Category: Habari

MO DEWJI AWAFUNGIA KAZI BOSSOU, KAMUSOKO

NA EZEKIEL TENDWA BAADA ya kufanikiwa kuinasa saini ya Haruna Niyonzima huku pia zikiwapo taarifa za Donald Ngoma naye kuingia kwenye mikono ya Simba, Wekundu wa Msimbazi hao wanataka kupeleka kilio kingine Yanga wakitajwa kuitaka saini ya Thaban Kamusoko na beki Vincent Bossou. Simba wamefanikiwa kuinasa saini ya Niyonzima baada ya Yanga kutangaza wazi kushindwa dau lake huku pia Ngoma […]

MINZIRO: TUNAENDELEA KUFANYA USAJILI WA HAJA

NA MAREGES NYAMAKA, BENCHI la Ufundi kwa kushirikiana na uongozi wa Singida United, wamebainisha kuwa bado wana nafasi ya kuendelea kufanya usajili wa nguvu kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Singida United iliyorejea Ligi Kuu Bara, ilianza usajili wao kwa kunasa saini ya mshambuliaji na mfungaji bora wa Rwanda, Danny Usingemana, kutoka Polisi FC ya nchini humo na […]

SINGANO AOMBA KURUDI SIMBA

NA MWANDISHI WETU MSHAMBULIAJI wa Azam,  Ramadhani Singano, amewatumia wapambe ili waweze kumwombea msamaha wa kurejea katika kikosi cha Simba kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Hatua ya Singano kutumia wapambe kuwaomba msamaha viongozi wa Simba inatokana na uondokaji wake ndani ya klabu hiyo, ambaye alionekana kuwakera Wekundu hao wa Msimbazi. Singano aliondoka Simba katika misimu miwili iliyopita […]

KAGERA WAIKATA MAINI YANGA

NA JESSCA NANGAWE, KLABU ya Kagera Sugar imewakata maini Yanga baada ya kocha wao, Mecky Mexime, kuongozewa mkataba wa mwaka mmoja ili aweze kuendeleza majukumu ya kuifundisha timu yao kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Yanga walitega ndoana kwa kutaka kumchukua Mexime ili aweze kuwa kocha msaidizi wa George Lwandamina baada ya Juma Mwambusi kubakisha siku chache mkataba […]

MKUDE: NIYONZIMA? WATATUKOMA BASI

NA ZAINAB IDDY, UJIO wa kiungo mchezeshaji, Haruna Niyonzima kwenye klabu ya Simba, umemfurahisha nahodha wa timu hiyo, Jonas Mkude, kwamba itakuwa poa sana kucheza na nyota huyo wa Rwanda. Tayari uongozi wa Yanga umekiri kushindwana na Niyonzima, ambaye tayari amedaiwa kusaini mkataba wa miaka miwili na Simba na msimu ujao atatinga uzi mwekundu. Akizungumza na BINGWA jana, Mkude amesema […]

NGOMA, OKWI KUMALIZANA NA SIMBA KESHO

NA ZAITUNI KIBWANA, HIKI wanachokifanya Simba kipindi hiki cha dirisha kubwa la usajili wa Ligi Kuu Tanzania Bara sasa ni sifa na Mungu anawaona. Baada ya kupeleka kilio kwa mahasimu wao, Yanga kwa kumnasa kiungo Haruna Niyonzima, sasa Wekundu hao wa Msimbazi wanataka kuzidisha machungu kwa mshambuliaji wa klabu hiyo ya Jangwani, Donald Ngoma. Pamoja na Ngoma, ambaye wengi hawajui […]

YANGA WAKUBALI YAISHE

NA ZAITUNI KIBWANA HATIMAYE Yanga wamesalimu amri kwa Simba, baada ya mpango wa kumbakisha Jangwani kiungo wao, Haruna Niyonzima kukwama. Tangu kuwapo kwa taarifa za Niyonzima kusaini Simba, Yanga walikuwa wakihangaika kufanya mapinduzi, lakini dau alilopewa mchezaji huyo wa Rwanda na Wekundu wa Msimbazi lilikuwa kubwa kwa klabu hiyo ya Jangwani. Kiungo huyo aliyetua Yanga mwaka 2011 akitokea APR ya […]

DIDA AITISHA YANGA, AZAM YATAJWA

NA ZAINAB IDDY MLINDA mlango wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’, ameiweka klabu yake roho juu, baada ya kukataa kuongeza mkataba mpya hadi atakaporejea kutoka Afrika Kusini kwenye majaribio. Wakati Dida akitoa maamuzi hayo, taarifa zinasema kwamba huo ni mpango wa Azam FC kutaka kumnasa kipa wao huyo wa zamani. Azam imefikia maamuzi hayo kwa kile kinachodaiwa kuhitaji wachezaji wenye uzoefu […]

KIGOGO SIMBA AMFUATA BEKI GHANA

NA ZAITUNI KIBWANA KLABU ya Simba imedhamiria makubwa msimu ujao, ambapo kwa sasa wanataka kuelekeza nguvu zao nchini Ghana kunasa beki wa kati. Wekundu wa Msimbazi wamemtuma Meneja wao, Abasi Ali, kwenda Ghana kwa ajili ya kushiriki harusi ya kiungo wao, James Kotei, ambaye amewatonya kwamba kuna beki bab kubwa anafaa kuichezea klabu hiyo. Kotei ambaye mkataba wake unakaribia kumalizika, […]

MBEYA CITY KUNASA SAINI YA STRAIKA PRISONS

NA SELEMANI MAJEMA (DSJ) MSHAMBULIAJI wa Tanzania Prisons, Victor Hangaya, anatarajiwa kusaini mkataba katika klabu ya Mbeya City kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Akizungumza na BINGWA jana, Hangaya alisema kwa sasa yupo kwenye mazungumzo na Mbeya City ambao wameonyesha nia ya kufanya naye kazi kwa msimu ujao. Hangaya alisema baada ya kumaliza kuitumikia klabu yake ya zamani […]