Category: Habari

SERENGETI BOYS WAIBANA MALI

Libreville, Gabon TIMU ya Tanzania ‘Serengeti Boys’, imewabana mabingwa watetezi wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, Mali na kutoka nao sare ya 0-0, katika mchezo wa Kundi B uliopigwa jana Uwanja wa I’Amitie Sino-Gabonaise, mjini Libreville, nchini Gabon. Matokeo hayo yalikuwa muhimu sana kwa Serengeti Boys, ambao ndio walikuwa wanashiriki […]

SINGIDA UNITED WAMNASA KIBOKO WA YANGA

NA WINFRIDA MTOI KATIKA kuonyesha kwamba imepania kufanya kweli msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Singida United inamnyatia mkali wa kuibua vipaji anayezitesa Simba na Yanga, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Mexime, ili kusaidiana na Hans van Pluijm. Mexime, ambaye awali alikuwa akihusishwa na mpango wa kutua Yanga kuwa msaidizi wa George Lwandamia, inadaiwa hivi sasa dili hilo […]

HANSPOPE AREJESHWA USIKU WA MANANE

NA SAADA SALIM, MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, amerejea kundini ikiwa ni siku moja baada ya kutangaza kujiengua. Hans Poppe aliamua kujiuzulu nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili kwa madai ya viongozi wa Simba kutomshirikisha katika mkataba wa miaka mitano wa udhamini wa klabu hiyo kutoka kwa kampuni ya SportPesa. Lakini jana Pope alithibitisha […]

YANGA YANOGESHA UBINGWA

NA WAANDISHI WETU, YANGA hawataki utani, kwani baada ya kuona kila dalili za kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wameamua ‘kuwaroga’ zaidi wachezaji wao kwa kuhakikisha wanawalipa madeni yao yote ya mishahara kama sehemu ya kunogesha sherehe za ubingwa unaonukia Jangwani. Bila shaka hizo zitakuwa ni habari njema kwa wachezaji wa timu hiyo ambao walijikuta wakiwa katika wakati […]

KISIGA AMTAJA ‘KIRUSI’ ANAYEINYIMA SIMBA MATAJI

NA WINFRIDA MTOI, KIUNGO wa zamani wa Simba, Shaaban Kisiga, amefichua kile kinachoimaliza timu hiyo kuwa ni ukosefu wa mchezaji kiongozi kwenye kikosi hicho tofauti na watani zao Yanga. Akizungumza na BINGWA juzi, Kisiga ambaye kwa sasa anaichezea Ruvu Shooting, alisema Simba ni timu nzuri iliyosheheni nyota wengi lakini inakosa wachezaji  wazoefu wenye uwezo wa kuwaongoza wenzao katika mambo mbalimbali […]

MAVUGO, MO WAMKIMBIZA ATHANAS SIMBA

NA ZAINAB IDDY, STRAIKA wa Simba, Pastory Athanas,  amekubali yaishe baada ya kuweka wazi nia yake ya kuvunja mkataba na klabu hiyo. Meneja wa mchezaji huyo, Muhibu Kanu, ameliambia BINGWA kuwa  wamefikia uamuzi huo kutokana na kuwa na nafasi finyu aliyonayo mchezaji wake katika kikosi cha Wekundu hao. “Si jambo zuri kuona mchezaji anakosa nafasi ya kucheza kisha ukaendelea kumuacha […]

KIPA AFRICAN LYON AMSHANGAA MSUVA

NA JESSCA NANGAWE, KIPA namba moja wa African Lyon, Youthe Rostand, amemshangaa winga wa Yanga, Simon Msuva, kuendelea kucheza Bongo wakati ana hadhi ya kucheza Ulaya. Akizungumza na BINGWA, Rostand ambaye anadaiwa kuivutia Yanga na huenda akatua katika klabu hiyo msimu ujao, anaamini huu ni wakati wa Msuva kutimkia Ulaya kama anataka kukuza zaidi kiwango chake. “Tangu nije Tanzania nimeona […]