Category: Habari

Aussems: Hata tucheze asubuhi, pointi tatu lazima

NA MWAMVITA MTANDA KOCHA wa Simba, Patrick Aussems, amesema pamoja na kubanwa na ratiba ya ligi kwa kucheza mechi kila baada ya siku tatu kufidia viporo vyao na kupangiwa kucheza mchana baadhi ya mechi, ameahidi kutoa dozi hata kama watacheza asubuhi. Simba, ambao wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Costal Union […]

Kampuni zilizoiingia mikataba na Kanumba, Majuto kuzilipa familia zao

Mwandishi Wetu Kampuni ya Steps Entertainment imeshamkabidhi Mama wa  muigizaji marehemu, Steven Kanumba malipo ya ziada ya Sh milioni 15 baada ya kugundulika kuwa iliingia mkataba mbovu na msanii huyo. Pia kampuni hiyo imeahidi kushirikiana na mama yake Marehemu Kanumba, kuandaa filamu ya maisha ya mwanawe huyo. Taarifa hiyo ilitolewa bungeni leo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, […]

Lulu: Hakuna ninachojutia kwenye maisha yangu

NA MWANDISHI WETU MWIGIZAJI nyota nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, amesema hakuna jambo  lolote analojutia kwenye maisha yake kwa kuwa yamemjenga na kuwa imara kama alivyo sasa. Akizungumza jana na kipindi cha XXL ya Clouds Fm, Lulu alisema anaamini katika mambo mazuri na mabaya aliyoyafanya yamekuwa na mchango mkubwa kwenye maisha yake ya sasa. “Kiukweli hakuna ninachojutia kwenye maisha yangu, sababu […]

MOTO CHINI Ni Liverpool v Barcelona, Ajax v Spurs nusu fainali

MANCHESTER, England NANI anakutana na nani katika hatua ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu imejulikana kufuatia matokeo ya mechi kali zilizochezwa usiku wa kuamkia leo. Tottenham Hotspurs walikuwa ni wageni wa Manchester City jana, mechi iliyochezwa kwenye dimba la Etihad, huku Liverpool ikishuka Estadio do Dragao kuchuana na FC Porto. Mechi hizo za marudiano hatua ya robo […]

Pele ‘arudi rasmi dimbani’ 

PARIS, Ufaransa NYOTA wa zamani wa Brazil, Pele, amewashukuru madaktari waliomtibu katika kipindi cha siku chache zilizopita, akiwahakikishia mashabiki wake kwamba yupo fiti ‘kurudi dimbani’ kwa sasa. Pele, mwenye umri wa miaka 78, alikuwa chini ya uangalizi wa wataalamu baada ya kukumbwa na maambukizi ya njia ya mkojo akiwa jijini Paris alipokuwa akishiriki hafla ya kibiashara. Mkongwe huyo alirejea nyumbani […]

AMEKUBALI Solskjaer ainua mikono juu, awapa Barca ubingwa UEFA

BARCELONA, Hispania KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, ameweka wazi imani yake kwa wababe wa Hispania, Barcelona, kuwa ndio watakaobeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu. Kauli hiyo ya Solskjaer, imekuja baada ya kushuhudia timu yake ya Man Utd iking’olewa na Barcelona kwenye robo fainali, kufuatia kichapo cha mabao 3-0 walichokipata katika mtanange uliochezwa usiku wa kuamkia […]

Ndayiragije aichokoza Simba

NA GLORY MLAY KOCHA wa KMC, Etienne Ndayiragije, amesema atatumia udhaifu wa Simba  kupata pointi tatu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa Aprili 26, mwaka huu, Uwanja wa Nyamagana, jijini Mwanza. Akizungumza na BINGWA jana, Ndayiragije alisema anaendelea kujipanga ili kuhakikisha wanaisimamisha Simba katika harakati zao za kutetea ubingwa msimu huu. Ndayiragije alisema pamoja na Simba kuwa timu […]

Majeruhi Kagera Sugar waanza mazoezi 

NA DAMIAN MASYENENE, MWANZA KIKOSI cha Kagera Sugar ya mjini Bukoba kiko kwenye mawindo makali tayari kuikabili Simba, ambayo imekuwa na mwendelezo mzuri wa matokeo katika michezo ya Ligi Kuu Bara, hata hivyo habari njema kwa Wana Nkurunkumbi ni kuanza mazoezi kwa baadhi ya nyota wake ambao walikuwa nje ya uwanja kutokana na majeruhi. Kagera Sugar ilipoteza michezo yake mitatu […]