwa kumpiga mpinzani wake, Wladimir Klitschko, Aprili 29 mwakani. Joshua, mwenye umri wa miaka 27, atakumbana na bingwa wa […]

MCHEZAJI GOFU AISHANGAA TGU

NA SHARIFA MMASI MCHEZAJI wa gofu, Amani Said, aliyeshiriki mashiriki mashindano ya Nyali Open yaliyomalizika wiki hii,  jijini  Mombasa,  nchini Kenya, ameshangazwa na Chama cha Gofu Tanzania (TGU), kutokana na kutowapa ushirikiano. Amani, ambaye ni mchezaji wa Klabu ya Gymkhana ya jijini Dar es Salaam, alisema amekuwa hapati ushirikiano kutoka TGU, kitu ambacho kimesababisha kuiangusha Tanzania katika mashindano hayo. Alisema […]

KICHUYA: TUTAANZA UPYA MZUNGUKO WA PILI

NA WINFRIDA MTOI WINGA wa Simba, Shiza Ramadhan ‘Kichuya’, amesema wanatarajia kuanza upya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuhakikisha wanapata matokeo bora zaidi ili waweze kutimiza malengo yao ya  kuchukua ubingwa. Simba wataanza na Ndanda katika mchezo wa mzunguko huo, utakaochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, mkoani Mtwara, baada ya mzunguko wa kwanza kuibuka na […]

BEKI MPYA AZAM JEMBE

NA MAREGES NYAMAKA AZAM hawakufanya makosa kumsajili beki wa kigeni, Yakub Mohamed, kwani wameonekana kupata  jembe kutokana na kiwango cha hali ya juu alichokionyesha katika mazoezi ya timu hiyo, yanayoendelea kwenye uwanja wao wa Azam Complex,  jijini Dar es Salaam. Mohamed ni kati ya wachezaji wapya waliosajiliwa na klabu hiyo kwa ajili ya kuongeza makali katika kikosi chao kinachojiandaa na […]